GE2025 Dorothy Semu: Mpina akigombea tutashinda, tuna imani na uwezo wake

GE2025 Dorothy Semu: Mpina akigombea tutashinda, tuna imani na uwezo wake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, amesema chama hicho hakina wasiwasi kuhusu muda uliosalia kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, endapo Luhaga Mpina ataruhusiwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dorothy amezungumza hayo leo, Septemba 29, 2025, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu jijini Dodoma, mara baada ya kuunguruma kwa shauri la kikatiba lililofunguliwa na Luhaga Mpina pamoja na chama chake cha ACT-Wazalendo dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuhusu kupinga uamuzi wa kumwondoa Mpina kugombea Urais.

Katika shauri hilo, lililosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu – Jaji Fredrick Manyanda, Jaji Abdallah Gonzi na Jaji Sylvester Kainda – Mahakama imeamuru upande wa waleta maombi kuwasilisha hoja kwa maandishi ndani ya siku mbili kuanzia leo, huku wajibu maombi wakitakiwa kuwasilisha majibu yao kwa maandishi pia.

Shauri hilo limepangwa kurejea tena Mahakamani Oktoba 6, 2025, saa 8:00 mchana kwa ajili ya kuangalia iwapo pande zote zimezingatia maagizo ya Mahakama, na litakuwa mubashara kupitia kiunganishi cha Mahakama.

 
Yaani bado wiki 4 uchaguzi na kampeni hamjaanza!! Hawa ACT ni wapuuzi sana walituona chadema wajinga ona sasa
 
Back
Top Bottom