sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Mashindano ya Kombe la FA yanarejea tena, baada ya kupotea kwa miaka 13.. na sasa yatajulikana kama Kombe la Shirikisho.
Zifuatazo ni dondoo kadhaa kuhusu michuano hii.
1. Ni timu zipi zinatakiwa kushiriki?
Timu zinazoshiriki michuano hii, ni;
Timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Timu zote za Ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Timu zote za Ligi daraja la Pili Tanzania Bara.
Mfumo wa mashindano ni upi?
Mashindano ya FA yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo timu inayoshinda inaenda raundi inayofuata. Mfumo huu ni kama ule wa kombe la FA la Uingereza.. Mashindano yataanza na preliminary rounds, ambapo timu za ligi ya chini huanza kupunguzana.. Baada ya hapo kutakua na Draw ambayo itazihusisha sasa timu za ligi kuu.
Bingwa wa kombe la FA atapata nini?
Big prize ni Mshindi kufuzu moja kwa moja kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Africa.. Kuhusu mkwanja itategemea na wazamini wataweka kiasi gani mezani. Pia Bingwa atapata Kombe.
Michuano hii itaanza lini?
Kuanzia November 2015, timu mbali mbali zitakuwa zikipambana kumuwania huyu mwali.
Ombi langu kwa TFF, kupitia kwa Bodi ya Ligi ambao ndio wasimamizi wa michuano hii.. wajitahidi yasijirudie ya msimu uliopita, mwaka huu wafanye kweli michuano hii iwepo.