Dowans: Kikwete akubali serikali kushindwa; Amruka Dr. Idris


Good observation mkuu, huyu rais wetu anataka kila kitu kiwe rahisi and doesn't want to make hard decisions.

Jasusi, it was not April's fool day because TBC repeated the speech this morning 🙂
 
Watu tunawapeleka nje ya nchi kusoma kumbe wananshindwa hata kusema hotuba hii ni ya mwanzo wa mwezi? Safari yetu ni ndefu mno.
 

Alikuwa na maana gani hapa aliposema taarifa hasi kuhusu mradi huo? Au anaona haya kumtuhumu mtangulizi wake 'Mr. Clean'
 
Tumesikia ahadi nyingine kutoka kwa Rais wetu. Ahadi ya jitihada za kuhakikisha kuwa hakuna mTanzania atakaekufa kwa njaa. Vile vile, Rais ameahidi kuwa jitihada za dhati zitafanyika kuhakikisha kuwa nchi inapata umeme wa kutosha. Je, ahadi hizi zitafanyiwa kazi kweli ama ndio zinaongeza wingi wa ahadi ambazo amewahi kuzitoa?

Kuhusiana na Mkutano wa G-20, sidhani kuwa kuna lolote la maana kwa Afrika litakalo jadiliwa. Nchi hizi tajiri duniani zina matatizo makubwa ambayo hata wao wangependa kuyapatia utatuzi. Kuongeza tatizo la Afrika kwao ni kuongeza tatizo wasilohusika nalo moja kwa moja. Nchi za Afrika na nchi nyingine changa duniani zinataka kutumia athari hizi kuhalalisha kushindwa kwao kiuchumi. Hata matajiri hao wakitoa msaada mkubwa kiasi gani, sioni jinsi nchi kama zetu zinavyoweza kuendelea bila kubadilika kiutendaji, vipaumbele na kadhalika.

Mimi nigefurahi zaidi kama Rais angebainisha namna anavyotaka wananchi wake kujiweka tayari kwa athari za GFC. Nilitegemea angebainisha mikakati ya ndani ambayo serikali yake imeanza kuichukua ili kuhakikisha madhara ya GFC yanakuwa madogo kadiri inavyowezekana. Sioni ushirikishi wa wananchi katika kuleta chachu za maendeleo baada ya kuona kuwa nchi tulizokuwa tunazitegemea zikianza kuhaha kutokana na GFC. Afrika must change. Haiwezekani kubaki tukisubiri maji yatoke kwenye bomba ambalo tunaambiwa uwezo wake wa kutoa maji umepungua au haupo kabisa. Hii ni catastrophic kwa Afrika. Hatuwezi kubaki tunasubiri, lazima tujipange kujihakikishia hali bora ndani ya matatizo yaliyopo. Lazima kubainisha opportunities tulizonazo katika sakata hili. Hii ni ishara kuwa utegemezi kwa nchi tajiri unatakiwa upungue, na jitihada binafsi zitumike kuleta ufanisi wa ndani.
 
Alikuwa na maana gani hapa aliposema taarifa hasi kuhusu mradi huo? Au anaona haya kumtuhumu mtangulizi wake 'Mr. Clean'

Nadhani maana ya statement hiyo ni kuwa, Wahisani wamesitisha kutoa misaada ya uendelezaji wa mradi huo kutokana na taarifa ambazo hazina manufaa kuhusiana na umilikiwa mgodi huo. Wahisani inaelekea wameona kujiingiza kwao katika kusaidia mgodi huo kunaweza kuharibu credibility yao kutokana na kashfa zinazouhusisha mgodi.
 
Ningeshangaa kama asingemsifiwa swahiba Rashid!!!! For sure ni lazima ampige Makyembe kijembe kwani ni chanzo cha anguko la vipenzi RA na EL. As usual no substance in it!!!
 
 
Ninasikitika kuwa huenda bado tuna miaka 7 ya mambo haya haya!
 
I'm out of here! ....please excuse me. 😡
 
ona sasa hotuba yake!!! masikini!!
yani akipewa na huyo mwandishi sidhani kama huwa anaipitia kabla ya kusoma kwa taifa.amempongez idris badala ya watanzani.
swala la mkutano wa G-20 amelisema kwa marefu kuliko maswala muhimu ya taifa,
hii hotuba ya zima moto.yani jamaa ameindaa fasta fasta na kumpa Rais.
maneno yake ni yale yale, ''nawahimiza,nawaomba,tushirikiane,tuvumiliane,tuwe pamoja katika kipindi hiki kigumu nk.
Inatia huruma
 
hotuba ya mhe. Jakaya mrisho kikwete, rais

http://issamichuzi.blogspot.com/
 
Hivi na economic Slow Down/ Credit Crunch, nchi yetu inashindwa kupata Mkopo wa kuwekeza kwenye Miradi ya Umeme? wakati potential ya kurudisha hiyo mikopo ipo, kwa sababu soko la Umeme lipo, cause only 13% ya watu wa Tanzania wana pata umeme, tukiongezea hata mpaka 50% si nchi itapiga hatua kubwa tu na Mkopo utarudi, tukiweka hiyo risk factor kwamba sio !00% ya watanzania kwa sasa wanaweza kulipia huo Umeme.
Ingawaje kwa Kiongozi Shupavu anaweza Sema Why not 100% ya watanzania wawe na Umeme.

