DPW ni adui wa kanisa na mafisadi na wafanyabiashara

Mambo ya DP World hayajaisha tuu? Je Gati anazosimamia DP World ndio Kanisa linapotishiaga mambo yake? 8-11
 
Mambo ya DP World hayajaisha tuu? Je Gati anazosimamia DP World ndio Kanisa linapotishiaga mambo yake? 8-11

Choice

Ahsante sana kwa suala lako

Lakini hiyo ilikuwa ni tathmini yangu tu. Si unajuwa kila baada vumbi fulani huwa kunafanywa tathimini. Kwahivyo ulosoma kutoka kwanu haikuwa zaidi ya kipomo cha vumbi lilozushwa katika akili za watu baada ya kupewa DPW fursa ya kuiokoa bandari ya Dar.
 
kwani serikali na idara zake zina milikiwa na kanisa ?.
aisee wanzanzzibari ndio maana mkapa aliwatandika sana mshukuru mkafika UK
 
Waache waje tu.
Wenye nchi tupo
Wakileta ujinga kama watwana wao tutawapindua.
Hiyo mikataba Yao ya Siri tutaipitia upwa wakati wetu.

Vijana wa kazi tupo msiwe na shaka.
Hapa Udini hautakiwa kabisa

Mama Tanganyika ni yetu sote. Wa Dini zote.
 
Huo ndio ukweli ndio maana kuna Professor mmoja wa kike alikuwa kila siku anakuja na poroja ila anatetea kanisa lake.

Meli zimeongezeka kwa kasi na mapato yataonekana.
 
Kanisa wanabiashara gani! zinazohusisha Bandari? Na kanisa peke yake ndio taasisi ya Kijamii inayopata Ruzuku?
 
Ndugu Mzanzibar Huru labda kidogo tufahamishane vizuri maana ulichoandika hapa juu kina maswali ya kujiuliza mengi
Moja ingekuwa vizuri ukalitaja hilo kanisa ambalo wewe unasema linapata mgao wake maana navyojua kila kanisa lina taratibu zake katika kupata mapato yake na huwa hayategemei serikali katika kujiendesha au kutoa huduma zao za kikanisa. Ndiyo maana ukienda makanisani utakuta kuna michango mbali mbali ambapo waumini wanachangishwa mbali na sadaka.Lakini pia kuna baadhi ya makanisa yanapata misaada toka nje ya nchi.

Pili tukirudi upande wa bandari ni kweli ndiyo lango kuu la mizigo kuingia nchini bidhaa ila hapa tuelewe kuwa kodi inayokusanywa ndiyo hii inayoenda kuendesha Serikali na yale yote ambayo imepanga kuyafanya atika mwaka husika ikiwa pamoja na kulipa madeni ambayo inadaiwa.

Kodi navyojua inatokana pia na mapato ya ndani ikiwa pamoja na wafanyabiashara wa ndani kulipa kama vile kodi ya mapato,VAT n.k. Kuna viwanda vingi nchini ukitembelea Mkoa wa Pwani ambapo serikali inapata fedha nyingi kupitia viwanda hivi maana pia kuna kodi ya mshahara.

Mbali na hii tukumbuke Mh Raisi alikuwa mstari wa mbele kuhsamasisha utalii na hii sekta pia inachangia pato kubwa sana kwenye kodi kwa sababu watalii wanapokuja kuanzia visa fee, airport tax, kukodisha magari ya utalii, hoteli kote huko kunaingiza fedha kwa kuwepo kwa watalii hawa.

Tusisahau pia kuna mipaka ambapo mizigo toka nje inaingia mbali na bandarini mfano uwanja wa ndege wa KIA ,Zanzibar na Dar napo kunaingia mizigo na maeneo kama Namanga,Tunduma, Sirali,Tarakea,Holili,Horohoro,Mtambaswala,Tarakea, Kabanga,Kasumulu,Mtukula,Bandari ya Kigoma,Bandari ya Tanga, Bandari ya Mtwaara, Bandari ya Mbamba bay, kote huku nako mizigo inapita.

Labda nikuombe kamanda lete jina la kanisa tuweze jifunza zaidi na kujua nini kulikoni ila mapaka sasa hiki ndicho nachokifahamu kwa upande wangu na kuwa serikali inakusanya kodi pitia TRA na zinaingia moja kwa moja BOT ambapo kwa kupitia Bunge mgawanyo wa pesa huo unapitishwa kwa ajili ya maendelea na ujenzi wa nchi ikiwa pamoja na kulipa madeni na mishahara ya watumishi wa umma.
 
