DP World yakabidhiwa rasmi Bandari ya Dar es Salaam

DP World yakabidhiwa rasmi Bandari ya Dar es Salaam

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wakati Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikikabidhi Bandari ya Dar es Salaam kwa Kampuni ya DP World, Serikali inaangalia namna ya kufanya upanuzi wa bandari hiyo ili kuendana na ongezeko la mizigo inayohudumiwa.

Hiyo ni baada ya baadhi ya wamiliki wa migodi kutoka nchi jirani pia kuonyesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam na Kigoma kwa ajili ya kusafirisha mizigo yao.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema DP World ilianza kazi Aprili 7, 2024 licha ya kuwa TPA inamalizia baadhi ya vitu kabla ya kuachia kila kitu chini ya mwendeshaji huyo.

Hayo yameelezwa leo Juni 3 2024 wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Ali Possy alipofika Bandari ya Dar es Salaam kuangalia namna shughuli zinazofanyika baada ya DP World kuanza utekelezaji akiambatana na ujumbe kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac).

Oktoba 22, mwaka jana Serikali iliingia makubaliano na DP World kupitia mikataba mitatu iliyosainiwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika bandari hiyo kwa miaka 30.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mrisho amesema kilichobakia chini ya TPA ni baadhi ya meli zilizokuwa zimesajiliwa katika mifumo ya TPA ambazo ni lazima wazihudumie.

“Shughuli hazijasimama pamoja na makabidhiano hayo, changamoto kama wadau fulani walizungumza kuhusu mifumo ndiyo hiyo tunayosema transition tunaimarika sana na hiyo mifumo wanayoizungumzia ya DP World, nadhani baada ya muda tutakaa sawa zaidi, kazi zinaendelea, gati zote zimejaa meli na meli zinahudumiwa,” amesema Mrisho.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Ali Possi amesema wakati watoa huduma hao wakianza kazi, lengo la Serikali ni kuona ufanisi unakua kama ilivyokuwa imetarajiwa.

MWANANCHI

Pia Soma:
- DP World kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DPW au kubaki TPA


- DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7
 
Kwani ilikuwa bado haijakabidhiwa rasmi ili ianza kufanya kazi kwa ufanisi?
 
Kwani ilikuwa bado haijakabidhiwa rasmi ili ianza kufanya kazi kwa ufanisi?
 
Kwani mwanzo na sasa tofauti ni ipi katika baadhi ya vipengele ikiwemo bei ya kupakua, utunzaji na gharama zake??
 
Nenda vita umeimaliza ☺☺☺
 
Kwa hiyo kapewa halafu Serikali inampanulia bandari tena?

Kwa hiyo huo mkataba wake yeye ni kuingiza mihela tu upanuzi unaofanywa na Serikali yeye hausiki?
 
Kuna siku haya yatasikika kila kona na itakuwa aibu kubwa. Hakuna anayeishi milele. na mpaka sasa experiments za ujanja ujanja na ukanjanja kwenye mambo makubwa, umefeli
👍
 
Back
Top Bottom