Pili ikiwa tuliweza kuweka Rehani nchi kwa ajili ya rada, ambayo ilishindwa kustimulate the economy, why not do so kwa kitu ambacho kitaleta stimulas ya kweli kwenye maendeleo yetu, after all financial institution zinatafuta watu wakuwakopesha, na wapo tayari ikiwa succcess ya mradi wenyewe ni kubwa na Security zipo. Inaweza kuwa hiyo miundo mbinu itakayo jengwa, potentiality ya wateja, na ile Signature ya Nchi tu, kwamba Government inaweka Guarantee.
 

To be honest, umepigilia msumali panapotakiwa. The whole team around him is nothing from upstairs. Kwa sababu ukiangalia hotuba zake huwa hazina jipya jipya zaidi ya kufanana naza Mkapa zile za kuteteana. Ina maana kwenye kumbukumbu zao hawakumbuko kuwa kuhusu njaa kuna waziri aliwahi kusema hakuna kitu kama hicho? Dowans jamaa si waliongea maneno ya kejeli?

Issue ya Dowans haikuwa kununua au kutokununua kuna kitu zaidi ya hicho yeye kama mkulu inabidi afanye lakini chaguo la mungu hili hata halioni. Lakini mimi nafikiri hawa jamaa wanajuana kwani hiyo Dowans na mkulu si anahusika? Maana kama ni maandalizi ya huo urais ni nani kama si yeye? Hivyo yeye anachukulia kawaida ili watafute njia nyingine maana hii watu wamekaba mpaka penati.

Hapa ni kuendelea kupiga kelele tu waone aibu kama hili la Dowans lakini HATUA SIDHANI KAMA ZITACHUKULIWA KWA KICHWA HIKI TULICHOCHAGUA JAPO MIMI SIKUMCHAGUA.
 
Ahsante JMK, right to the point, nimekufahamu mkuu, asiyekufahamu ajinyonge:

1) Hili la mvuwa naona hata mmoja humu hajalipinga wala kulikosowa na ni zuri sana kulikumbusha kama kawaida yako Mkuu nakupa heko kwa kugusia na kuwajulisha waTanzania kitu hichi muhimu sana.

2) La umeme tumefahamu na tatizo la umeme lipo na halikuanzia wakati wako na ahsante sana kuwa serikali ya awamu yako inalishughulikia ipasavyo na nimekuelewa uliposema litapokuwa tayari litatangazwa. Ahsante kaka, kazi kwa Ngeleja na Waziri Mkuu Pinda, haya sasa mtufanyie madudu kama ya Lowassa, Karamagi na Msabaha halafu tuwa Bangusilo mseme JMK mbaya hajatutetea.

Hapa inaonyesha Mkuu unavyoshughulikia matatizo uliyowachiwa na waliopita na nina uhakika umeshalipatia ufumbuzi wa kudumu, na ule ufumbuzi wa muda mfupi wakati wa emergency tuliona watendaji wako walivyokuangusha na tuliona ulivyo washughulikia, uliweka history ya siasa za Tanzania pale ambapo uliruhusu tume itowe wazi matokeo ya uchunguzi wake na yaliyojiri baada ya hapo tunayafahamu. Si umetuonyesha mfano bora kuliko awamu zilizopita tulizoona ripoti za tume zinavyokaliwa mpaka zinakuwa hazina maana yoyote. Ki-chama na ki-serikali ulikuwa na uwezo wa kuizuwia lakini kwa busara zako hukufanya hivyo. Nina uhakika isingekuwa wewe mpaka leo bado wangekuwepo serikalini. Kwa hilo umeonyesha mfano bora, na hawa sasa wachunge na wayafanye uliyoahidi unayashughulikia kwa umakini na kufuata sheria, watapo-pinda tu usisite kuwa bangusilo kama waleeee.

3) La G20 nimekufahamu sana, asiyekufahamu ajinyonge, macho ya dunia nzima yako huko na ni vizuri kuwaelimisha wa Tanzania na wao wawe wanayaona mambo kwa upeo mpana kwani dunia sasa ni kijiji kimoja na chochote kitachoamuliwa na hao wenye mifedha kinaweza kutuathiri sisi kwa njia moja au nyingine.

Ahsante kwa kugusia mambo matatu muhimu kwa wakati huu, mvua,umeme na athari za uchumi duniani.

Asiye kuelewa kwa hayo ana lake, sio siri.

Mwisho, ahsante kwa dua yako njema kwa waliopatwa na misiba uliyoitaja nami naungana nawe kuwapa pole wafiwa wote. Inna liLlahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…