View attachment 2580252
Umeitazama muvi ya
John Wick Chapter 4? Humo utakutana na mtaalamu Donnie Yen kacheza kama kipofu aaitwaye. Ni noma sana humo ndani kakiwasha balaa.
Donnie Yen ana miaka 59 sasa anaelekea 60 lakini muonekano wake utadhani ana miaka 40s. Sio kama wenzake Vincent Zhao, Andy lao, Yuen Biao, Jack Chan, Jet lee (huyu kidogo maradhi yamemzoofisha). Bado yuko fit kabisa kuliko beki kisiki wa msimbazi Josh Onyango😅
Kibongo bongo ukiwa na umri huo tayari ushakua babu unajiandaa kufa.
View attachment 2580250
Ni kama huyu mbabu wa kihindi Anil Kapur unaweza kujua anakua kwa kurudi nyuma. Ukiangalia muvi zake za 90s alikua anamuonekano wa kizee ila miaka inavyozidi kwenda anaonekana kijana. Kwasasa ana miaka 66.
View attachment 2580258
[Anil Kapur aliyevaa viatu vya pink, Huyo binti ni mtoto wake, mwanaume aliye kulia kwake kajishika mkono ni mume wa binti yake]