Kaka hiyo sio biashara wala soko huru, hiyo inaitwa anarchism. Sibishi kuwa haiwezekani kuwa na hali kama hiyo, kwani Somalia inaendelea, lakini kwa nchi yenye 'serikali' kama yetu, hiyo huwa inaitwa fujo.
Labda utuambie definition yako ya anarchism, maana sioni ni kwa jinsi gani iko applicable kwa case hii. (
Anarchism - Wikipedia, the free encyclopedia ). Unless uniambie kuna sheria bwana Kyaruzi anazivunja, anarchism is in the other extreme kabisa. Kuifananisha case hii na somalia kidogo kaka imepitiliza.
Kwa kifupi kama unaamini kuwa soko huria linafanya kazi likiachiwa lifanye kazi, muulize Bush au Obama, ambao ndio walimu wetu wa mfumo huo.
Unachanganya ubepari na soko huria kaka. Ni consept mbili tofauti. Na ukweli ni kwamba wapo mabepari ambao hawapendi soko huria, na hujikinga na soko huria kwa kutumia monopolies na cartels ili kufanikiwa kupanga bei.
Soko huria haimaanishi hakuna taratibu, au haimaanishi sheria zisifutwe. Soko huria maana yake rules are set na zinakuwa applicable kwa kila mshiriki katika soko sawa sawa. Soko huria maana yake bei ya kitu au huduma ni makubaliano ya hiyari kati ya muuzaji na mnunuzi.
Wengi tunalalamikia soko huria pale tunapokuwa wanunuzi, halafu hatukubaliani na bei za wauzaji. Wewe ukitaka kuuza kitu chako ungependa upangiwe bei? Sasa mbona unapenda mwingine akitaka kuuza chake apangiwe? Mda si mrefu mtu atalalamika Kempisk wapangiwe bei ili sote tufaidi.
Pale unapoona umeuza kitu chako kwa bei unayotaka mwenyewe, basi ujue soko huria hapo limefanya kazi. Ninauhakika usingependa serikali ikupangie bei ya gari yako au redio yako utakapotaka kuiuza. Yes, kuna maeneo soko huria halifanyi kazi na inabidi kuingilia kati. Lakini kulalamikia soko huria kama ni lidudu ambalo halitakiwi kuwepo, na wakati wewe wenyewe unalitumia kila siku pengine ni aina ya unafiki, au kutokuelewa kinachoendelea.
Kama sentensi yako kuhusu obama na bush inamaanisha li credit crunch ni kwa sababu ya soko huria, ningekushauri ufuatilie vizuri zaidi. Na jibu lingekuwa ni rahisi tu kwamba ni kwa sababu soko huria ni kitu kibaya, basi tungeeona wakijaribu kurekebisha kwa kuanza kupanga bei za vitu ... na cha kwanza ambacho wangeanza nacho ni kupanga bei za share zinazoporomoka kila siku na kuhakikisha kwamba haziporomoki maana wananchi wao wanapata hasara na wengine hata wanajiua.
🙂