DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

Your browser is not able to display this video.
 
Your browser is not able to display this video.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa taharuki ilojitokeza ilipaswa kuwepo na mtu au watu wa kujiuzuru voluntarily baada ya kujitathmini.

Lakini wapo tu wamekomaa duuh.

Bongo bana!
 
MKATABA WA DUBAI, TANZANIA NA VIUMBE WALIOLAANIWA

(Re-edited) Na Joseph Mihangwa

“Wakajazwa kasumba za kitabaka kwa utamaduni wa kigeni wasioujua; wakapewa maneno yasiyo mantiki, nayo yakawajaa vinywani, wakawa kama Kasuku mbele ya ndugu zao; wakang’olewa mizizi ya asili yao, wakapoteza utu na uzalendo; ubinafsi ukawajaa, utosini hadi unyayoni. Wakaghairi uhusiano na umma wa nchi zao; wakawa Mamluki kwa vitendo kugeuza nchi zao danguro la wageni”
(Franz Fanon, katika kitabu The Wretched of The Earth/Viumbe Waliolaaniwa)

SAKATA la Mkataba kati ya Ufalme wa Dubai na Serikali ya Tanzania kuhusu uwekezaji katika Bandari nchini, limezua mtafaruku wa Kisiasa, Kijamii na Kikatiba likichagizwa na maelezo hafifu yasiyotosheleza, ya Serikali na Bunge, mara nyingi kwa kujikanganya kuashiria kwamba, ama taasisi hizi mbili haziyaelewi vyema maudhui ya Mkataba huu, tafsiri ya yaliyomo na athari zake kwa nchi; au zinayajua lakini zinajaribu kuficha ukweli kutaka kufunga goli la mkono kwa maslahi binafsi na ya kivikundi dhidi ya maslahi mapana ya nchi na wananchi. Ili iweje?

Serikali na Bunge wanadai kuwa, Bunge limepitisha Azimio la kuthibitisha/kuridhia Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kuhusu Bandari na uwekezaji, na kwamba hakuna Mkataba wowote uliotiwa saini, kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World (DPW) ya Dubai. Wanataka kuuaminisha Umma kwamba Mkataba wa Kiserikali (Intergovernmental Agreement) IGA uliotiwa saini na wakuu wa Serikali mbili hizi Mjini Dodoma, Oktoba 25,2022 kwa kuwakilishwa na wateule wao, si Mkataba bali ni Azimio la Serikali hizo, sawa tu na Kumbukumbu ya Maelewano (MoU), na kwamba Mkataba husika utafikiwa baadaye kati ya PDW na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na “Mikataba” mingine ya kiutekelezaji(HGAs).

Kwa kujua au kwa kutokujua na sababu zake, Serikali na Bunge wanashindwa kutofautisha kati ya Mkataba na MoU (isiyo na nguvu ya kisheria) iliyofikiwa na DPW na TPA Mjini Dubai, Februari 27, 2022 wakati wa ziara ya Rais wetu nchini humo.

”Mkataba” ni Makubaliano kati ya pande mbili za maelewano, yanayokusudiwa kuwa na nguvu ya Kisheria kuweza kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria. Si kila Makubaliano ni Mkataba kama wanayoyaingia hawakusudii yawe na nguvu kuwabana kisheria.

Kati ya vitatu vinavyotajwa katika sakata hili, yaani MoU, IGA na HGA, Mkataba ni ule wa IGA ambao chini ya ibara yake ya pili unaweka msingi wenye nguvu ya utekelezaji na uwajibikaji Kisheria kwa washirika wake kwa maeneo husika ambayo ni, Ushirikiano juu ya Kuendeleza, Kuboresha, Kusimamia, Kutawala, Kudhibiti na Kuendesha Bandari za Bahari,Maziwa na Maeneo Maalumu Huru ya Kiuchumi (sio kwa bandari tu), Maegesho na Uchukuzi, Vishoroba(corridors) vya biashara na Miundombinu mingine ya kimkakati kuhusiana na Bandari nchini Tanzania.

