PreGE2025 Dorothy Semu: Hatutaki kubaki kimya mbele ya kanuni kandamizi, lazima kuwe na rekodi kwamba tulipinga

PreGE2025 Dorothy Semu: Hatutaki kubaki kimya mbele ya kanuni kandamizi, lazima kuwe na rekodi kwamba tulipinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kuwa kitafungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya kanuni za maadili ya uchaguzi ambazo kinaamini zinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikisema lengo ni kutafuta tafsiri sahihi ya haki za wananchi kisiasa.

“Chama cha siasa ni mdau, lakini yule mwananchi ambaye yupo chini ya hicho chama analindwa kikatiba na ana haki zake za msingi. Tunafikiri baadhi ya kanuni zinavunja Katiba na tunakwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya kikatiba. Hatutaki kubaki kimya mbele ya kanuni kandamizi, lazima kuwe na rekodi kwamba tulipinga,” ameeleza Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu akizungumza wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa majimbo ya ACT Wazalendo wa Kanda za Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika Makambako, mkoani Njombe,

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya kisheria haiwaondoi ACT Wazalendo katika mazungumzo ya kisiasa, kwani chama hicho kinaendelea kushiriki mazungumzo kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) pamoja na makongamano mbalimbali ya kitaifa kwa lengo la kusisitiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
 
Kwanini walizisaini kama zinachangamoto? ACT wanaturudisha nyuma sana
 
images.jpeg
 
Back
Top Bottom