Labda nitoe maelezo kidogo ya VPN, naona kuna wasomaji wengi wanauliza kwa kutofahamu matumizi yake. VPN maana yake ni Virtual Private Network, matumizi yake haswa ni kutumia network nyingine badala ya ile uliyonayo. Nitatoa mfano, uko TZ lakini unaweza browse internet/mtandao kama mtu alieko US au mahali mengine. Au kwa mfano uko nyumbani ukatumia internet kama vile uko ofisini n.k.
Lengo lake kwa mfano kama kuna firewalls zinazotumia IP, kwa hio IP ya office ina access lakini sio za nyumbani. Kwa hio wafanyakazi wote wakiwa nyumbani wanaconnect kwa kupitia VPN n.k.
P:S
- Sidhani kama VPN ni kosa la jinai, pengine kwa TZ wengi watakuwa wanatumia kuongeza privacy au protection ya kuwa identified. I hope this info helps.