Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema kuwa ACT Wazalendo ndicho chama kilichobeba matumaini ya Watanzania. Amesema, "Tuna waambia Tume ya Uchaguzi Zanzibar, wasijaribu kuharibu Uchaguzi hatutakubali, kama kiongozi wenu nipo tayari kuyaongoza haya mapambano, nimeendelea kuonyesha kwa vitendo kwamba Umma umeitika,umejiandaa kwa uchaguzi na tutaendelea kufanya hivyo hadi ushindi upatikane"
Kauli hiyo ametoa leo Agosti 9, 2025 wakati Wagombea urais wa Tanzania na Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Luhaga Mpina na Othman Masoud, walipowasili mjini Unguja kwa ajili ya utambulisho kwa wanachama na wananchi wa kisiwa hicho, wakitokea jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu maalumu uliowapitisha kuwania nafasi hizo.