DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

DP-World-Cochin-records-highest-ever-Monthly-Volumes-750x420.jpg

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 67% katika Bajeti ya Tanzania

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

 
DP world wapewe majengo ya CCM miaka 5 tuone maendeleo ila sio Bandari
Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.

Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.

Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
 
Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.

Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.

Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
Kama wewe unavyopotosha hapa kwamba DP world ni watu wema?
 
Pato la taifa Kwa maana ni GDP(ama GNI),Kwa hizo takwimu ni uongo. Bandari pekee haiwezi changia kiwango hiko.

Mnaelezea faida ambazo ni matazamio Tu Ila mbona mnashindwa kueleza vipengele vyenye utata kwenye ule mkataba.

Tufafanulie na wengine tuelewa kifungu cha 23 ibara ya 4 kutoka kwenye huo mkataba.
 
Wewe ni mjinga na hujui chochote zaidi ya uchawa! Na ndio maana unaita " Bandali"!

Huwezi ku- run Bandari bila storage! Kuna watu mzigo unafika hajapata fedha za kulipia mzigo wake na hivyo lazima Bandari iu- store huo mzigo kwa gharama za mteja (demurrage ).

Vijana wa UVCCM hakuna mnachojua kwenye dunia ya uchumi!
Nyie fanyeni kazi za Uchawa mkivizia teuzi basi!
 
Mkataba wake ni wa mda gani?
Mkuu, watu wanapotosha, hakuna Mkataba uliojadiliwa. Wakianza kujadili Mkataba ndio wataweka muda. Haya ya sasa ni Maazimio tu ya kufanya biashara ya bandari kati ya Nchi na Nchi. Hata Bunge limepitisha maazimio. Kama maazimip yakikubalika ndipo mikataba sasa inaanza. Yaani hii ni kama barua ya Posa, bado mwali kuolewa.
 
Vipi kuhusu ushuru wa magari utashuka au ndio yale yale ya kodi 110% ya bei ya kuagiza?
Mkuu, DP World wao wanajihushisha na kupakua na kupakia Makontena kiufanisi zaidi na kwa haraka.

Na wanachukua sehemu ya bandari tu. Ile sehemu ya Magari bado itaendelea kuendeshwa na TPA. Labda waamue kumpa muwekezaji mwingine. DP World watakuwa kama ilivyokuwa TICTS.
 
Back
Top Bottom