Nafasi za DPP, CAG, Gavan Benki Kuu, Mkurugenzi TISS, AG, Waziri wa Fedha, na nyingine zinazofanana na hizo zinastahili kushikiliwa na watu wenye umri above 60, umri ni factor muhimu sana kwa binadamu kuweza kufahamu namna anavyopaswa kuwa mbele ya jamii, muhimu ni ile hali ya kuwa juu ya mambo yanayokwaza watu wengi hasa vijana..kiburi, anasa, ujeuri, tamaa, dharau nk mtu mwenye umri mkubwa wengi huwa wamevuka hali hizi..tatizo tulilo nalo ni wanaofanya vetting (TISS) wanataka kupata watu wanaoweza kuwaingilia kwenye majukumu yao na hasa vijana vijana, ni vigumu sana kumuingilia mtu mzima ili afanye kinyume na anavyopaswa kufanya! si kazi zote sifa ni elimu..Nooooo! AGE ni factor muhimu sana..kwa vile vitabu vya imani ni rejea nzuri na ya uhakika ili tujifunze soma kisa hiki kutoka kitabu cha 1 WAFALME 12: 3-18 utaona tofauti ya kuwa na vijana au wazee kwenye majukumu ya kutoa MAAMUZI!