Ni kwa vipi Mkataba huu(IGA) utapata nguvu ya Kisheria, imefafanuliwa vyema kwenye ibara ya 25(2) kwamba, itabidi uridhiwe na Bunge kwa kutungiwa Sheria ya Utekelezaji (ibara 26,27) kwa kuzingatia matakwa ya sheria za Kimataifa na ibara ya 63(c), (d) na (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo Bunge letu tayari limekwishatekeleza hapo June 10, 2023.

Kwa mantiki hiyo, si kweli kwamba Serikali yetu haijaingia Mkataba na Dubai. Hati iliyotiwa saini na nchi mbili hizi Mjini Dodoma tahehe 25 Oktoba 2022, ni Mkataba kamili kama tutakavyoona hivi punde katika andiko hili. DPW na TPA kwa upande wao, ni watekelezaji tu wateuli wa Miradi husika chini yan na kwa nguvu za Mkataba huo. Ni kwa nini Serikali inajaribu kuuficha Umma kwa nguvu kubwa isiyo ya kawaida kwa propaganda za Kisiasa na kwa kutumia vikundi vya kitabaka na wakati mwingine vya kidini ni jambo linalofikirisha.

Ukweli ni kwamba, Mkataba huu na yaliyomo katika hati bishaniwa ni suala la Kisheria zaidi kuliko mengine yote hivi kwamba ni Wanasheria wanataaluma wa Sheria za Mikataba, Sheria za Kikatiba na za Kiutawala(Contract Law, Constitutional and Administrative Law) pekee ndio wanaoweza kuchambua na kutoa majibu sahihi yenye kumaliza Mtanziko.

“Uchawa” pofu, potofu, angamizi na wa kimbumbumbu, Siasa za Kihemshaji na uropokaji hauna nia mjema, wala hautoi nuru kwa Taifa letu lenye kiu ya ukweli, hekima na busara kutawala, badala ya kutia giza nchi kwa maslahi binafsi kutugeuza Viumbe Waliolaaniwa. Tutaona katika andiko hili jinsi Mkataba huu ulivyo mtego kwetu kutaka tujikwae kisiasa, kiuchumi na kijamii tuuze uhuru wetu.

Tutamke mapema hapa kwamba katika hili, uwezekano wa TPA kuuza Bandari kwa DWP kwa sababu ya au kupitia HGA mbovu haupo kwa sababu Bandari ni mali ya Serikali ambaye ni mshirika wa IGA hii. Kama ni hivyo, basi, itakuwa ni Serikali yenyewe kwa njia ya IGA. Na hilo si geni katika historia ya Ukoloni na Ubeberu wa Kimataifa Barani Afrika, kwa Mikataba mibovu kuuza Nchi au kupora rasilimali za Taifa.

Ni kwa mantiki ya usemi wa Kikoloni na Ubeberu wa Kimataifa Karne mbili zilizopita kwamba, “Trade follows Flag”. Maana yake kwamba baada ya Biashara hufuata Utawala (Nchi ya Kikoloni) kunyakua na kutawala nchi.

Historia ya Ukoloni Barani Afrika inaonyesha yote hayo, kwamba Wamisionari ndio walikuwa wageni wa kwanza kufika kueneza Dini ya kigeni (Ukristo) kama wapelelezi pia wan chi zilizowatuma. Wakafuatia wafanyabiashara baada ya kuhakikishiwa na Wamisionari hao kwamba hali ilikuwa shwari kwa nguvu ya Injili na Uinjilishaji uliofanywa kutuliza hali (pacification) na Wamisionari hao.

Wafanyabiashara kwa kiu ya utajiri na kutaka kupora rasilimali za nchi, kwa kulindwa Kijeshi na Serikali za nchi zao wakaingia kuchakaza na kutumikisha wenyeji na hatimaye nchi Mama zilizowatuma kunyakua nchi zetu na kuzifanya Makoloni.