Hii kali yaani mamlaka ya mapato Tanzania inakusanya kodi kwa ajili ya Kanisa? hahahaa da ama kweli hii kali ya mwaka maana tra wapo wakristo tu wanafanya azi hiyo tena forodha kuna wakristo wote hahahaaaa da nchi hii inavituko. Unatoa wapi mawazo haya ndugu? Makanisa yanafanya biashara gani? Yapewe mgao gani kwani wamewekeza nini? hata kama wangekuwa wamewekeza je kuwekeza ndiyo wapewe mgao maana tra kazi yao kukusanya kodi. ushasikia tra wanatoa hisa? sasa iweje useme leo eti kanisa wanapata mgao toka tra. tra viongozi wake ukiulizia wapo mchanganyiko waislamu na wakristo sasa iweje useme eti wanasimamia kanisa kweli?
 
Aise!!
 
Kwa uelewa wangu mdogo wakati nasota kutafuta maisha niliwahi pitia pitia nyaraka mbali mbali za tra sababu nilikuwa napenda sana kujifunza sababu chuoni Arusha tulikuwa tunasoma pia na Business laws na taxi .Labda nami nichangie kulingana na maoni yangu

Misamaha ya kodi ni jambo la kisheria na sio maono au matakwa ya mtu binafsi au kundi la watu wa aina fulani, laa hasha bali kila msahama wa kodi unatoka katika tamko rasmi la sheria ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo na katika hili naomba nikupe mifano kadhaa ya sheria inayotoa misamaha ya kodi na sababu ni takwa la kisheria mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kama msimamizi wa masuala ya kodi nchini Tanzania hana budi kusimamia utekelezaji wa sheria kama ipasavyo kikamilifu.

1. Katika masuala ya kilimo (misamaha ya kodi hutolewa katika uingizaji wa vifaa vya kilimo),

2. katika sekta ya tiba na afya (misamaha ya kodi hutolewa katika uingizaji wa dawa na vifaa tiba),

3. katika kuendeleza biashara na uwekezaji (msamaha wa kodi huwekwa katika maeneo husika la utengenezaji wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi),

4. katika kudumisha ustawi wa jamii (serikali hutoa misamaha ya kodi katika taasisi zote za kidini zilizosajiliwa nchini, mashirika yote ya hisani yaliyo sajiliwa nchini na mashirika yasiyo ya serikali yaliyosajiliwa nchini)

5. katika kudumisha mahusiano na ushirikiano wa kimataifa (serikali hutoa misamaha ya kodi kwa balozi zote zenye hati thabiti za utambulisho, mabalozi wote duniani watakao tembelea nchi yetu ya Tanzania, taasisi zote za kimataifa zenye hadhi ya kidiplomasia inayotambulika kisheria)

6. katika shughuli wa uchimbaji wa madini, serikali pia hutoa misamaha ya kodi mfano Matumizi yote yaliyotumika kwa mwaka (matumizi ya mtaji na mapato) hukatwa wakati wa kukokotoa mapato yanayotozwa kodi.

7. Katika masuala ya elimu na kuhakikisha taasisi za elimu zinaajiri wafanyakazi wa kutosha na kutoka huduma bora serikali imeweka msamaha wa kodi wazi wazi na bure kabisa kwenye ushuru wa kukuza ujuzi katika shule za awali, shule za msingi, shule za sekondari; shule za ufundi, elimu na mafunzo; vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu; na taasisi za afya za kidini.

Kwa ufupi mifano ni mingi sana lakini naomba ufahamu kila msamaha wa kodi ambao mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inausimamia na kutekeleza, TAMBUA KUWA YOTE INATOLEWA KISHERIA kwa mujibu wa vipengele husika vya sheria husika kulingana na msamaha wenyewe na mlengwa wa huo msamaha.
 
Mungu chukua kiumbe chako hiki ,maana hakina faida
 
Nilitaka kushangaa Kanisa linapewaje pesa na tra wakati TRA ipo kwa ajili ya serekali ili kuendesha nchi? kumbe taratibu ni misamaha ambayo ipo kisheria.Sasa DPW itazuiaje wakati tra bado watakuwa na jukumu la kukusanya? vingine watu tuwe tunafanya tafiti siyo majungu yasiyo na uthibitisho.Eti kanisa linatoka kivipi? hii kali nimesoma nashukuru mdau umetupatia mwanga na uelewa data kama hizi zinaweka uzi vizuri kwa kuweka facts
 
Mungu chukua kiumbe chako hiki ,maana hakina faida
Kabisa. Kuna mijitu inapenda sana kuona kuna machafuko yanatokea.Jitu linaleta ukabila mara udini kwa kuleta vitu vya kufikirika. Sasa ukisoma unashangaa mara wakristu huku anajiita Mzanzibar Huru kama siyo kuleta uchonganishi kwa makusudi na kuihusisha taasisi ya serekali inayotegemewa kukusanya mapato. Mijitu kama hii ni kuikamata na kuichapa fimbo kisha sweka ndani. Wakristo wamekosa nini? Kwani karamagi alipokuwa TICTS waislamu walipita bure na wakristo walibanwa? Tuache ujinga na kutaka kuona nchi inavurugika wengine familia zetu zimeingiliana dini mpaka makabila.Pumba kama hizi tusingependa kuzisikia sababu hakuna ukweli wowote eti maoni yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…