Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
- Thread starter
- #61
Asante kwa matusi. Pia samahani kwa typing errors.Wewe ni mjinga na hujui chochote zaidi ya uchawa! Na ndio maana unaita " Bandali"!
Huwezi ku- run Bandari bila storage! Kuna watu mzigo unafika hajapata fedha za kulipia mzigo wake na hivyo lazima Bandari iu- store huo mzigo kwa gharama za mteja (demurrage ).
Vijana wa UVCCM hakuna mnachojua kwenye dunia ya uchumi!
Nyie fanyeni kazi za Uchawa mkivizia teuzi basi!
Sasa turudi kwenye hoja.
Bandari yetu ni ndogo ni kama Mwaro tu. Meli kupakua hadi zisubiriane kule maji marefu. Bandari yetu inakosa ufanisi na Teknolojia ndo maana unaona mambo ya Storage. Meli inapakuliwa mzigo kwa siku nne badala ya siku moja kwa ukosefu wa vifaa. Unaenda kutoa mzigo unaambiwa system ipo down. Au unaenda kutafuta Kontena lako haulioni wala haujui lipo ICD ipi unatumia hata wiki kulitafuta. Halafu ukienda unakuta storage ya kufa mtu watu wanaamua kutelekeza mzigo.
Kingine mifumo ya bandari haisomani. Inafanya mzunguko leo upo TRA kesho upo Bandari kitu kilekile.
Nchi ikasema hapana. Tutafute mtu wa kuendesha ili kuwapunguzia usumbufu watanzania.
Pale Kurasini kuna eneo la EPZ Authority, anapewa na kutengeneza ambapo mizigo yote itachukuliwa pale. Wa Mikoani zipo Bandari kavu zishaanza kujengwa Pwani na Dodoma. Malori hakuna haja ya kufika Dar.
Yaani Kontena ikifika Bandarini kila kitu kinakuwa tayari. Yaani mzigo unapakiwa kwenye meli ukishalipa kila kitu. Yaani ni kushusha na kuchukua mzigo wako. Ni kama mwendo kasi, ikifika ni kupanda sababu tiketi ushalipa mapema. Na pale EPZA utapewa muda wa kutosha wa kuchukua muzigo. Ukichelewa kwa muda ndo utaanza lipishwa storage