Pre GE2025 Dosari na Rafu kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA Taifa 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rushwa na vurugu zimeikumba CHADEMA katika uchaguzi wa Taifa 2025 uliofanyika Januari 13 na 16, ambapo mabaraza ya vijana (Bavicha), wazee (Bazecha), na wanawake (Bawacha) yalichagua viongozi wapya. Hata hivyo, baadhi ya wanachama walidaiwa kupokea rushwa, jambo lililosababisha vurugu kwenye ukumbi wa kupigia kura, ambapo polisi walilazimika kuingilia kati.

Soma, Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Mvutano mkali unaendelea kati ya wagombea wa Uenyekiti, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, kutokana na tofauti za kisiasa na ushawishi wao. Januari 21, 2025 inatarajiwa kuwa siku ya kumalizika kwa uchaguzi, ambapo mustakabali wa CHADEMA utaamuliwa.

Soma: ACT Wazalendo waelezea rafu walizokutana nazo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kwenye uzi huu nitakuwekea matukio yote yanayohusisha matukio ya rushwa na mambo mengine ambayo yametia dosari kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA.

1737365845025.png
Matukio ya CHADEMA yaliyojaa rafu katika Uchaguzi wa Mabaraza na Uenyekiti 2025
 
Nasikitika sana this kind of things kutokea CHADEMA.

Nilidhani ni mambo yanayotokea CCM tu

Wakuu Erythrocyte Benjamini Netanyahu Missile of the Nation semeni lolote CHADEMA ipone
Kosa lilikua mfumo wa vyama Vingi hatukua tayari nao na viongozi wengi wa vyama vya upinzani wanashiriki haya maigizo,sasa watu kweli wasiojua huu mchezo wanapoonekana kuwa serious mizengwe inaanzishwa vyama vinaanza upya yani kama ile story ya Babeli kwamba walivyojaribu kusimamisha mnara kuelewana kati yao kunaondoka.
 
Rushwa na vurugu zimeikumba CHADEMA katika uchaguzi wa Taifa 2025 uliofanyika Januari 13 na 16, ambapo mabaraza ya vijana (Bavicha), wazee (Bazecha), na wanawake (Bawacha) yalichagua viongozi wapya. Hata hivyo, baadhi ya wanachama walidaiwa kupokea rushwa, jambo lililosababisha vurugu kwenye ukumbi wa kupigia kura, ambapo polisi walilazimika kuingilia kati.

Soma, Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025

Mvutano mkali unaendelea kati ya wagombea wa Uenyekiti, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, kutokana na tofauti za kisiasa na ushawishi wao. Januari 21, 2025 inatarajiwa kuwa siku ya kumalizika kwa uchaguzi, ambapo mustakabali wa CHADEMA utaamuliwa.

Kwenye uzi huu nitakuwekea matukio yote yanayohusisha matukio ya rushwa na mambo mengine ambayo yametia dosari kwenye Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA.

Matukio ya CHADEMA yaliyojaa rafu katika Uchaguzi wa Mabaraza na Uenyekiti 2025

Live with hidden updates or Live with no updates
 
Back
Top Bottom