DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA

Hakuna haja ya kupanick wafanyakazi hicho ni kitu cha kawaida
Mashirika yote ya umma huwa na mikataba ya hali bora na wafanyakazi kupitia mabaraza yao ya wafanyakazi inayoainisha endapo kutatokea ajira kusimama au retrenchment mfanyakazi atalipwa nini na huwa sio siri iko wazi

Mwekezaji mpya akija aweza sema nachukua wafanyakazi wote au baadhi tu hawa ndio nitaendelea nao kwa mikataba mipya ila haruhusiwi.kuwashusha mishahara akiwachukua.Atakaokataa kuwachukua huachia kampuni yao wajue watawafanyaje kama hawana pa kuwapeleka huwataka wanaotaka kuondoka kwa hiari waandike barua kuondoka na malipo huwa makubwa kuliko akisubiri kustaafu kawaida

Kampuni binafsi wazoefu kwenye hili hasa za mafuta kila siku mwekezaji mpya huja utasikia leo kampuni inaitwa Caltex kesho anakuja mwekezaji mpya inaitwa BP keshokutwa inauzwa anakuja mwekezaji mwingine anaitwa Puma kila akija mpya mikataba ya wafanyakazi husainiwa upya anaowataka mwekezaji mpya asiowataka wanalipwa Chao wanaendelea na maisha.mengine Sema watu wa mashirika ya umma wanaona kitu kigeni lakini kitu cha kawaida sana akija mwekezaji mpya kampuni binafsi
 
1. Kama nakumbuka vizuri! Tuliambiwa DP watapewa gati no 7&8 pekee!..sasa mbona hapo wamepewa gati zaidi ya hizo?

2..TPA wamebaki na gati ngapi?.
Hizo zilikuwa danganyà toto tu TPA wanabaki na sehemu ya wavuvi hata ile sehemu ya tics anakuja kupewa Dp na reli ikikamilika bandari za maziwa zinaenda kwa dp salamaleko
 
DP wana world class standard hakuna longo longo kama unajijua wewe unga unga mwana bora bakia TPA....wako very strictly watanzania nawajua wataanza kulalamika soon.....wako atrictly niamini mm
 
Sifa uwe unaitwa Ally,Hussein, Mohamed,Iddy,Yusufu au abdalah..nyie akina John,Frank,George msijichoshe
Na msikiti Utajengwa humo humo ndani, muda utaongea tu hawa Akina Tippp Tipp wamepewa Nchi na Elimu yao tunaenda kuifundisha Shuleni! Mungu atusimamie na hawa Wakoloni waliotugeuza watumwa. Daaaah
 
Bandari imekuwa kama Simba SC Wana Makolo 🐼
 
Kwahyo hakutakuwa na wajiriwa wapya??
Wanakuwepo critical areas
Ujue wawekezaji wakija huja na teknolojia mpya ambazo huhitaji wanaozijua na serikali haiwezi kubali waje nao wakati watanzania wapo wanaozijua wakati TPA ilikuwa ikiendeshwa teknolojia za zamani hawakuhitaji vijana wajua teknolojia mpya

Aliyesoma mfano computer technology miaka ya 1980 huwezi linganisha na aliyesoma computer technology na kumaliza digrii mwaka jana Wa mwaka jana yuko more current na yuko advanced kuliko obsolete technology ya TPA iliyopo hivyo wataajiri vijana wapya

Pili wa marketing wengi wa TPA mfano wamesoma kingereza tu na digrii za kingereza tu hawana third language kama kifaransa .Soko la TPA liko hadi Central Africa nchi ya kongo ambako lugha kuu kifaransa
Definitely wataajiri watanzania vijana wapya marketing officers wenye digrii za marketing lakini wanajua kifaransa kwa ajili ya kuwa marketing officers wao soko la Kongo tofauti na TPA ambayo ilikuwa haijali hilo kuwa na maafisa masoko wajua kifaransa ambako kuna wateja wengi mizigo ipitayo bandarini

Wapya wataajiriwa wala sio siri.Kuna maeneo wafanyakazi wa TPA waliopo hawawezi enea hata wajitutumue vipi
Degree zao na uzoefu wao haywezi fit kwenye teknolojia za kisasa na utendaji wa kibiashara za kimataifa wa kisasa uletwao na DP World

Mfano Dp world ni kampuni ya kimataifa Auditor na wahasibu wakuu lazima wawe na certification za kimataifa ili wakisaini document wanahisa wa DP World wawe na confidence ya kuanzia mhasibu mkuu au mkrugenzi wa fedha sio awe na Sifa za CPA ya Tanzania awe mhasibu au Auditor wanatakiwa wenye certification za kimataifa kama ACCA nk sio CPA (T) International shareholders wa kampuni yeyote ya kimataifa huhitaji wenye certification za kimataifa.Na wapo na serikali haiwezi kubali waajiri wa nje wakati Tanzania wapo.TPA ilikuwa haiwahitaji hao wenye certification za kimataifa .Hiivyo ajira mpya zitakuwepo

Watanzania wenye sifa za kimataifa ajira zitakuwepo nyingi vitengo vyote iwe IT ,uhasibu,masoko,procurements,Engineering,Port operations etc wataajiri tu hawana ujanja
 
Sijaona anaeondolewa, au huelewi ulichokibandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…