Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema sera ya elimu bure inayopigiwa kelele na Serikali ya CCM ni ulaghai mtupu. Haitekelezeki kwa ufanisi kiasi cha kurejesha tena michango lukuki kwa wazazi.
“Wazazi wanachangishwa fedha kwa ajili ya mitihani, vitabu, chakula, walinzi, ukamilishaji wa madarasa na kadhalika. Michango mingi inaelekezwa kwa wazazi wakati Serikali ilishatoa ahadi ya kutoa elimu bila malipo. Sasa, je hii ni elimu bure kweli au ulaghai? Ni wazi kuwa Serikali haipeleki fedha kufikia lengo la kutoa elimu iliyo bora bali ni bora elimu.”
Ameongeza kuna ucheleweshwaji wa fedha za ruzuku za kuendesha shule (capitation grants) tangu mwaka 2023, Serikali haitoi fedha kwa wakati. Mfano mwaka huu shule hazikupokea fedha tangu mwezi Januari hadi Aprili.
Ameongea hayo akiwa Babati Mjini mkoani Manyara.