Naweka kiswahili kwa ajili ya Badili Tabia na wengineo poleni sana baadhi yetu tumejizoeza kupita kiasi na hii lugha ya wageni..
Ni hivi ''nilikuwa nina uhusiano msichana fulani kipindi cha nyuma kidogo.Nilimpenda kwa kuwa alikuwa wa kwanza kwangu lakini alikuwa na mazoea ya kunitishia kauli ya 'naomba tuachane' ili kuniogopesha au kunitikisa kidogo.
Ikafika siku na mimi nikachoshwa na huo mchezo nikamwambia mimi na wewe basi,mara ya kwanza alidhani ninafanya mzaha lakini baadaye alikuja kutambua nilimaanisha nilichokisema.Napenda wanawake wanaojua wanachokihitaji maishani mwao.Lakini pia ni wazi wanawake huwatenda wapenzi wao kama tu wanaume wafanyavyo.Kama unaye umependaye tafadhali mtunze na mthamini kabla haijawa kuchelewa mno.Nawatakia heri wote humu MMU''