Donnie Yen hazeeki

Donnie Yen hazeeki

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
images - 2023-04-07T225504.893.jpeg

Umeitazama muvi ya John Wick Chapter 4? Humo utakutana na mtaalamu Donnie Yen kacheza kama kipofu aaitwaye. Ni noma sana humo ndani kakiwasha balaa.

Donnie Yen ana miaka 59 sasa anaelekea 60 lakini muonekano wake utadhani ana miaka 40s. Sio kama wenzake Vincent Zhao, Andy lao, Yuen Biao, Jack Chan, Jet lee (huyu kidogo maradhi yamemzoofisha). Bado yuko fit kabisa kuliko beki kisiki wa msimbazi Josh Onyango😅

Kibongo bongo ukiwa na umri huo tayari ushakua babu unajiandaa kufa.

images - 2023-04-07T225603.077.jpeg

Ni kama huyu mbabu wa kihindi Anil Kapur unaweza kujua anakua kwa kurudi nyuma. Ukiangalia muvi zake za 90s alikua anamuonekano wa kizee ila miaka inavyozidi kwenda anaonekana kijana. Kwasasa ana miaka 66.

images - 2023-04-07T225145.507.jpeg

[Anil Kapur aliyevaa viatu vya pink, Huyo binti ni mtoto wake, mwanaume aliye kulia kwake kajishika mkono ni mume wa binti yake]
 
Daah hata mi nilikuwa najiuliza huyu jamaa hazeeki ukilinganisha na wenzake akina Yuen Biao , Jackie Chan , Samo hung, hata Jetli anaonekana age imeenda ila mwamba still yupo imara sana , spendi movie zake za mapanga , visu na mafarasi napenda zile za town na mafia a.k a drug dealer akiwa kama afisa upelelezi utapenda , alafu viwemo vyuma vya kutosha
 
Ongezea View attachment 2580330
Na huyuuu sijui wanatumia nin hawa watu
Huyu ndio vampire sasa sijui anakulaga nini?? Anaitafuta 70 jamaa
Mimi nahisi ni maumbile ya mtu tu.

Mwingine ni Paul Rudd (Ant-Man) nae ana sura ya kutokuzeeka. Mwangalie Mark Rufallo(Hulk) anaonekana mzee kuliko yeye.

Nilishangaa sana kusika Kanumba alikua na miaka 28🤔

1680901945858.png
 
Daah hata mi nilikuwa najiuliza huyu jamaa hazeeki ukilinganisha na wenzake akina Yuen Biao , Jackie Chan , Samo hung, hata Jetli anaonekana age imeenda ila mwamba still yupo imara sana , spendi movie zake za mapanga , visu na mafarasi napenda zile za town na mafia a.k a drug dealer akiwa kama afisa upelelezi utapenda , alafu viwemo vyuma vya kutosha
Jack Chan na Yuan Biao hawa rika moja, ila Samo Hung ni rika la aina Sylvester Stallone, Anold Schwarzenegger, Stephen Cheung nk. Jet lee ni rika sawa Donnie au Jack Ma ila yeye malazi yake yamemchokesha
 
Huyu jamaa hata mwenyewe ananiacha sana njia panda

Ukicheki umri wake halafu ukaangalia na age mate wenzake kina Jet li na Jack Chan unaona kabisa jamaa ni kama immortal
Jack chan sio agemate wa Donnie wala Jet lee. Jack kaanza kuigiza 70s na Bruce ila akina Jetlee wamekuja miaka 80katikati. Leo jack katimiza 69yr wakati donie mwezi wa 7 anatimiza 60.

Mazoezi na kutokua na maradhi + maumbile tu ya mwili wake yamembeba kua hivyo.
 
Jack Chan na Yuan Biao hawa rika moja, ila Samo Hung ni rika la aina Sylvester Stallone, Anold Schwarzenegger, Stephen Cheung nk. Jet lee ni rika sawa Donnie au Jack Ma ila yeye malazi yake yamemchokesha
Wheels-on-Meals.jpg

Hii Combination ilikuwaga fire sana, sidhani kama China/Hong kong itashuhudia kizazi bora cha martial art kama hiki
 
Jack chan sio agemate wa Donnie wala Jet lee. Jack kaanza kuigiza 70s na Bruce ila akina Jetlee wamekuja miaka 80katikati. Leo jack katimiza 69yr wakati donie mwezi wa 7 anatimiza 60.

Mazoezi na kutokua na maradhi + maumbile tu ya mwili wake yamembeba kua hivyo.
pia mwamba ni master of kungfu in real life
 
View attachment 2580342

Hii Combination ilikuwaga fire sana, sidhani kama China/Hong kong itashuhudia kizazi bora cha martial art kama hiki
Kuna kitu inaitwa Millionaire Express, Wheel in Meals, Project A ni nomasana. Ila Sammo Hung ni director mzuri sana huwezi amaini ndio aliandaa kitu cha Estern Condors. Nataka siku moja nikusanye muvi zao zote maana KIX hua zinaonyeshwa mara chache
 
Back
Top Bottom