Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Ndugu, Dorothy Semu, leo 17 Septemba, 2024 akiwa safarini kuelekea Jimbo la Rombo amepita Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga kwenye kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga, Askofu Chediel Sendoro ambaye alifariki tarehe 9 Septemba, 2024 kwa ajali ya Gari.
Kiongozi wa Chama amesaini kitabu Cha Wageni na kukutana na Katibu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mwanga Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Ndugu, Mathias Kanyika Msemo kumpa salaam za pole kwa niaba ya chama Cha ACT Wazalendo.
Kiongozi wa Chama yuko ziarani Mkoani Kilimanjaro ya ujenzi wa chama na kuzungumza na Wananchi.