DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)

Hayo mazingira ya wanasiasa kupewa ziara za kutalii huko dubai ni kitu gani, pambav.....mnataka kutufunga midomo wakati kila kitu kinajulikana, bila kuwa na maslahi binafsi utaingiza nchi kwenye mkataba wa hovyo namna hiyo?

Mkataba huo hapo tuoneshe u"hovyo" wake uko wapi?

Au wewe mkatoliki?
 
Mkataba huo hapo tuoneshe u"hovyo" wake uko wapi?

Au wewe mkatoliki?
Nina maswali mawili tu nijibu tafadhali.

1. Mkataba utakoma lini?

2. Je, tunaweza kuuvunja mkataba huu ikiwa hatutaridhishwi na mwekazaji kutokidhi matakwa ya mkataba huu?
 
Mbona hujatuwekea hata kifungu kimoja kilicho kibaya?


Mkataba huo hapo post #1 upo wa Kiswahili na Kingereza, tuwekee kifungu unachoona wewe kibaya, tuone kama hakijibiwi na mkataba wenyewe wa IGA.
IBARA 4 (2) kwamba Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi. Yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai Tena kwa Mali zake? Huu ujinga ubaki CCM na Dubai.
 
Mbona hujatuwekea hata kifungu kimoja kilicho kibaya?


Mkataba huo hapo post #1 upo wa Kiswahili na Kingereza, tuwekee kifungu unachoona wewe kibaya, tuone kama hakijibiwi na mkataba wenyewe wa IGA.
IBARA 4 (2) kwamba Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi. Yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai Tena kwa Mali zake? Huu ujinga ubaki CCM na Dubai.
 
Hapo hapo bandarini kutakuwa na wawekezaji wawili, Bagamoyo atakuwepo mwekezaji mwingine.
 
Nina maswali mawili tu nijibu tafadhali.

1. Mkataba utakoma lini?

2. Je, tunaweza kuuvunja mkataba huu ikiwa hatutaridhishwi na mwekazaji kutokidhi matakwa ya mkataba huu?
Kikomo cha mkataba wowote wa IGA ukomo wake ni pale mnapouvunja, iwe mwezi, iwe mwaka, iwe miaka 50.

Soma kifungu cha 23 cha mkataba kwa ukamilifu wake kinajibu maswàli yako yote mawili. Jisomee:

KIFUNGU CHA 23
MUDA NA UTARATIBU WA KUSITISHA MKATABA


1. Kwa mujibu wa aya ya 2 ya ibara hii ya 23, Mkataba huu utaendelea kutumika hadi pale itakapotokea mojawapo ya yafuatayo: (i) kusitishwa kabisa kwa shughuli zote za mradi; au (ii) kumalizika muda kwa HGA zote na Mikataba yote ya Mradi (pamoja na ya nyongeza yoyote ya muda itakayo fanyika) na utatuzi wa migogoro, ikiwa ipo, kama inavyoelezwa hapochini.
2. Iwapo HGA itasitishwa kabla ya muda wake kuisha, Mkataba huu utaendelea kutumika kwa muda huo, na kwa kiwango kinachohitajika na Nchi yoyote Mwanachama au Kampuni ya Mradi kudai haki zozote zinazotokana na, kulinda maslahi yoyote yanayohatarishwa na au kuleta shauri lolote linalotokana na kusitishwa kwa HGA. Kusitishwa au kuisha muda kwa HGA hakutaathiri haki zozote zilizopatikana, madeni au masuluhisho ya Mwanachama yeyote chini ya HGA hiyo au Mikataba ya Mradi inayohusiana au Mkataba huu.
3. Kusitishwa kwa Mkataba huu kutategemea idhini ya awali ya Nchi Wanachama, idhini hiyo haipaswi kuzuiliwa bila sababu.
4. Nchi Wanachama hazitakuwa na haki ya kushutumu, kujiondoa, kusimamisha au kusitisha Mkataba huu katika hali yoyote, hata ikitokea ukiukwaji wa mkataba (material breach), mabadiliko ya kimsingi ya hali, kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia au kibalozi, au sababu zingine zozote zinazotambuliwa chini ya sheria ya kimataifa. Bila kujali yaliyotajwa hapo juu, mgogoro wowote kati ya Nchi Wanachama kuhusiana na hali kama hizo utashughulikiwa kulingana na mahitaji ya Ibara ya 20 ya Mkataba huu.
 
