Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Uwanja wa siasa nchini Marekani umezidi kuchangamka na hii ni baada ya mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump, hivi karibuni kusema kuwa hata kama humpendi yeye kama yeye ni muhimu sana kumpigia kura.
Trump aliyasema hayo kwenye jimbo la Pennsylvania huko nchini Marekani akiwa kwenye kipindi special cha Trump Townhall pale Fox News.
Rais huyo wa zamani alidokeza kuwa wamarekani "have no choice" na kwamba haijalishi unampenda au humpendi, anachohitaji ni kura yako tu.
Zikiwa zimebaki takribani siku 60 mpaka uchaguzi wa Marekani kufanyika, Trump yuko kwenye ushindani na mzito na Kamala Harris ambaye anawakilisha chama cha Democrats.
Unaionaje kauli hii ya Bwana Trump? Unadhani maji yamefika shingoni ndo maana anatoa kauli kama hizi au upepo bado upo upande wake?
Nawasilisha.
Soma pia: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu Marekani 2024: Nani kuibuka kidedea?

"You have no choice, you've gotta vote for me ........ even if you don't like me"