DP World walifukuzwa Yemeni (Aden Port)

DP World walifukuzwa Yemeni (Aden Port)

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kwanini viongozi wetu hawataki kujifunza makosa ya nchi zingine zilizowahi kuingia mikataba ya aina hii na DP World.

Mwaka 2008 Yemeni waliingia mkataba wa miaka 30 kwa bandari yao ya Aden Port na DPW na kusainiwa haraka haraka na rais wa wakati huo aliyekuwa anamaliza muda wake Rais Ali Abdullah Saleh, lkn ndani ya miaka 4 bandari iliingia hasara kubwa, Yemeni ikavunja mkataba DPW wakafukuzwa.

Kwenye mkataba huo Yemeni iliahidiwa kama huu wa kwetu kuwa DPW wataongeza ufanisi wa Bandari kwa kuhudumia makontena kutoka 500,000 hadi 900,000 kwa mwaka lkn ndani ya miaka 2 yakapungua hadi chini ya makontena 140,000 kwa mwaka, yaani chini ya uwezo iliokuwa nao kabla ya DPW kuja.

“The contract with DP World failed to deliver the needed “fresh start” because the government agreed terms that were too favourable to the company.

The DPW promises under the contract to raise container traffic from 500,000 20ft-equivalent units a year in 2008 to 900,000 had faltered, with throughput dropping as low as 140,000 a year in 2011.” Yemen Official.

 
Bandari zote Tanganyika, amepewa milele, na ameshaanza kazi field tangu October 2022, nimeona mahali unaandika upuuzi eti bado mkataba rasmi kati ya serikali ya mkoloni wa Tanganyika na mwarabu haujasainiwa, wewe ni juha muongo.
Nipe ushahidi ameanza kazi kwenye field gani? Nipe kipengele pia kinachosema amepewa bandari zote
 
Huko Yemen walifukuzwa kwa sababu Yemen nchi ya Wakristu. Hawakupendezwa na Waarab tena Waislam kupewa bandari yao.

Yemen wabaguzi sana. Hawawapendi Waarab na Waislam
Walifukuzwa Marekani wakafukuzwa UK, walifukuzwa Djibouti wakafukuzwa Somalia, walifukuzwa Belgium wakafukuzwa Port of Fallujah huko kwao, wamekataliwa Kenya na nchi nyingi tu, hata hapa kwetu watafukuzwa tu.
 
Tuseme wewe ndo mwekezaji na umewekeza Yemen!! Niambie na machafuko pamoja na vita vile utaongezaje ufanisi wa Bandari?

Tuambie pia kwa Bandari anazoziendesha Uingereza. Canada na Dubai anaziendeshaje?
Ndio maana tunasema mikataba yao ni ya kijanja kijanja sana utaingiaje mkataba huku ukijua kuna machafuko na wakati huo huo unaahidi ufanisi, kama sio bribery kwa viongozi ni kitu gani.
 
Ndio maana tunasema mikataba yao ni ya ujanja ujanja sana utaingiaje mkataba huku ukijua kuna machafuko na wakati huo huo unaahidi ufanisi, kama sio bribery kwa viongozi ni kitu gani.
Hadi Southampton wameingia mkataba wa kiujanja ujanja?
 
Nipe ushahidi ameanza kazi kwenye field gani? Nipe kipengele pia kinachosema amepewa bandari zote
Kasome Article 2 ya ule mkataba; Objectives of the Agreement.

Ile imeonesha vizuri kabisa kila kitu, jinsi makubaliano yale yalivyokuwa legally binding, ndio maana nakwambia mwarabu ameshaanza kazi tangu October 2022, maeneo yote ambayo waarabu watafanya shughuli zao Tanganyika, ambapo pameeleza wazi ni bandari zote za bahari na maziwa Tanganyika.

Nikushauri tu, kwa hili la mkataba wa bandari na waarabu, chutama, usiendelee kujivua nguo humu.
 
Hii inaonesha kabisa hawa jamaa zetu walihongwa kuipa kazi hiyo kampuni, hawakufanya uchunguzi wowote kabla, kuna watu ni wa kunyongwa nchi hii.
Tukianza naaa...................
 
Hadi Southampton wameingia mkataba wa kiujanja ujanja?
Umeuona mkataba wao ni wa milele kama wetu, kuna nchi zina utawala smart viongozi waliochaguliwa na wananchi hawawezi kukubali mikataba ya hovyo kama yetu yenye viongozi corrupt.
 
Back
Top Bottom