pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,422
- 6,108
Rostam kaomba radhi huko, umesikia?Uchizi kamili.
Unajiachia wazi na kuonyesha hali yako halisi.
Usifikiri unaweza kunivuta kwenye kujadili ukichaa wako. Sina muda wa kupoteza na watu wa aina yako.
Mkataba ulisainiwa na Wazanzibari wawili kwa niaba ya watu milioni 60 wa nchi ya Tanganyika! Tena inawezekana ni baada ya kurubuniwa na hapo DP World!DP wanahusikaje na mkataba mmesaini tayari bila kushurutishwa? vigezo na Masharti vilikuwemo ndani ya mkataba, nyie mkakimbilia kuweka saini tu bila kusoma. Kosa la nani? Next time (mikataba mipya/mwingine) kuweni makini kabla ya kusaini
**Kuna mengi ya kujifunza katika hili, tuache kushupaza makomwe kwenye kichaka cha 'uzalendo'
Hakuna kilichouzwa, upotoshaji huanzia hapa. Kasome kifungu cha expopriation 14 kifungu kidogo namba 2.Hauna ukomo na umehusisha bandari zote za kwenye bahari na maziwa, special economic zones na anga la nchi. Kimsingi tumeuza nchi nzima.
Hao wazanzibari sio watanzania?. Ubaguzi unaanzia kwenye mada kama hii.Mkataba ulisainiwa na Wazanzibari wawili kwa niaba ya watu milioni 60 wa nchi ya Tanganyika! Tena inawezekana ni baada ya kurubuniwa na hapo DP World!
Sasa unaposema "nyie", "kuweni", nk! Huoni kama hututendei haki! Tunahusika vipi na huo mkataba?
Mkataba una umangungo upi?
Utakapouona mkataba mahali soma kifungu hicho. Hawa wazee kina Shivji na Warioba wameamua kwa makusudi kusimamia vifungu wanavyojua wakiviweka wazi hadharani wataendelea kulinda heshima yao.Sasa hicho kifungu si ukilete hapa au unapenda kuongea bila ushahidi?
Una uhakika raia wa huko wanajitambulisha kama Watanzania?Hao wazanzibari sio watanzania?. Ubaguzi unaanzia kwenye mada kama hii.
Mkataba upo na kifungu kipo, mimi sina mkataba hapa lakini najua kuwa kifungu namba 14 sehemu namba 2 kumeelezewa juu ya utaifishaji.Sasa hicho kifungu si ukilete hapa au unapenda kuongea bila ushahidi?
Mkuu nimekuomba ulete vifungu bado unabisha? Hebu nukuu hivyo vifungu unavyoona vina manufaa uviweke hapa. Na pia hivyo vifungu wanavyotumia Warioba na Shivji kama unaona havina maana yoyote vilete hapa tuvichambue. Kama huna hoja ukae kimya.Mkataba upo na kifungu kipo, mimi sina mkataba hapa lakini najua kuwa kifungu namba 14 sehemu namba 2 kumeelezewa juu ya utaifishaji.
Tunayo hulka ya kuchagua baadhi ya vifungu ambavyo tunadhani vinatupa hoja za kuupinga uwekezaji mzima wa DPW kumbe vipo vingine vyenye kuelezea tunatoka vipi kwenye matatizo hayo hayo.
Inasikitisha kuona wazee wa hadhi ya Shivji na Warioba wakinasa kwenye mitego hii hii inayowanasa watanzania wengi wa mitandaoni.