Dorothy Gwajima: Shikaneni mabega tuone kama Nyeti zinapotea, huu ni uongo

Dorothy Gwajima: Shikaneni mabega tuone kama Nyeti zinapotea, huu ni uongo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amekemea uzushi unaoenezwa na baadhi ya watu wenye nia ya kupotosha jamii kuwa mwanaume akishikwa bega hupoteza sehemu zake za siri (Nyeti).

Dkt. Gwajima amekemea uzushi huo wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto Anayeishi na Kufanya Kazi Mtaani yaliyofanyika katika Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, yaliyolenga kuhamasisha ulinzi, malezi na ustawi wa watoto. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mhe. Angelah Kairuki, Mbunge wa Kibamba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na viongozi wa kisekta, mkoa, wilaya na wadau wa maendeleo.

Baada ya kuongea mambo ya msingi, wamekazana na huo upuuzi usiokuwa na ushahidi wowote.
 
1769242001865.jpg
 
Baada ya kuongea mambo ya msingi, wamekazana na huo upuuzi usiokuwa na ushahidi wowote.
Mama hana baya
Jamii imegawanyika kuhusiana na hili Sakata
Watu wanapigwa(kama video nnazo ona nizakweli)
Nambaya zaidi kuna wasomi wanaamini hili jambo kua lipo kweli mifano ninayo
Sasa sirikali wanyamaze watu wauane nakuumizana au watoe muongozo kuhusiana na hili suala
 
Toka mwanzo hili suala kama lingepuuzwa ilikuwa rahisi sana kusahaulika, kutoka na kwa kiongozi na kulizungumzia, tegemea hali kuwa mbaya zaidi ya awali.
 
Toka mwanzo hili suala kama lingepuuzwa ilikuwa rahisi sana kusahaulika, kutoka na kwa kiongozi na kulizungumzia, tegemea hali kuwa mbaya zaidi ya awali.
Unapuuziliaje jambo ambalo liwe lakweli ama sio lakweli linapoteza ama kuumiza maisha ya watu???
 
Back
Top Bottom