DP world na Ongezeko la Ajira 43,907 Bandarini

Full 8

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
313
Reaction score
271
Uwekezaji wa DP world katika bandari zetu Tanzania, umepokelewa kwa mitazamo tofauti. Wengi wameonesha kutokubaliana nao kwa asilimia kubwa na kudai maboresho kadha wa kadha kwa manufaa ya nchi yetu huku wanaoupigia chapuo wakisema mkataba huo ni bora na utasaidia kuboresha utendaji bandarini na kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Kufuatia wasilisho lilitolewa na waziri mwenye dhamana, inaonekana kwamba kutakua na ongezeko la ajira bandarini kutoka 28,000 mwaka 2021/22 hadi 71,907 2032/33 sawa na ajira mpya 43907 ambalo ni ongezeko la asilimia 157, bila shaka ongezeko hili kubwa la ajira ni habari njema kwetu sote.

Kufuatia habari hiyo nikachukua muda kufiriki namna ajira hizo mpya zitatengenezwa. Nikabaini kuwa zaweza kuwa katika makundi haya.
1. Operators
2. IT
3. Administrators
4. Drivers
5. Engeneers n.k

Pia, nikajiuliza katika miaka kumi ijayo, ajira hizi zitakuwa na soko? ndipo nikakumbuka zimwi la AI.
Ukitazama promotion video za DPW utaona bandari inayoendeshwa kisasa kwa kutumia semi au automatic machinery na wafanyakazi wachache. Jambo hili pia lilishuhudiwa na mbunge yule mwenye phd aliyemwona binti mdogo anabonyeza tu container zinajipanga, akachukua na namba ya simu kwa follow-ups! mbali na AI, nikakumbuka kuwa mwekezaji mpya pia atakuaja na skilled labor kutoka uarabuni ili kuwezesha shughuli zake kwenda vema, hivyo kuna ajira ambazo hatutazipata.

Ndipo nilipogundua kuwa pamoja na maneno mazuri ya waziri mwenye dhamana, ndoto hii ya ajira nyingi inaweza isifikiwe kwa sababu AI imeshika kasi katika sekta zote hadi upasuaji wa wagonjwa, vile vile ukilinganisha faida za Automation na machinery katika kampuni utaona kuna faida zaidi kuajri roboti kuliko watu maana haziugui, haziibi, hazina maternity and perterty leave, hazidai mshahara na zinafanya kazi kwa masaa mengi tofauti na mwanadamu.

Hivyo nawiwa kusema kuwa tusiwe na matarajio makubwa ya ajira katika uwekezaji huu kwani kama watawekeza kama wanayodai yaani uwekezaji wa kisasa, ajira nyingi zitakufa; na kama wakiendeleza hali iliyopo sasa ufanisi hautafikiwa.

Ni hayo tu kwa leo.

Full 8.
 
Ndipo nilipogundua kuwa pamoja na maneno mazuri ya waziri mwenye dhamana, ndoto hii ya ajira nyingi inaweza isifikiwe kwa sababu AI imeshika kasi katika sekta zote hadi upasuaji wa wagonjwa, vile vile ukilinganisha faida za Automation na machinery katika kampuni utaona kuna faida zaidi kuajri roboti kuliko watu maana haziugui, haziibi, hazina maternity and perterty leave, hazidai mshahara na zinafanya kazi kwa masaa mengi tofauti na mwanadamu,
Huu ndio ukwelia
 
Huwa namsikilizaga sana JACK MA founder wa ALIBABA

HUPENDA KUSEMA DON'T FEAR FOR THE FUTURE & TECHNOLOGIES....

Yeye aliwai kumchukia founder wa Microsoft bwana BILL GATES kua uvumbuzi wake ungewanyima ajira watu......

All in all, apart from uvumbuzi wa Al, still human resources ni muhimu zaidi na hakuna haja ya kuhofia Technologies

Wasalaam 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Uwekezaji wa DP world katika bandari zetu Tanzania, umepokelewa kwa mitazamo tofauti. Wengi wameonesha kutokubaliana nao kwa asilimia kubwa na kudai maboresho kadha wa kadha kwa manufaa ya nchi yetu huku wanaoupigia chapuo wakisema mkataba huo ni bora na utasaidia kuboresha utendaji bandarini na kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania.

Kufuatia wasilisho lilitolewa na waziri mwenye dhamana, inaonekana kwamba kutakua na ongezeko la ajira bandarini kutoka 28,000 mwaka 2021/22 hadi 71,907 2032/33 sawa na ajira mpya 43907 ambalo ni ongezeko la asilimia 157, bila shaka ongezeko hili kubwa la ajira ni habari njema kwetu sote.

Kufuatia habari hiyo nikachukua muda kufiriki namna ajira hizo mpya zitatengenezwa. Nikabaini kuwa zaweza kuwa katika makundi haya.
1. Operators
2. IT
3. Administrators
4. Drivers
5. Engeneers n.k

Pia, nikajiuliza katika miaka kumi ijayo, ajira hizi zitakuwa na soko? ndipo nikakumbuka zimwi la AI.
Ukitazama promotion video za DPW utaona bandari inayoendeshwa kisasa kwa kutumia semi au automatic machinery na wafanyakazi wachache. Jambo hili pia lilishuhudiwa na mbunge yule mwenye phd aliyemwona binti mdogo anabonyeza tu container zinajipanga, akachukua na namba ya simu kwa follow-ups! mbali na AI, nikakumbuka kuwa mwekezaji mpya pia atakuaja na skilled labor kutoka uarabuni ili kuwezesha shughuli zake kwenda vema, hivyo kuna ajira ambazo hatutazipata.

Ndipo nilipogundua kuwa pamoja na maneno mazuri ya waziri mwenye dhamana, ndoto hii ya ajira nyingi inaweza isifikiwe kwa sababu AI imeshika kasi katika sekta zote hadi upasuaji wa wagonjwa, vile vile ukilinganisha faida za Automation na machinery katika kampuni utaona kuna faida zaidi kuajri roboti kuliko watu maana haziugui, haziibi, hazina maternity and perterty leave, hazidai mshahara na zinafanya kazi kwa masaa mengi tofauti na mwanadamu.

Hivyo nawiwa kusema kuwa tusiwe na matarajio makubwa ya ajira katika uwekezaji huu kwani kama watawekeza kama wanayodai yaani uwekezaji wa kisasa, ajira nyingi zitakufa; na kama wakiendeleza hali iliyopo sasa ufanisi hautafikiwa.

Ni hayo tu kwa leo.

Full 8.

Msitupigie kelele
 
Huwa namsikilizaga sana JACK MA founder wa ALIBABA

HUPENDA KUSEMA DON'T FEAR FOR THE FUTURE & TECHNOLOGIES....

Yeye aliwai kumchukia founder wa Microsoft bwana BILL GATES kua uvumbuzi wake ungewanyima ajira watu......

All in all, apart from uvumbuzi wa Al, still human resources ni muhimu zaidi na hakuna haja ya kuhofia Technologies

Wasalaam 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Ni kweli mkuu lakini kuna ajira ambazo zimetoweka kutokana na kukua kwa sayansi na tech mfano ajira za kutumia nguvu migodini na viwandani ambazo zimechukuliwa na roboti.
 
Back
Top Bottom