Kwa akili ya kawaida unaona kilichoandikwa hapo ni sahihi ndio majibu ya maswali ya hapo juu?. Unaweza kuingia mkataba bila kujua ukomo wake? maneno Nchi wanachama hazina HAKI ya KUJIONDOA au KUSITISHA mkataba huu kwa hali YOYOTE hata kukitokea ukiukwaji wa mkataba kwako wewe ni sawa? ni kichaa peke yake ndiye anaweza kusign mkataba wa aina hii.
 


Ndivyo mnavyojidanganya?

Mmechelewa jamvini karamu imeshaliwa.
 
Kama ilisainiwa nchi ya waarabu.Alipata muda gani wa kuusoma mkataba na kujirishisha!??Kwa Nini mkataba usainiwe nje na SIYO ndani ya TZ?
ALIKUWA NA haraka gani za kusaini.
Nyumbani NI sehemu salama kwa mtoto.Ifike kipindi Bibi atulie nyumbani,wakihitaji kuwekeza watamfata na sio yeye kuwafata..
 
[emoji4][emoji4]
Kwanini Watu hawaamini Akili na maamuzi ya viongozi wao?

HAYA NI BAADHI YA MADUDU

Sehemu ya pili , kifungu cha 2 kuhusu lengo la mkataba je ndo lile wanalisema ccm kwenye majukwaa?

Sehemu ya pili kifungu cha 3 aya B , inataka siri zitunzwe dhidi ya nani? je ni siri Ipi hasa ? kwamba serikali ikiona madudu bandarin , hawana haki ya disclose kwa jamii mpk kibali?

Sehemu ya 2 kifungu cha 4 aya namba 2 inatulazimu kuwajulisha dp world kwa fursa yoyote kwenye waterbodies zetu then wao ndo watoe go ahead au waje wawekeze

Sehemu ya 2 kifungu cha 4 aya ya 5 kinaonesha kuwa DPW ni madalali tu wala wao hawana cash mfukoni ila serikalo haistuk kwann uweke middleman wkt unaeza fanya biashara ya moja kwa moja na mwenye hela

Bila kusahau kifungu cha 7 aya ya 3 inatufunga kutoweza fanya marekebisho ya vibali vyetu mpk tuwasiliane nao kwanza so maboresho yoyote ya na hayawahusu mpk waridhie

Pia kifungu cha 23 hakioneshi muda , wenzetu SA na Ufilipino wameweka mkataba wa miaka 25 sisi je ?

kifungu cha 23 kinaidhinisha mkataba huu kutotambua sheria za kimataifa kbs , huu sio uhuni sasa ?

Ngoja tujifukize [emoji16]
 
Mtu unashindwa kuandika hata sentensi moja ya Kiswahili ilinyooka, halafu bado unaamini una akili timamu?


Wacha porojo,mkataba wa IGA huu hapa post namba 1, tuoneshe huo wa kuendesha bandari anaewadanganya huyo poyoyo mwenzenu uko wapi?

Msifikiri Watanzania wote ni kondoo kama nyinyi.
 
Tuoneshe hicho kipengele cha "milele" kiko wapi?

Mkataba huo hapo post#1.
 
Nina maswali mawili tu nijibu tafadhali.

1. Mkataba utakoma lini?

2. Je, tunaweza kuuvunja mkataba huu ikiwa hatutaridhishwi na mwekazaji kutokidhi matakwa ya mkataba huu?
Hata bila reference Hakuna mkataba usiyo vunjika
Ukomo ni miaka 30 kwa term ya mi5tano
 

Kwahiyo mikataba yote miwili unaunga mkono??ukija Tena watatu ....unaunga mkono???dandara kweli ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…