Kuna kitu sielewi, kama hii Reli ya Kenya haifiki Uganda, ina maana itakuwa imeshia Nairobi au sijui Mji gabi nchini Kenya, sasa si itakuwa hasara kubwa kwa Wakenya? Kwa maana itakuwa haina maana yoyote ile kwani huwezi kuendesha Reli kwa nauli za abiria tu, hapo hapo kuna ushindani ya mabasi pia hivyo siyo abiria wote watakaotumia hii Treni matokeo yake kuishia kuwa white elephant project na Wachina kuja kutembelea kama Watalii miaka ijayo kuona kazi ya watu wao, basi na hizo Stesheni zote zitageuka kuwa magofu tu na Wapokoto watafugia Ng'ombe!