#COVID19 Dotto Bulendu: Kwenye hili la chanjo, Rais Samia alikwama kimkakati

MwanaJF mmoja kajibu hivi
 


Siyo rahisi kiivyo!
Labda wawajibike/wawajibishwe zije sura mpya yamkini watakapokuja kutoa hamasa na elimu pengine wataweza kueleweka!

Lakini kwa watu walewale kuwa na ndimi mbili kiukweli inachanganya wananchi wengi!
 
Ilifika mahala hata kutamka neno ugonjwa wa Corona ilikuwa kama kufanya kosa !

Eti ikabidi isemwe changamoto zakupumua ! Imagine! [emoji15][emoji15]

Barakoa ikasemwa si salama ikibidi watu wavae za kushona na top officials walikuwa hawavai kabisa !

Gafla kimekuja kiswahili kingine tofauti kabisa, Je hapo wananchi washike lipi?! Lile u hili? Kwanini labda?!
 
Hakuna zababu za msingi za kuchanjwa hadi sasa. Ni porojo porojo tu za wanasiasa na wataalamu wetu wa afya ambao pia wanadai chanjo ni bora na salama kwa kuambiwa. WHO pia imetoa kibali cha dharura (EUA) cha matumizi ya baadhi ya hizo chanjo. Watengenezaji wa chanjo nao wanakiri kuwa bado wako kwenye maabara wakifuatilia matokeo ya chanjo zao.

Tanzania UVIKO-19 imekuwa ikitibika kwa dawa mbadala km nyungu. Dawa hizo pia zimetumika na kuendelea kutumika kama kinga ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za kujikinga dhidi ya maambukizi.

Pamoja na wimbi jipya (variants) la UVIKO-19, Watanzania wanaendelea na maisha yao kama kawa. Wanaosemekana wamekufa kutokana UVIKO-19 nchini (wengi wao wenye uwezo kifedha na madaraka), wataalamu hawathibitishi ukweli huo bali hisia za watu, kama wakati wa mwanzo wa UKIMWI.

Katika mazingira hayo hakuna shaka WaTz wengi hawatachanja. Ukweli tayari umejidhihirisha kwa chanjo ya awamu ya kwanza (1m) hadi sasa hajaisha. Hata watumishi wa huduma ya afya (madaktari na wauguzi wapatao zaidi ya milioni) wamesita kuchanjwa.
 
Hili mambo yaende sawa, sirikali ikawabananishe Maaskofu wa Katoriki pamoja na Mashehe wa Bakwata, waandike waraka kwa waumini wao kuwa hawataruhusiwa kuingia kanisani au msikitini kama haujachanjwa. Hii itawafanya wananchi wachanje fasta. Ndani ya wiki tuu hizo dawa zote zitakuwa chache. Maana huu mziki unaonekana kama ni one woman show.
 
Tatizo liko wapi? Waliochanjwa wako salama, kwa nini wanataka kuwalazimisha wasio chanjwa? Waliochanjwa waendelee kula kuku kwa mrija wafaidi matunda ya ulimwengu kwa miongo kadhaa waachane na wasiochanjwa.
 
Madai ya Askofu Gwajima ni kuwa chanjo ni njia ya kumdhibiti (control) aliyechanjwa. Kujichanganya kwa Waziri wa Afya na Naibu wake kila siku yawezekana ni kutokana na kuchanjwa (dalili za awali). Yajayo kwa waliochanjwa watajiju
 
Siyo rahisi kiivyo!
Labda wawajibike/wawajibishwe zije sura mpya yamkini watakapokuja kutoa hamasa na elimu pengine wataweza kueleweka!

Lakini kwa watu walewale kuwa na ndimi mbili kiukweli inachanganya wananchi wengi!
Mimi binafsi sikuwaunga mkono walati wanahimiza nyungu na kukandia chanjo,nilijua walikuwa wanaangalia boss wao anaenda kwa gia ipi!
Binafsi naiamini WHO na ndio maana nimechanja tayari!
Ambao watataka waje wabembelezwe sawa wasubiri,ningeliwa mimi wala hata nisingehamasisha!
Ningesema tu serikali imejiridhisha kuwa chanjo inaongeza kinga,anayetaka kuchanja ajiandikishe,asiyetaka aache!Maisha yaendelee!
 


