DP World kuchukua Eneo la Chuo Cha Polisi Kurasini

DP World kuchukua Eneo la Chuo Cha Polisi Kurasini

Mambo ya mkataba yameanza utekelezaji haraka sana, huku mipango ikianza kufanyika Ili ndugu zetu DP world waanze kufanya kazi mara moja.

Sijui mambo ya Mikataba, lakini DP world katika mkataba wao watachukua pia Eneo la Chuo Cha Polisi Kurasini Kinachosimamiwa na kamishna Msaidizi Mambo Sasa.
Sijajua kwanini serikali haitagazi hatua mbalimbali zinazoendelea za utekelezaji wa mkataba huu , ambao Umekuwa ukipingwa Kwa nguvu na watu wanna, Mwabukusi, Slaa, Padri kitima na Mdude.

Wataalamu Wa serikali na wawakilishi wa DP world walitembelea maeneo ya chuo Cha Polisi Kurasini na kufanya na kuchua vipimo vya mipaka, huku dp world ikijiandaa kulipa fidia zote za uhamishaji wa chuo hicho Cha jeshi.

Jingine linaloendelea , ambalo silijui rasmi. Ni kuwa DP world ataingiza magari zaidi ya 2000 yaani maroli Kwa ajili ya kisafirisha mizigo nje ya nchi, inavyosemekana DP world ndio atakuwa transporter pekee wa kisafirisha mizigo nje ya nchi, na watanzania watabaki Tanzania.p

Hizi ni habari zinaukweli lakini nashangaa kwanini Serikali ya Chama Tawala haitoi maendeleo ya utekelezaji wa mradi huu ambao unaendelea kimya kimya kama alivyosema Mangwea "KIMYA KIMYA"
DPW inatugawa kama Taifa
 
Kwa hili sitavumilia nipo tayari nijichome moto hadharani kwaajili ya watanzia wenzangu, labda Dp world wakinipa mgao na mimi ndo ntakaa kimya

Bila hivyo ntajichoma moto hadharani
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kama chuo kinapelekwa sehemu nyingine kuna shida gani? Kwani wanachukua kuondoka nalo ?
Kwanini na Ikulu na Chuo Kikuu vyote wasivihamishe eneo liwe kubwa zaidi ?

Sababu naona hakuna shida yoyote la kuhamishwa kama unakwenda sehemu nyingine..
 
Kwa hili sitavumilia nipo tayari nijichome moto hadharani kwaajili ya watanzia wenzangu, labda Dp world wakinipa mgao na mimi ndo ntakaa kimya

Bila hivyo ntajichoma moto hadharani
Mambo ya Tunisia yalianza hivi hivi kiutani[emoji2][emoji51][emoji26],serikali iachane na mkataba
 
Duh, hivi kweli wewe ni Mtanzania? Mbona kila hoja inayoigusa DPW unajitokeza kutetea? Hivi una maslahi gani na hao wageni?

Unakata sana aise
Huyo ni mmojawapo ya wanaofaidi asali mkuu
 
Back
Top Bottom