GE2025 Dotto Bulendu: Wanahabari wametekeleza wajibu wao kuelekea uchaguzi mkuu

GE2025 Dotto Bulendu: Wanahabari wametekeleza wajibu wao kuelekea uchaguzi mkuu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mhadhiri mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) kilichopo mkoani Mwanza, Dkt. Dotto Bulendu amesema waandishi wa habari wametekeleza wajibu wao katika kutangaza kampeni kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Dkt. Bulendu amesema waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo redio, magazeti na televisheni wameepuka kuripoti habari zitakazoleta mpasuko katika jamii na hii imesaidia kuwapa wananchi haki yao ya kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua wagombea wanaowafaa kutokana na sera za mgombea husika.

Aidha, Dkt.Bulendu amewataka wagombea kujiepusha na kauli za kuchafuana na kuweka vipaumbele kupitia ilani za vyama vyao.

Amesisitiza kuwa ni jukumu la wanahabari kuwalinda watu kwa kuhakikisha amani inakuwepo, kuepuka kushambulia imani ya mtu na kabila ili kuepuka migogoro.

Dkt. Bulendu amesema hayo leo Septemba 9,2025 katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1.

 
Back
Top Bottom