Dondoo za masomo ya PhD UDSM

Dondoo za masomo ya PhD UDSM

Tundazuri

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Posts
1,932
Reaction score
2,525
Napenda kuwasapa salamu rafiki zangu.

Kama nilivyosema hapo juu kuhusu dondoo za masomo ya ngazi ya PHD katika chuo cha UDSM.

Nimekuwa nikipata ukakasi wa kwenda kusoma hapo kwa kushauri kwamba bora nikasome Ardhi University kuliko UDSM kwa sababu ya usumbufu.

Usumbufu wenyewe ni kwamba unaweza ukawa uko speed kuandika lakini ukawa unakwamishwa kwenye comments kutoka kwa supervisor na kujikuta unachelewa. Mfano, baadhi ya watu niliowauliza wanasema wamekuwa wakituma andiko lao kwa supervisor na kujikuta wanakaaa hata miezi bila kupata feedback na kubaki wanahang tuu.

Kitu kingine unaweza, ukapata comments kutoka kwa supervisor ila ukija kwenda kwa discussant unabadilishiwa muelekeo wa study yako, au unaweza kwenda kwenye study committee nako ukakutana na kadhia zake na kujikuta hata kama unabidii kwenye kufanya PHD yako lazima tu utachelewa kumaliza.

Nimesikia kuna walaka kwamba wale ambao watamaliza miaka yao ya masomo lakini bado hujagraduate basi utalipa ada nzima ambapo kwa kuchekecha akili yamkini supervisor au hao wanaopitia paper yako wanaweza kuwa ndio chanzo cha kukufanya usimalize kwa wakati. Lakini kama ni kwa uzembe wako mwenyewe unapaswa kufanya hivyo maana unakuwa mwenyewd umejichelewesha.

Nimeandika huu uzi ili niweze kupata ushauri maana nimepata chuo zaidi ya kimoja UDDM ikiwa ni kimoja wapo kusoma PHD.

Naombeni dondoo zenu mliopitia au mnaosoma hapo wapendwa.

Ahsanteni.
 
SUA ni hatari Masters tu hutagraduate on time hata kama uko hard working utacheleweshwa mno, kupangiwa presentation tu ni kazi hadi wajiskie
Sua wanasumbua sanaa, bora UDOM, nina ndugu yangu kasoma Master utadhani anasoma PHD ya miaka mitano, supervisor anamwambia hivi akirekebisha anaenda anabadilsha eti nilikuambia hv, yaan kuna siku ndio nilichoka alimwambia nasafiri nikirudi tutadiscuss, sasa ww umsubiri mtu na kazini umepewa likizo ya masomo sasa si ujinga huu, nawashauri watu ni bora ukaangalia chuo cha kusoma ambacho hakitakupa stress
 
Mkeka wa graduates wa mwaka huu huo wa SUA soma registration number uone walikuwa registered mwaka gani. Watu wamesoma masters 3 to 4 years, kuna PhD graduates wawili apo walikuwa registered 2017 wamesoma 7 years. Japo elimu ya PhD hata masters pia ni kipimo cha resilience usiogope kwenda SUA.
SUA ni hatari Masters tu hutagraduate on time hata kama uko hard working utacheleweshwa mno, kupangiwa presentation tu ni kazi hadi wajiskie
Screenshot_20241003-114636_1.jpg
 
Sua wanasumbua sanaa, bora UDOM, nina ndugu yangu kasoma Master utadhani anasoma PHD ya miaka mitano, supervisor anamwambia hivi akirekebisha anaenda anabadilsha eti nilikuambia hv, yaan kuna siku ndio nilichoka alimwambia nasafiri nikirudi tutadiscuss, sasa ww umsubiri mtu na kazini umepewa likizo ya masomo sasa si ujinga huu, nawashauri watu ni bora ukaangalia chuo cha kusoma ambacho hakitakupa stress
Kusoma SUA kunataka moyo sana na navyosikia na UDSM pia
 
Mkeka wa graduates wa mwaka huu huo wa SUA soma registration number uone walikuwa registered mwaka gani. Watu wamesoma masters 3 to 4 years, kuna PhD graduates wawili apo walikuwa registered 2017 wamesoma 7 years. Japo elimu ya PhD hata masters pia ni kipimo cha resilience usiogope kwenda SUA.

View attachment 3113998
Kusoma kwa mateso maana yake nn? Bora usome umalize uendelee na mipango mingine habari za kuchoshana na kukimbizana kuviziana inaumiza akili
 
Back
Top Bottom