Dondoo Kadhaa kuhusu Kombe la FA, Tanzania.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mashindano ya Kombe la FA yanarejea tena, baada ya kupotea kwa miaka 13.. na sasa yatajulikana kama Kombe la Shirikisho.
Zifuatazo ni dondoo kadhaa kuhusu michuano hii.

1. Ni timu zipi zinatakiwa kushiriki?
Timu zinazoshiriki michuano hii, ni;
• Timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara.
• Timu zote za Ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara.
• Timu zote za Ligi daraja la Pili Tanzania Bara.

Mfumo wa mashindano ni upi?
• Mashindano ya FA yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano, ambapo timu inayoshinda inaenda raundi inayofuata. Mfumo huu ni kama ule wa kombe la FA la Uingereza.. Mashindano yataanza na preliminary rounds, ambapo timu za ligi ya chini huanza kupunguzana.. Baada ya hapo kutakua na Draw ambayo itazihusisha sasa timu za ligi kuu.

Bingwa wa kombe la FA atapata nini?
• Big prize ni Mshindi kufuzu moja kwa moja kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Africa.. Kuhusu mkwanja itategemea na wazamini wataweka kiasi gani mezani. Pia Bingwa atapata Kombe.

Michuano hii itaanza lini?
• Kuanzia November 2015, timu mbali mbali zitakuwa zikipambana kumuwania huyu mwali.

Ombi langu kwa TFF, kupitia kwa Bodi ya Ligi ambao ndio wasimamizi wa michuano hii.. wajitahidi yasijirudie ya msimu uliopita, mwaka huu wafanye kweli michuano hii iwepo.
 
Mshindi atafuzu kucheza kombe la shirikisho...
Kuna timu zitapotea mazima ktk ramani ya soka tz
 
Hata mi nishaliona hilo.. Shime TFF fanyeni juu chini hii michuano iwepo.
 
Simba bye bye kupanda ndege.

Kombe la vpl hamlipati
Fa pia

Mkuu Deo, ushauri wangu wa mapema kwa Ndugu Evance Aveva.. achonge kabisa kabati lingine kwa ajili ya kuhifadhi makombe ya msimu ujao.. Maana..
1. Kombe la Ligi
2. Kombe la FA
3. Kombe la Mtani Jembe
4. Kombe la Muungano
5. Ngao ya Jamii.
... yote haya yanaelekea mtaa wa Msimbazi, ni suala la mda tu.
 
..hizi mechi za mtoano ndio zinamfaa mnyama, ngoja ilo kombe lao lianze...na wale wanaosema mnyama bye bye mashindano mngejua hapo ndio mmejiingiza kingi wenyewe mngetulia tuli.
Msimu uliopita mnyama kachukua pointi nyingi kwa "kandambili" na "lambalamba",mi nasema WALETE.
 
Naomba kuuliza kwa mfano ikatokea Yanga kashinda ligi kuu kama kawaida yake na pia kashinda hili la shirikisho kwa hiyo mashindano yote atashiriki na atapanda ndege peke yake au itakuwaje?
 
Hapo unatakiwa uulize hivi..

"Naomba kuuliza baada ya Simba kushinda ligi kuu
kama kawaida yake na pia kashinda hili la shirikisho kwa hiyo
mashindano yote atashiriki na atapanda ndege peke yake au
itakuwaje?"

Jibu ni.. Timu itakayokua mshindi wa pili wa kombe la FA ndo itapanda ndege.
 
Hahaha haya mzee wa Mtani Jembe ila siku hizi Mmeshuka thamani Hadi wenzenu wa DOKTA MWAKA NDONDO CUP Wamewatenga. Poleni sana
 
Mkuu Deo, ushauri wangu wa mapema kwa Ndugu Evance Aveva.. achonge kabisa kabati lingine kwa ajili ya kuhifadhi makombe ya msimu ujao.. Maana..
1. Kombe la Ligi
2. Kombe la FA
3. Kombe la Mtani Jembe
4. Kombe la Muungano
5. Ngao ya Jamii.
... yote haya yanaelekea mtaa wa Msimbazi, ni suala la mda tu.

mkuu ngoja niitunzee hii kauli yako ntakuwa nakukumbusha tu mie
 
Hapo unatakiwa uulize hivi..

"Naomba kuuliza baada ya Simba kushinda ligi kuu
kama kawaida yake na pia kashinda hili la shirikisho kwa hiyo
mashindano yote atashiriki na atapanda ndege peke yake au
iitakuwaje?"

Jibu ni.. Timu itakayokua mshindi wa pili wa kombe la FA ndo itapanda ndege.

mkuu naomba nieleweshwe maana ya hiyo kauli yako ya kama simba atashinda ligi kuu kama KAWAIDA YAKE,,unamaana gan hapo au unamaaniaha kushinda nafasi yenu ya nne ligi kuu kama kawaida yenu?????
 
Naomba kuuliza, hivi mshindi wa mtani jembe na mapinduzi cup atawakilisha kombe gani afrika?
 
Mkuu hapo nazumgumzia ile Simba SC ya 2011/12.. nadhani unaikumbuka?! Sasa imerudi kivingine chini ya Watalamu wenye leseni za juu kabisa katika Professional zao, Dylan Kerr na Momcilovic.
 
Naomba kuuliza, hivi mshindi wa mtani jembe na mapinduzi cup atawakilisha kombe gani afrika?

Hawakilishi chochote Mkuu, ila anapata mkwanja mzuri tu na kujaza kabati lake Makombe.
 
Na hiyo "fa" ndiyo nini?! Kama kuna tff! Au ni kuiga iga tu kwa kuwa liko pia uingereza?!
 
Back
Top Bottom