Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,772
- 22,598
Kufanya kazi ni sehemu ya maisha ya binadamu yeyote. Mtu asipofanya kazi huugua kwasababu mwili unashindwa kujiendesha na kuzalisha seli mpya ambazo zinatakiwa zitumike. Kwa kila anayefanya kazi huchoka na huitaji mapumziko.
Mapumziko huwa wakati wa usiku ambapo mtu huacha kila kitu na kupanda kitandani kulala ili kuurudisha mwili katika hali ya kawaida. Wapo watu wakifika kitandani wanakosa usingizi kabisa au wengine wanachelewa kupata usingizi. Wataalamu wa afya wanashauri mtu kulala masaa 6 hadi 8 kwa usiku mmoja ili kuufanya mwili kuwa na afya bora.
Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 25 ya watu wazima wanasumbuliwa na matatizo ya usingizi na asilimia 6 hadi 10 wanasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.
Imewalazimu baadhi ya watu kutumia vidonge vya usingizi lakini bado tatizo haliishi. Baadhi ya tabia ambazo zinasababisha mtu akose usingizi, husababishwa na mabadiliko ya mazingira ya sehemu ya kulala kama vile kuwa kwenye mazingira ya baridi kali, moshi au harufu mbaya.
Sababu nyingine ni mabadiliko ya muda wa kulala tofauti na mtu alivyozoea. Lingine ni makelele katika maeneo ya makazi, muziki wenye midundo mizito na sauti ya juu au vurugu. Mambo mengine ni msongo wa mawazo, wasiwasi, woga na hofu zitokanazo na matatizo ya kimaisha kama vile kukosa fedha, matatizo ya kifamilia na ugomvi wa wanandoa .
Zingatia mambo yafuatayo ili upate usingizi wa kutosha na wenye uhakika:
Epuka kuangalia runinga (TV) au kusikiliza radio ukiwa kitandani utakuchukua muda mrefu kupata usingizi. Jaribu kadri uwezavyo kukifanya chumba cha kulala kuwa na mazingira yanayovutia kupata usingizi.
Ukiruhusu akili yako kufikiri hayo utakosa usingizi na utaingiwa na wasiwasi na kuhofia matukio hayo kujirudia tena usiku. Fahamu mambo yaliyotokea hayawezi kutokea tena, pia jitathmini mwenyewe uko wapi na unafanya nini kwa wakati huo.
Kumbuka dondoo hizi ni njia rahisi zitakazokusaidia kupata usingizi wa uhakika. Ikiwa baada ya kutumia njia hizo hapo juu bado unakosa usingizi, muone daktari akusaidie kwa matibabu zaidi.
http://www.fikrapevu.com/dondoo-muhimu-ili-kupata-usingizi-wa-uhakika/
Chanzo: fikrapevu.com

- Lala kwa muda muafaka
- Epuka mazoezi muda mfupi kabla ya kulala
- Usitumie eneo la kulala kwa shughuli nyingine
Epuka kuangalia runinga (TV) au kusikiliza radio ukiwa kitandani utakuchukua muda mrefu kupata usingizi. Jaribu kadri uwezavyo kukifanya chumba cha kulala kuwa na mazingira yanayovutia kupata usingizi.
- Jiandae kisaikolojia
Ukiruhusu akili yako kufikiri hayo utakosa usingizi na utaingiwa na wasiwasi na kuhofia matukio hayo kujirudia tena usiku. Fahamu mambo yaliyotokea hayawezi kutokea tena, pia jitathmini mwenyewe uko wapi na unafanya nini kwa wakati huo.
- Epuka kunywa pombe, kahawa na tumbaku kabla ya kulala