Wakuu
=====
Hizi taarifa niza kweli kwamba Dorothy Semu ametimuliwa kimya kimya ndani ya ACT Wazalendo?
=====
Hizi taarifa niza kweli kwamba Dorothy Semu ametimuliwa kimya kimya ndani ya ACT Wazalendo?
- Tunachokijua
- Dorothy Semu ni mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo ambaye pia Aprili 22, 2025, alichukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 ambapo baada ya kuchukua fomu hiyo Semu alisema,
"Nimechukua fomu hii kama ishara ya utayari wangu wa kumkabili Rais Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu wameshindwa kuendesha nchi na kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii,"
Aidha kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na ACT Wazalendo Agosti 06, 2025 ilieleza kuwa halmashauri kuu ya chama hicho ilipokea na kuridhia hatua ya Dorothy Semu kujitoa kugombea nafasi ya Urais.
Baadaye mkutano mkuu maalum wa ACT Wazalendo ulimchagua Luhaga Mpina aliyetokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo.
Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni inayodai kuwa Dorothy Semu aondolewa ACT Wazalendo na kusema mageuzi ni kwa wanaume pekee.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Afisa Kitengo cha Mawasiliano cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis amekanusha taarifa hiyo na kusema,
"Dorothy ni sehemu ya Viongozi wa ACT Wazalendo ambao mpaka muda huu wanapambana kuona haki ya Luhaga Mpina na ACT Wazalendo kuwa na Mgombea Urais inapatikana. Hiyo yaarifa siyo ya kweli."
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu imebainika grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani hazijachapishwa na vyombo hivyo (Global TV, Clouds Media na The Chanzo) kama inavyoonekana.
Aidha grafiki hizo zimebainika na mapungufu kadhaa ikiwemo, matumizi ya fonti zisizotumiwa na vyombo hivyo, makosa ya kiuandishi jambo linalodhihirisha kuwa ni za kughushi.