Ahsante JMK, right to the point, nimekufahamu mkuu, asiyekufahamu ajinyonge:
1) Hili la mvuwa naona hata mmoja humu hajalipinga wala kulikosowa na ni zuri sana kulikumbusha kama kawaida yako Mkuu nakupa heko kwa kugusia na kuwajulisha waTanzania kitu hichi muhimu sana.
2) La umeme tumefahamu na tatizo la umeme lipo na halikuanzia wakati wako na ahsante sana kuwa serikali ya awamu yako inalishughulikia ipasavyo na nimekuelewa uliposema litapokuwa tayari litatangazwa. Ahsante kaka, kazi kwa Ngeleja na Waziri Mkuu Pinda, haya sasa mtufanyie madudu kama ya Lowassa, Karamagi na Msabaha halafu tuwa Bangusilo mseme JMK mbaya hajatutetea.
Hapa inaonyesha Mkuu unavyoshughulikia matatizo uliyowachiwa na waliopita na nina uhakika umeshalipatia ufumbuzi wa kudumu, na ule ufumbuzi wa muda mfupi wakati wa emergency tuliona watendaji wako walivyokuangusha na tuliona ulivyo washughulikia, uliweka history ya siasa za Tanzania pale ambapo uliruhusu tume itowe wazi matokeo ya uchunguzi wake na yaliyojiri baada ya hapo tunayafahamu. Si umetuonyesha mfano bora kuliko awamu zilizopita tulizoona ripoti za tume zinavyokaliwa mpaka zinakuwa hazina maana yoyote. Ki-chama na ki-serikali ulikuwa na uwezo wa kuizuwia lakini kwa busara zako hukufanya hivyo. Nina uhakika isingekuwa wewe mpaka leo bado wangekuwepo serikalini. Kwa hilo umeonyesha mfano bora, na hawa sasa wachunge na wayafanye uliyoahidi unayashughulikia kwa umakini na kufuata sheria, watapo-pinda tu usisite kuwa bangusilo kama waleeee.
3) La G20 nimekufahamu sana, asiyekufahamu ajinyonge, macho ya dunia nzima yako huko na ni vizuri kuwaelimisha wa Tanzania na wao wawe wanayaona mambo kwa upeo mpana kwani dunia sasa ni kijiji kimoja na chochote kitachoamuliwa na hao wenye mifedha kinaweza kutuathiri sisi kwa njia moja au nyingine.
Ahsante kwa kugusia mambo matatu muhimu kwa wakati huu, mvua,umeme na athari za uchumi duniani.
Asiye kuelewa kwa hayo ana lake, sio siri.
Mwisho, ahsante kwa dua yako njema kwa waliopatwa na misiba uliyoitaja nami naungana nawe kuwapa pole wafiwa wote. Inna liLlahi wa Inna Ilayhi Rajiun.