DP Gachagua: Rais Ruto kama nimekukosea naomba msamaha, Wabunge kama nimewakosea naomba msamaha na Kanisa mnisamehe!

DP Gachagua: Rais Ruto kama nimekukosea naomba msamaha, Wabunge kama nimewakosea naomba msamaha na Kanisa mnisamehe!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naibu Rais mh Gachagua akiwa Kanisani amewaomba msamaha Wakenya wote kama kuna jambo amewakosea

Aidha Gachagua amemuomba msamaha Rais Ruto na Wabunge endapo aliwakosea jambo lolote

Citizen Tv

===================​

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, jana ameomba msamaha ikiwa ni siku mbili kabla ya kujitetea kwa saa mbili (dakika 120) mbele ya umma juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Gachagua aliomba radhi wakati wa ibada wakati wa Ibada wa Kitaifa ya Maombi jijini Nairobi, na kusema kama kuna aliyemkosea akiwa Naibu rais, amsamehe kutoka moyoni.

Pia alimuomba msamaha Rais William Ruto, wabunge waliowasilisha hoja katika Bunge la Taifa ya kumwondoa madarakani, na Wakenya kwa makosa aliyoyafanya.

Bunge la Taifa lilianza mchakato wa kumshtaki na kumng’oa madarakani Naibu Rais, baada ya Spika Moses Wateng’ula kuzikubali hoja 11 zilizowasilishwa na Mbunge wa Kibwezi West, Mwengi Mutuse.

Aidha, jumla ya wabunge 291 kati ya 349 wa Bunge la Taifa wamesaini hoja ya kumshataki na kumng’oa madarakani Naibu huyo.

Ibara ya 150 ya Katiba ya Kenya inaeleza masharti ya kuondolewa kwa Naibu Rais, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa sheria na kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake.

Aidha, hoja ya kumshtaki lazima iungwe mkono na angalau theluthi moja ya wabunge 117 katika Bunge ili taratibu zianze ikiwa Bunge la Kitaifa na Seneti wataridhia kwa theluthi mbili.
 
Huyu amevurunda nini huko Kenya?
 
Huyu amevurunda nini huko Kenya?
Msamaha mtu huamba pale anapogundua kosa ila usipoliona kosa kuomba msamaha ni kujidhalilisha.
Neno "kama" kwenye sentesi ya kuomba msamaha linamaanisha mtu aombae msamaha hajui kosa lake na hivyo hana uhakika na kile wanachomtuhumu kwacho kuwa na ukweli wowote.
 
Adui aliekuanza sio wa kumsamehe maana atakutaftia timing muda mwingine.
 
Politicians wote worldwide are out of touch...., Yaani badala ya kuomba masamaha kwa wananchi ambao ndio inabidi wawe defacto-mabosi wako, unaomba masamaha kwa manyangau wenzako ?
 
Viongozi wa kenya waungwana sana.wakikosea wanakubali kuwa wamekosea na kuuomba msamaha umma.Sisi Huku Tanzania kunalitekaji linauwa watu lakini limekataa kukubali kuwa limekosea na halitaki kuwajibika hata kutuomba tu msamaha halitaki.Ndiyo linaendelea kukamua Kodi zetu.
 
Naibu Rais mh Gachagua akiwa Kanisani amewaomba msamaha Wakenya wote kama kuna jambo amewakosea

Aidha Gachagua amemuomba msamaha Rais Ruto na Wabunge endapo aliwakosea jambo lolote

Citizen Tv
Cheo kitamu sana kuliko pesa 😆😆😆

Hapo ameogopa kwenda jela maana alijifanyaga kwamba sana huyu Jamaa 😆😆👇👇
 
Msamaha mtu huamba pale anapogundua kosa ila usipoliona kosa kuomba msamaha ni kujidhalilisha.
Neno "kama" kwenye sentesi ya kuomba msamaha linamaanisha mtu aombae msamaha hajui kosa lake na hivyo hana uhakika na kile wanachomtuhumu kwacho kuwa na ukweli wowote.
👍
 
Cheo kitamu
Cheo kinaleta heshima
Cheo kinampa fedha
Cheo ni CV
Cheo ni machine ya kurahisisha mambo binafsi
Asiposamehewa ajiandae kuwa harassed.

Hata hivyo akiachwa atadharaulika sana na Jamaa wa Ruto 😂😂

Na atakuwa hana Cha kufanya yaani VP wa Katiba tuu
 
Viongozi wa kenya waungwana sana.wakikosea wanakubali kuwa wamekosea na kuuomba msamaha umma.Sisi Huku Tanzania kunalitekaji linauwa watu lakini limekataa kukubali kuwa limekosea na halitaki kuwajibika hata kutuomba tu msamaha halitaki.Ndiyo linaendelea kukamua Kodi zetu.
LI nani Hilo?
 
Back
Top Bottom