#COVID19 Dotto Bulendu: Kwenye hili la chanjo, Rais Samia alikwama kimkakati

#COVID19 Dotto Bulendu: Kwenye hili la chanjo, Rais Samia alikwama kimkakati

blance86

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2016
Posts
2,138
Reaction score
5,632
Kwenye hili la Chanjo, Rais Samia alikwama kimkakati.

Na Dotto Bulendu(MwanaPuge),nikiandika kutoka kijijini Puge.
:::::::::::::
Vita ya hoja juu ya Ugonjwa wa Corona nchini kati ya Ndugu wawili ,Dr Doroth Gwajima (MB) na Waziri wa Afya dhidi ya Shemeji yake Askofu Josephat Gwajima (Mb) zimevuka mipaka Sasa hakuna hoja ni vijembe ,kebehi ,kudhalilishana na kuvua a nguo.

Askofu Dr Josephat Gwajima ana hoja zake za msingi ambazo Serikali ilitakiwa izitolee ufafanuzi Ili kuondoa hofu kubwa ambayo imetengenezwa Na Serikali Yeye.

Leo ukienda mtaani watanzania wapo njia panda kuhusu uwepo ama kutokuwepo Kwa Ugonjwa wa UVIKO-19,na Kama Chanjo dhidi ya UVIKO-19 ni Salama ama si Salama.

Watanzania wamekuwa njia panda Maana ni Serikali hii hii,Viongozi hawahawa Mwaka huu walizunguka kila kona ya nchi hii,wakasambaa Kwenye kila aina ya chombo cha Habari Na kuuambia umma Kuwa Tanzania hakuna Corona,hata watu walipoanza kufariki wao walisema hakuna Corona,watu walipougua walisema hakuna Corona bali kuna Changamoto ya kupumua.

Dunia ilipoleta Chanjo,Viongozi hawahawa,Mwaka Huu Huu waliwaambia wananchi kataeni Chanjo Maana imepandikizwa Vitu vibaya vyenye madhara Kwa wananchi Na hasa Waafrika.

Watanzania hawahawa ambao wamechanjwa Ndui,Homa ya manjano,Pepopunda ,Polio,Tetanasi Na zote zimetoka huko Ulaya,Marekani Na Asia wakalielewa vizuri somo kuhusu Chanjo Na wakasusia kila kitu kuhusu Chanjo.

Watanzania hawahawa ambao wakipata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wanameza ARV za msaada kutoka Marekani,wadada wakipata Ujauzito wanameza P2 za Mabeberu wakalielewa somo la wivu wa watu wa Magharibi Kuwa wamepandikiza Sumu Kwenye Chanjo za Corona Na Sasa wamezikataa.

Toka UVIKO ufumuke Mpaka mwezi wa Tatu Mwaka huu,ni viongozi hawahawa waliwaambia wananchi hakuna Corona,Chanjo ni Sumu,leo wamegeuka Na kuwaambia wananchi Corona ipo,Chanjo ni Salama tena wanawaambia kawaida.

Kampeni dhidi ya Chanjo Na Corona awamu ya kwanza chini ya Rais Magufuli ilipigwa Na Serikali nzima chini ya Raisi Magufuli mwenyewe lakini kampeni ya Sasa ya kukiri Corona ipo Na Chanjo itumike inapigwa na Waziri Gwajima pekee yake ,hii ni ishara Kuwa Samia Yupo peke yake katika hili wakati mtangulizi wake alikuwa Na watu nyuma wa kumsaidia kufanya kampeni za kusema hakuna Corona.

Rais Samia hatafanikiwa kubadili fikra za watanzania hata Kama atawakamata wote wanaopingana Na msimamo wa Serikali yake Kwani Serikali yake imeshawavuruga wananchi.

Doroth Na Mollel ndiyo walikuwa Vinara wa nyungu,Na kusema hakuna Corona leo wageuke kusema Corona ipo Na Chanjo ni Salama,hakuna wa kumuelewa Maana Watanzania siyo miti,ni watu wenye akili zao timamu.

Askofu Gwajima Kwa kifupi ana hoja nzito,na Bahati nzuri hoja zake zote za kisayansi zimejibiwa Na wanasayansi labda Kama nae Askofu Gwajima hataki kusikiliza hao wanasayansi.

