DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
“Miaka 60 badala ya kukabiliana na ujinga, tumeamua kuupamba; tumeamua kusheherekea wahitimu wa shule za msingi wasiojua kusoma na kuandika: tumeamua kuwa na wahitimu wa sekondari wasioweza kufikiri na kujitegemea; tumeamua kuwa na wasomi wa vyuo vikuu wasioweza kujieleza na kujisimamia.
Tumeamua kuusimika ujinga kwenye tambo za madarasa matupu na tumeamua kuuficha ujinga kwa kuuvisha magauni shahada za uzuzu. Hivi sasa, ujinga si adui tena, tumeutokomeza kwa kugawa vyeti kama njugu.
“Mapambano yaliyoasisiwa na wazee wetu, wake kwa waume, yamesalitiwa, yamepuuzwa, yamewekwa kapuni. Mapambano yaliyolenga kunusuru watu wa nchi hi kutoka kwenye makucha ya unyonyaji, ukandamizaji na udhalili, uliosababishwa na utawala wa kikoloni, yametelekezwa.
Mapambano ya kuhakikisha nchi hii inaongozwa na kuwanufaisha wakulima na wafanyakazi yamezimwa na genge la wahuni wachache- mapambano ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya haki, usawa na uhuru yamenajisiwa na walafi wa madaraka”.
Semu. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu, Makao Makuu ya ACT, Magomeni, Dar es Salaam.
Chanzo: Jambo Tv