DPP awafutia kesi Maimu, wenzake wawili mashtaka 10 ya utakatishaji fedha

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
FRIDAY OCTOBER 22 2021

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) amewafutia mashitaka 10 ya utakatishaji fedha washtakiwa watatu kati ya watano akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu.

Mbali na Maimu washitakiwa wengine waliofutiwa mashitaka hayo ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida, George Ntalima na Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 55 likiwamo utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya amedai leo Oktoba 22 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kutajwa lakini wanakusudia kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.

Amedai kesi hiyo iko katika hatua za usikilizwaji lakini Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) amekusudia kufanya marekebisho madogo chini ya kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

"Jumla ya mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ni 55, baada ya marekebisho haya yatakuwa mashtaka 45, kwa mshtakiwa wa kwanza Dickson Maimu, mshtakiwa wa tatu, George Ntalima na wa nne Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo ambao wameondolewa mashtaka ya utakatishaji fedha," amedai Wakili Komanya.

Wakili Komanya amedai endapo hakutakuwa na pingamizi, wangeomba kuwasilisha hati mpya, hata hivyo hati hiyo haikupokelewa kutokana na Hakimu Mkazi Mkuu Rashid Chaungu anayesikiliza kesi kutokuwepo.

"Hata mkiwasilisha hati mpya, kesi hii haiko haiko mbele yangu, nawashauri muiwasilishe mbele ya Hakimu husika tarehe itakayopangwa, na kuhusu dhamana nawashauri kuwasilisha maombi Mahakama Kuu," alieleza Hakimu Shaidi.

Baada ya maelezo hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4 mwaka itakapotajwa ambapo upande wa mashtaka utawasilisha hati mpya.

Katika kesi hiyo, tayari upande wa mashitaka umeshafunga ushahidi kwa kuwaita jumla ya mashahidi 26 pamoja na kuwasilisha vielelezo 45.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Meneja Biashara wa (Nida), Aveln Momburi na Mkurugenzi wa Sheria, Sajina Raymond.

Mwananchi
 
Taaratibu pengine DPP anakaribia faili la Mwenyekiti na wenzie 3 ktk kesi namba 16 / 2021, hivyo anatuma ujumbe wa moshi mweupe utaonekana ukitoka kuashiria habari njema. Moshi mweupe ktk jumba la Papa kule Vatican huashiria habari nzuri.

HISTORIA YA MOSHI MWEUPE

White smoke appears at the Vatican, signaling that a new pope has been chosen by the cardinals.

Source: The New York Times
 
Huu utaratibu wa kubambika watu kesi then mnawafutia sio haki. Kama hamna ushahidi kwann mnawaweka watu ndani. Mda ambao mtu yupo ndani angezaa watoto wangapi, angechangia uchumi kiasi gani.

Tuwe watu ambao ni civilized. Wenzetu kesi zote zina dhamana.
 
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) amewafutia mashitaka 10 ya utakatishaji fedha washtakiwa watatu kati ya watano akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu.

Mbali na Maimu washitakiwa wengine waliofutiwa mashitaka hayo ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida, George Ntalima na Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 55 likiwamo utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya amedai leo Oktoba 22 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kutajwa lakini wanakusudia kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.

Amedai kesi hiyo iko katika hatua za usikilizwaji lakini Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) amekusudia kufanya marekebisho madogo chini ya kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

"Jumla ya mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ni 55, baada ya marekebisho haya yatakuwa mashtaka 45, kwa mshtakiwa wa kwanza Dickson Maimu, mshtakiwa wa tatu, George Ntalima na wa nne Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo ambao wameondolewa mashtaka ya utakatishaji fedha," amedai Wakili Komanya.

Wakili Komanya amedai endapo hakutakuwa na pingamizi, wangeomba kuwasilisha hati mpya, hata hivyo hati hiyo haikupokelewa kutokana na Hakimu Mkazi Mkuu Rashid Chaungu anayesikiliza kesi kutokuwepo.

"Hata mkiwasilisha hati mpya, kesi hii haiko haiko mbele yangu, nawashauri muiwasilishe mbele ya Hakimu husika tarehe itakayopangwa, na kuhusu dhamana nawashauri kuwasilisha maombi Mahakama Kuu," alieleza Hakimu Shaidi.

Baada ya maelezo hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4 mwaka itakapotajwa ambapo upande wa mashtaka utawasilisha hati mpya.

Katika kesi hiyo, tayari upande wa mashitaka umeshafunga ushahidi kwa kuwaita jumla ya mashahidi 26 pamoja na kuwasilisha vielelezo 45.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Meneja Biashara wa (Nida), Aveln Momburi na Mkurugenzi wa Sheria, Sajina Raymond.

Chanzo: MWANANCHI
 
DPP anakuwa guided na nini kwenye haya maamuzi yake, au akiamua tu leo mtu atoke anatoka? - maana ofisi hii ina mamlaka makubwa mno kwa sasa kuliko enzi za awamu nyingine zote.
 
Ndio ubovu wa kutokuwa n taasisi imara na zenye meno. DPP yeye alipewa maagizo kutoka kwa ibilisi mwovu joka kuu weka ndani hao kwa visasi vyake. DPP naye hana hata muda wa kujiridhisha kama kweli kuna jinai sma la anatekeleza maagizo. Sasa tukisema hawa walikuwa wafungwa wa kisiasa mtatukatalia?
 
Tunamuomba Mungu sana mahakama itende haki kwa kumfunga Mbowe ambaye anakabiliwa na kosa la ugaidi.
 
Awamu ya 6 inapooza fujo kutengeneza transparency, go...
..
go...

Mama Mkwe wangu
 
DPP anakuwa guided na nini kwenye haya maamuzi yake, au akiamua tu leo mtu atoke anatoka? - maana ofisi hii ina mamlaka makubwa mno kwa sasa kuliko enzi za awamu nyingine zote.
Siyo kweli. Yaani DPP sasa hivi ndiyo ana mamlaka makubwa kuliko wakati wote? Mamlaka ya DPP ya jana, juzi ndiyo ya leo. Anaongozwa na sheria.
 
DICKSON arudishe Eagle akapumzike ajiandae kustaafu ametumika kama c.o.n.d.o.m na kutupwa kuleee....sasa anapambana nabhali yake.....wapi Gotham ?? Kazi ipoo
 
Kesi za kukomoa watu kijinga
Kesi za wapigaji ndio zinafutwa. Miaka mingapi vitambulisho bado watu kupewa wote kwa upigaji wa funds za vitambulisho. Halafu wapigaji wamerudishwa ulingoni wanafutiana kesi. Eti kesi za kijinga? Wakati ndio kesi za maana.
 
Wanawafutia mashtaka wengine huku wakiwapachika wengine mashtaka ya uongo, huu ni muendelezo wa upuuzi wa awamu iloyopita.
 
Naona kama ile mahakama iloanzisha ya uhujum uchumi bora ifutwe tuu wanakula kodi zetu bure
 
Back
Top Bottom