Binafsi nimesikia Hoja za Askofu Gwajima zikijibiwa vizuri Na Dr Mwele Malecela kuhusu muda wa utafiti wa Chanjo,hoja ya damu kuganda ilijibiwa vizuri Na Prof Janabi,hoja ya watu kuchanjwa Na kupata maambukizi imejibiwa vizuri na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja Na Dr Derick wa Tanzanite Hospital kupitia Vyombo vya Habari .

Tatizo kubwa naloliona walewale walioendesha propaganda za Kuwa Hakuna Corona leo wanaongoza propaganda za Kuwa kuna Corona Na Chanjo ni salama .

Hoja za Askofu Gwajima ndiyo Hoja za wananchi huku nje,zijibiwe kisayansi na Mara Kwa Mara!maana Hoja za Kuwa Corona haipo,Chanjo siyo Salama haiwezi kujibiwa Siku Moja kupitia TBC ikafuta imani iliyopandikizwa kichwani mwa wananchi Kwa muda wa Mwaka mmoja Na Serikali hii hii na watu hawahawa.

Samia Kama anataka kuaminika Kwenye hili,Yeye binafsi awe kinara wa kutoa elimu,wasaidizi wake wawe Vinara Maana Sasa kaachwa Doroth Gwajima pekee tofauti Na wakati wa Magufuli.

Kitu cha mwisho,CCM kaeni Na Askofu Gwajima zungumzeni nae,tuhuma anazozitoa Kuwa Serikali imehongwa Ili ipokee chanjo ni tuhuma nzito.

Askofu Gwajima anataka kumaanisha Rais Samia kahongwa Ili kuwauwa Watanzania?kwamba Samia kahongwa ili 2025 watanzania wote wawe wamekufa?hizi ni tuhuma nzito.

Tuhuma hizi pekee ni hoja binafsi Bungeni kuwa Mbunge ka mtuhumu Rais kuhongwa Ili aangamize watu wake.

Tuhuma za Serikali(Rais)kuhongwa ni tuhuma nzito kuliko tuhuma ya aina yeyote,kumtuhumu Rais kuhongwa tena Ili watu wafe ni tuhuma mbaya Na nzito.

Naamini kikao kijacho cha Bunge,wabunge waihoji serikali kuhusu tuhuma hizi nzito zilizotolewa Na Mbunge Kuwa Serikali imehongwa.

Hizi ni tuhuma nzito kuliko tuhuma yeyote Kwa Serikali na Chama Tawala.

Kwa sasa dhana ya Uwajibikaji wa pamoja ambayo ilikuwepo wakati wa Serikali ya Rais Magufuli ilikuwepo wakati wa janga la Corona,Ila Kwa Sasa hakuna dhana ya uwajibikaji wa Pamoja!Katika Corona!CCM Na Serikali hawapo pamoja kila mtu Na msimamo wake.

Gharama za Kuwa sehemu ya taasisi ni kuwajibika pamoja,Kama huwezi kuiishi dhana ya uwajibikaji wa pamoja unanshauriwa usiwe sehemu ya Serikali.
 
Jibu la utata uliopo kuhusu chanjo, Rais SSH, na wateule wake waliochanjwa kuaminisha wananchi chanjo ni bora na salama, wapimwe hadharani kuthibitisha kuwa miili yao imetengeneza kinga.
 
Jibu la utata uliopo kuhusu chanjo, Rais SSH, na wateule wake waliichanjwa kuaminisha wananchi chanjo ni bora na salama, wapimwe hadharani kuthibitisha kuwa miili yao imetengeneza kinga.
Mimi kama shabiki wa mpira,niliacha kuangalia mpira wa ulaya baada ya kuona wanacheza bila mashabiki,mpira ukawa unaboa na nikarudi kuangalia VPL!Ligi zimeanza Ulaya na awamu hii nyomi kama lote,nimefarijika!

Hii inanipa picha kuwa Chanzo imeleta matokeo mazuri!Vifo ulaya vimepungua na maisha yameanza kurejea kawaida!

Hapa swala la msingi liwe serikali ihakikishe Chanjo zinazokuja ziwe halisi!
 
Mh Mbowe aliwashauri Chanjo iwe lazima kwa makundi yanayotakiwa kuchanja mkamuona msaliti - sasa nani akachanje tena wakati watu wanahubiria watu kwamba watageuza mazombi - who wants to be a Zombi after 5 yrs?

Nawaambia tutamaliza mwaka huu tukiwa tumechanja 3% ya raia wetu wote na hii itakuwa failure ya ajabu duniani.
 