Kwanini mnapenda ku-force mambo ?
Kwanini mnapenda ubabe?

Kwanini njia ya hamasa na elimu isitumike kuliko vitisho?

Je wakiamua kutokwenda kusali huko makanisani na misikitini ? Wakaamua kusali majumbani?!

Tena siku hizi kuna global church services hata kwenye simu ya kiganjani kunaweza kufuatilia Ibada mubashara
 
Kabla ya kuanza na mkakati mpya, ili kutoa sintofahamu zilizotangulia ilibidi viongozi wote walioshiriki kwenye (kampeni) mikakati ya Nyungu & anti chanjo, maombi ya kitaifa - wote angewapiga chini ili sasa aanze na watu wapya kutangaza upya Chanjo, maombi hayaondoi ungonjwa sababu ugonjwa ni sayansi na si wa kiroho, Nyungu haijawahi kuua virus..

sasa hapa ndipo kwenye tatizo, wale wale waliotuambia Nyunguuu pigeni nyunguuu wale wale, chanjo si nzuri, maombi maombi ndiyo hawa hawa leo wanatuambia na kutuambia opposite side of it.
 
Watanzania hawa hawa waliokuwa wanampinga Magufuli kwa kuamini Corona itaondolewa na maombi, ndio hawa hawa wanaopinga chanjo ya Corona sasa hivi.
Very confusing
 
Mkuu mwambie Dotto Bulendu kuwa serikali ya Tanzania haijawahi kusema hakuna corona, wala haitaki kuchukua hatua za kupambana na corona, na wala kukataa chanjo ya corona- MENGINE yote sina shida nayo maana ni hulka za kiana harakati.
Kwa faida ya wengi na nukuu maneno haya

“You can be wrong if you’re dealing with information that is evolving.” The data about covid-19 and the vaccines seems to change nearly every day; for those of us with potentially confounding conditions, we carefully monitor that changing and updating data" (Anthony S. Fauci, infectious-disease expert)
 
Josephat Gwajima yuko na hoja lakini kwanini anafanya kama mashindano yani kila siku akilala akiamka anaanza kuipondea hiyo chanjo serikali ilishasema kuchanja sio lazima yeye alishasema hatachanja lakini kwanini amekua mtu wa kurudiarudia hili kila siku mpaka mtu unaitukana serikali kweli?Nauona mwisho mbaya sana kwa huyu jamaa hata time will tell huwezi shindana na serikali .....Upande wa Gwajima Waziri hakupaswa kuendelea kuwa waziri ingekua vyema angejiuzulu hauwezi kuwa kigeugeu watu hawawezi kukuelewa hata kidogo ulituambia ni tisa saivi unasema sita ...yote kwa yote elimu bado inahitajika sana kwa watu
 
Tatizo kubwa sio serikali wala Gwajimas. Tatizo kubwa ni ujinga wa baadhi ya waTanzania walio wengi tena wakiwemo walioenda shule. Ni wajinga nasisitiza.
Serikali imeleta chanjo. Anayetaka achanje, bure! Asiyetaka aache, pia kuacha ni bure! Sasa makelele ya nini? Au ni kukosa kazi za kufanya?
Mtu asiyetaka chanjo anaidai nini Serikali? Ni vitu vya ajabu kila siku kuwe na ubishani kuhusu chanjo, kama mtu anaona haifai siaiache tu?? Narudia, shida sio Serikali wala Gwajimas, shida ni ujinga wa baadhi ya miTanzania.
 
Kwa mawazo yako unaisi kila mtz, hanautashi wa kutosha juu ya chanjo zote.
Wewe mwenyewe tukikuuliza juu ya chanjo gani ni salama?? utabaki kimya.
But sipo kwa ya kumtetea huyu Askof Rashidi . The problems is government
Kwa nini wasitoe elimu ya kutosha juu ya chanjo. Kwa hiyo wananchi wengi wanabaki dailema hawajui ipi ni kipi , sasa wanatokea watu wapuuuzi kama Askof, hanaongea vitu alivyo viota usiku, nakuongea as if hana scientific research juu hiyo .
Wakati ni layman tuu, Hanaye itaji msada wa ki- psychology
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…