DPP Biswalo Mganga unalazimika kuwajibika kujiuzulu baada ya kumtoa "mahabusu" Nusrat Hanje gerezani akawe ghafla Mbunge

Sasa Magu ndiye kamtuma atamwondoaje?
Moja ya jukumu la Rais wa nchi ni kuhakikisha kuwa kila aliyemteua anafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria ma taratibu zilizowekwa nchini.

Kwa hiki kitendo cha DPP, Biswalo Mganga, kufanya makosa ya wazi kabisa, Rais analazimika kumtimua kazi ili aiokoe serikali yake kutokana na aibu kubwa inayopata hapa nchini na kwenye Jumuiya ya kimataifa.
 
Watu hawaheshimu Katiba sheria wala taratibu, Wanaikanyaga tu wanavopenda wenyewe. Wala hakuna sababu ya kumlaumu DPP maana anafuata maelekezo ya boss wake.
 
Hivi ubunge ungekuwa hauna pesa yoyote ungetumia nguvu kubwa kuandika haya madudu?

Mbona nyie watu mnawivu Sana?

Makelele yote haya ni kwasababu mdada wa watu kapata ubunge, hivi kama angekuwa ametolewa usiku na kuachiwa huru akaendelee na maisha yake ungekuja hapa kupiga kelele?
 
Hakuna namna nyingine. Ajiuzulu na kufunguliwa mashtaka. Ameinajisi Katiba na ametumia vibaya madaraka.
DPP Hana makosa, yeye alitumwa
Wangedanganya hata asubuhi aitwe na gati ya dharula kwenda mahakamani,mahakama ndiyo imwachie kwa kusema,upande wa mashitaka unaondoa shauri Hili mahakamani, sababu upande wa shitaka umeona hakuna sababu ya kuendelea na shauri hili,
Ilikuwa inatosha kabisa, hata sisi wanyonge tusinge jua.
 
Watu awaheshimu katiba sheria wala taratibu, Wanaikanyaga tu wanavopenda wenyewe. Wala hakuna sababu ya kumlaumu DPP mana anafuata maelekezo ya boss wake.
Lakini ni lazima ajihadhari kwa kuwa huyo Boss wake, analindwa na hiyo Katiba "mbovu" kuwa awapo madarakani na hata akitoka madarakani hakuna mahakama yoyote nchini, inayoweza kumshitaki kwa makosa yoyote aliyoyafanya alipokuwa madarakani.

Lakini yeye Biswalo Mganga halindwi na Katiba hiyo, kwa hiyo anaweza kuburuzwa mahakamani wakati wowote iwe mwakani, mwaka kesho kutwa hata miaka 20 ijayo, kwa maana makosa ya jinai hayana muda
 
Eti nawewe unasubiri uteuzi, kwa akili huzi utasubiri sana mkuu.
 
Umeongea utumbo,

Nilichosema ni kuwa yeye DPP ndiye anayepaswa kuwa mstari wa mbele kuitiii Katiba, kama yeye hataki kuitii Katiba basi anawajibika kujiuzulu Mara moja

Nyiye maccm mnachekelea sana jinsi wakubwa wenu wanaivyoisigina sigina Katiba yetu na kuwa kama "toilet paper"
 
Mkuu Mystery umeandika mengi yenye kuwakilisha hisia zako tu ili lawama ziwe za mwenye mamlaka ya uteuzi.

Yawezekana kabisa, kwa lugha iliyotumika kuwasilisha bandiko lako, wewe ni mfuasi wa upinzani. Wafuasi wa upinzani humu JF, kama viongozi wao ni kupingapinga, kulaumu na kutukana wakijifanya wajuaji kumbe upumbavu na ulofa tu.

Kwa mfano wa hilo la huyo mtuhumiwa kama kaachiwa ni kwa sheria na taratibu zote kukamilishwa. Sambamba na hilo ni uteuzi wa wabunge wa viti maalumu lawama zinahamishiwa kwa Tume ya Uchaguzi na Spika wa bunge.

Ni wakati sasa wa upinzani kujikita kujenga misingi imara ya uongozi ndani ya vyama. Malalamiko, madai na shutuma za upinzani dhidi ya Chama Tawala, Serikali na vyombo vyake, vitaendelea kuishia mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.
 
Kama mlivyomuamini mdee halafu akavunja uaminifu ndivyo mnyika anavyojaribu kukwepa msala lakini yeye na mbowe wanajua mpango wote Halima sio kichaa tu wa kumshukuru Mbowe!
 
Hakuna sheria yoyote imevunjwa
Yule sio mfungwa ni mahabusu tu

Mbona bavicha walikuwa wanampelekea cheq na documents za kusaini akiwa jela je wao walikuwa wanatumia sheria gani?

Mtu akiwa jela anaweza kufanya kazi za office? Mbona hamkulalamika?
 
Kwa namna mambo yanavyokwenda kwa zaidi ya miaka minne, ni dhahiri hili Rais Magufuli hawezi kulifanya.
 
Tanzania has turned into chamber of monsters, gangsters and mobsters who killing and violating national principles for the sake of personal gains.

Biswalo is a looter, must go out of the office.
 
Hakuna kiongozi wa chadema aliyewaita hivo bali ni watu wa kawaida. Inawezekana wakawa hata kutoka CCM au hawana chama.
 
Hakuna kiongozi wa chadema aliyewaita hivo bali ni watu wa kawaida. Inawezekana wakawa hata kutoka CCM au hawana chama.
Haaaaa haaaaaaa. Musihamishe magoliii, muliwaandalia mabango yenye kuwaita wao ni covid 19 huku mkiwa mumevalia sare zenu nyekundu na kuzagaa makao makuuu yenu hapo ufipa. Mumeanza kutesekaa na kauli zenu za kukurupuka. Msibadilishe gia anganiiiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…