Mimi kama shabiki wa mpira,niliacha kuangalia mpira wa ulaya baada ya kuona wanacheza bila mashabiki,mpira ukawa unaboa na nikarudi kuangalia VPL!Ligi zimeanza Ulaya na awamu hii nyomi kama lote,nimefarijika!
Hii inanipa picha kuwa Chanzo imeleta matokeo mazuri!Vifo ulaya vimepungua na maisha yameanza kurejea kawaida!
Hapa swala la msingi liwe serikali ihakikishe Chanjo zinazokuja ziwe halisi!
Siku zote wanaojazana huko kwenye viwanja vya mipira ni vijana na waathirika wakubwa wa corona ni wazee, na hata hizi chanjo wao ndio walengwa hasa na si vijana.
 
Hata mm nawaona Samia, waziri wa afya na naibu wake kama kituko. Hasa wanapo ongelea kuhusu chanjo ya korona.

Walisema korona haipo nchini lkn Sasa wanasema ipo. Hili linasameheka, maana yawezekana korona imeingia hivi karibuni.

Lkn walisema chanjo ni njama ya mabeberu kuangamiza waafrika. Sasa wanasema tuchanjwe. Kwa hili kamwe hawasameheki na ndiyo kikwazo kikubwa cha ubishani na mgomo wa watanzania kuchanjwa.
 
Mh Mbowe aliwashauri Chanjo iwe lazima kwa makundi yanayotakiwa kuchanja mkamuona msaliti - sasa nani akachanje tena wakati watu wanahubiria watu kwamba watageuza mazombi - who wants to be a Zombi after 5 yrs ?

Nawaambia tutamaliza mwaka huu tukiwa tumechanja 3% ya raia wetu wote na hii itakuwa failure ya ajabu duniani.
Utaanzaje kukurupuka kufanya chanjo kuwa lazima wakati hata uvaaji wa barakoa tu umetushinda? kuchukua tahadhari za kujikinga na corona tumefeli na ndio jambo lenye kupunguza maambukizi, sasa itakuwa ajabu kwamba tunaacha maambukizi yanazidi halafu sie huku tunalazimishana kuchanjana hivyo vichanjo M1 vya msaada.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Siku zote wanaojazana huko kwenye viwanja vya mipira ni vijana na waathirika wakubwa wa corona ni wazee, na hata hizi chanjo wao ndio walengwa hasa na si vijana.
Mashabiki vijana kwa wazee wanaingia uwanjani,nimeona jana kwenye super cup Dortmund vs Munich!

Hata data zinaonesha vifo vimepungua sana Ulaya baada ya chanjo!Kuna daktari mmoja bingwa wa mfumo wa upumuaji, ni mtanzania anayeishi USA alieleza namna chanjo inavyowasaidia watu kupambana na Corona na akaeleza kuwa waliochanjwa wengi hawawi Critical wanapopata maambukizi!

Tusiwe wabishi wa asili,tuangalie facts
 
Hata mm nawaona Samia, waziri wa afya na naibu wake kama kituko. Hasa wanapo ongelea kuhusu chanjo ya korona.

Walisema korona haipo nchini lkn Sasa wanasema ipo. Hili linasameheka, maana yawezekana korona imeingia hivi karibuni.

Lkn walisema chanjo ni njama ya mabeberu kuangamiza waafrika. Sasa wanasema tuchanjwe. Kwa hili kamwe hawasameheki na ndiyo kikwazo kikubwa cha ubishani na mgomo wa watanzania kuchanjwa.
Ni kweli wamekuwa vigeugeu!Lakini turudi kwenye uhalisia, kipindi cha mwendazake waliendeshwa na wao wakakubali kuweka taaluma zao pembeni!

Si wakati wa kunyoosheana vidole kuwa wewe ulisema hiki juzi,ni walati wa kuangalia tunavukaje!
Je,chanjo inasaidia?
 
Umefafanua vizuri sana na umeeleweka kuwa wawili hawa wameanza kuumbuana hadharani. Kama ulivyokazia hapo juu kuwa watanzania wanazo akili ni kweli lakini wapo watakaodanganyika.

Kati ya wawili hao wanaosigana, mchungaji Gwajima hoja zake zimesimama na hazijajibiwa popote kisayansi kama unavyojaribu kuaminisha watu. Hao wanasayansi uliowataja iwe hapa kwetu au marekani,uchina au ulaya majibu yao ni mepesi tu kuwa chanjo ni salama kachanjeni.

