Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waambie waliokutuma wakagawe bandari za Zanzibar na sio TanganyikaMkuu, watu wanapotosha, hakuna Mkataba uliojadiliwa. Wakianza kujadili Mkataba ndio wataweka muda. Haya ya sasa ni Maazimio tu ya kufanya biashara ya bandari kati ya Nchi na Nchi. Hata Bunge limepitisha maazimio. Kama maazimip yakikubalika ndipo mikataba sasa inaanza. Yaani hii ni kama barua ya Posa, bado mwali kuolewa.
Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 97%
Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka ...
View attachment 2658110
Ndio. Wanachukua nafasi ya TICTS sababu ilikosa ufanisi. Sema watu wamepotoshwa na Wanaharakati. Marekani na Uingereza hawapendi kuona Afrika tukijikomboa. So ndo maana unaona mambo ni mengi. Waarabu na Wachina wakiingia Afrika Wazungu hawana chao. Ndo maana wanawachanganya watanzania ili Washindwe then aje apewe kibaraka mmoja. Utashitukia eti Lowassa kapewa bandari mtu ambaye hana uzoefu wala vifaa.Wanachukua nafasi ya ile kampuni ya Karamagi
Kwahiyo kuuza nchi ni kuleta manufaaMimi sio chawa na jitambua siwezi ni kapinga kitu cha kjleta manifa katika nchi ili kufurahisha wachache.
Nimekulia makuzi na madhira na maudhi ya muwekezaji hewa anaitwa Anger trust lmtd asie na ofisi wala anuani. Siwezi kuwa sehemu ya kuunga mkono wawekezaji kutoka bala asia daima dumu.Mkuu kuazimia kitu ni kuuza? Sikiliza pande zote kabla ya kuhukumu.
Ubaya wa kuuza Bandari zote Tanganyika Kwa DP world ni mwingi sana kuliko uzuri wa kuwauzia Bandari DP world zote za Tanganyika.Mkuu kila kitu kina ubaya wake na uzuri wake. Ila chenye uzuri mwingi kuliko ubaya hicho kinafaa kuliko chenye ubaya mwingi kuliko uzuri
Unauzaje Bandari zote?Kwahiyo Mkuu, unataka TICTS arudi ndo mtu aonekane sio chawa wa Samia. Tuambia wewe basi mtazamo wako ni upi. Ukute una point za kusaidia kuboresha mambo ya Uwekezaji.
Mngewapa DP world waendeshe bunge sio bandari. Maana bungeni wamejaa vilaza wengi.Salaam Wakuu,
Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.
View attachment 2658109
Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.
Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.
Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.
Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.
Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.
Nimewapenda bure DP World.
Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?
Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.
Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.
Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.
Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.
Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.
Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 97%
Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.
Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.
Watanzania tujitafakari na tujielewe.
Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?
Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.
Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.
View attachment 2658110