Ili dhahabu ifikie usafi kwa kiwango kinachotakiwa ni lazima ipite kwenye tanuru la moto lenye nyuzi joto zinazotambulika kisayansi, kinyume chake hutapata dhahabu ya kiwango tarajiwa,aidha Ili ifikie kuitwa Professor ni lazima upitie ngazi mbali mbali za madaraja ikiwemo mitihani na maandiko kadhaa. Hivyo hivyo chanjo yoyote inapitia mchakato mrefu wa majaribio kujihakikishia usalama wake kabla ya kutumika. Chanjo ya Corona haikupitia mchakato huo na ndio Maana inakosolewa utengenezaji wake Dunia nzima kwa sababu imekiuka misingi ya kitalaamu ambayo hata huyo Janabi na yule mwingine Malecela wanajua. Majibu yao ni mepesi mno kuliko hata majibu yanayotolewa vijiweni na wananchi wa kawaida.

Chanjo hii ya Corona J&J inatolewa nje ya utaratibu wa kawaida kwa idhini ya dharula na matokeo ya chanjo hii hayajulikani kwa sasa mpaka pale aliyechanjwa atakapoanza kuona mabadiliko kwenye mwili wake miaka ijayo na hivyo kutoa mwanya kwa watengenezaji kujifunza madhara yatokanayo na chanjo.

Chanjo hii ni hiari hivyo ni busara kwa binadamu anayejitambua kuhoji kama anaona mambo hayako sawa. Mchungaji Gwajima yuko sahihi kwenye hoja zake...Asibezwe wala kutishwa.
 
Chanjo hii ya Corona J&J inatolewa nje ya utaratibu wa kawaida kwa idhini ya dharula na matokeo ya chanjo hii hayajulikani kwa sasa
Inasemekana wanaume waliochanjwa ninilii zao zinakosa nguvu ya kusimama dede na kubakia zimening'inia kama mikufu. (Source: hapo Kenya kwa majirani zetu).
 
Uzi umesheheni hoja nzito!! Dr Gwajima and her company whoever, lacks the moral authority to campaign successfuly for covid 19 vaccine because she successfuly campaigned against covid 19 vaccines!! The same applies to her deputy Dr Mollel!!

Mama apende asipende they have to go!! Ila ugumu uko hapa!! Ukimwondoa kwa kigezo hiki itabidi awang'oe wengi kwa kigezo hicho hicho!! Je ubavu huo anao?? Dr Gwajima aendelee kupigia kampeni nyungu na wote tutamwelewa!! Kampeni ya chanjo awaachie wengine !!
 
Halafu bila haya usoni Katibu mkuu wa wizara ya afya anasema Tanzania itaanza kutengeneza chanjo yake! Shit!

Nimelogwa nichanje chanjo iliyotengenezwa hapa Tanzania!
 
Tatizo kubwa ni pale ikulu, hakuna watu sahihi wanaojiamini, nchi inayumba sana
 
Mh Mbowe aliwashauri Chanjo iwe lazima kwa makundi yanayotakiwa kuchanja mkamuona msaliti - sasa nani akachanje tena wakati watu wanahubiria watu kwamba watageuza mazombi - who wants to be a Zombi after 5 yrs ?

Nawaambia tutamaliza mwaka huu tukiwa tumechanja 3% ya raia wetu wote na hii itakuwa failure ya ajabu duniani.
Hiyo 3% ni kubwa mno wala haiwezi kufikiwa!! Tuko 60,000,000 kwa hiyo 3% ni watu 1,800,000!! Mpaka leo hizo dozi 1,000,000 za chanjo bado zimedoda!! Watu wameshachanganya akili za kuambiwa na za kwao halafu wanawacheki tu!! Nani wa kumsikiliza yule Dr gwaji mtaalamu wa mipasho na kudelemka?
 
Naunga mkono hoja hili suala wameachiwa Wizara ya Afya pekee na Rais tofauti na awamu ya 5 ilikuwa viongozi wote wa Serikali wako mstari wa mbele kutueleza tupige nyungu hadi wengine waka anza kuzipa Season1 hadi 3,
Saiv wakuu wa mikoa wanajitokeza na kusema hali mikoani kwao ni mbaya sana (Mtaka wa Dodoma)
Hamna Waziri mwingine anayelizungumza hili suala.!
 
Back
Top Bottom