Waliosaidia mchakato huo nchini kwa Wamisionari na Wafanyabiashara kuingia jikoni, kisha Ukoloni, ni vijana wa Kiafrika waliojiona bora mbele ya ndugu zao kama waumini wazuri wa dini na utamaduni mpya, waliogeuka Kasuku kwa ndugu zao, Wakalimani wakihubiri sifa za utamaduni mpya na Ukoloni anavyoeleza Franz Fanon hapo juu.

Katika historia kujirudia, leo, Kasuku wa zama zetu ni watu wetu waliojing’oa mizizi kuwa mamluki wa Ubeberu wa Kimataifa kustahili kuitwa “Makuwadi wa Soko huria na Utandawazi”

Novemba, 1884, huku Afrika Mashariki, Chifu Mangungo wa Msovelo, aliuza nchi yake kwa Carl Peters wa Shirika la Society for Germany Colonization(SGC) lililoanzishwa Mwaka huo nchini Ujerumani mahsusi kuitafutia Ujerumani Makoloni popote Duniani, kwa kusaini kichwa kichwa bila kuelewa, Mkataba wa kimagumashi usio na muda wala kikomo kumpa Peters haki zote za Kiuchumi na Kijamii nchini mwake.

Februari 1895, Carl Peters akaunda Kampuni ya Germany East African Company(GEAC) na kuhamishia kwa kurithisha haki zote za Mkataba kwa Kampuni hiyo ambayo hapo hapo ikapatiwa na Mtawala wa Ujerumani hadhi ya Kampuni ya Serikali ya nchi hiyo na kupewa ulinzi wa Kiserikali.

Mkataba huu uliohusu eneo lote la Usagara, Uzigua, Nguru, Ukami na maeneo mengine, ndio uliotumiwa na Ujerumani kudai haki ya kupewa Tanganyika kuwa Koloni lake kwenye Mkutano wa Berlin wa Mataifa ya Ulaya, ulioketi huko kuigawana Afrika Mwaka 1884/85 kwa sababu tu ilikuwa na ridhaa ya Machifu wa maeneo husika. Tanganyika, kabla ya kuitwa hivyo, ikapewa jina Deustch Ostafrika, yaani Afrika Mashariki ya Kidachi.

Mwaka 1888, huko Afrika Kusini, Mfalme wa nchi ya Ndebele na Shona, (sasa Zimbabwe), Lobengula, alitia saini Mikataba miwili na Wazungu – The Moffat Treaty (MT) na The Rudd Concession (RC) bila kuelewa Maudhui wala mantiki yake, Mikataba iliyotoa haki ya kumiliki ardhi na madini kwa Mfanyabiashara Mzungu wa Kampuni ya British South African Company (BSAC), Cecil Rhodes, iliyomwezesha kutambuliwa, na Mikataba hiyo kuhesabiwa kama Mikataba ya Serikali ya Uingereza na kupewa ulinzi.

Ni kupitia Mikataba hiyo Uingereza ilinyakua Ufalme wa Lobengula na kutawala kama nchi iliyopewa jina “Rhodesia”, ambayo sasa ni Zimbabwe.

Ni kwa sababu kama hizo kwamba, leo tunaposikia Mikataba kati ya nchi na nchi (IGA) ikitiwa saini tofauti na Mikataba ya kawaida ya kibiashara na kiuwekezaji, tena kwa kificho na ghiliba, nywele husisimka kwa hofu ya historia kujirudia zama hizi za Ukoloni mpya kwa Sera za Soko huria na Utandawazi. Na ndivyo ilivyo kwa Sakata hili la Mkataba kati ya Dubai na nchi yetu ambalo limezua bila sababu, hisia za Kidini(Umisionari), Kibiashara(Uporaji rasilimali) na Kiutawala(Ubeberu wa Kimataifa) pia.



Dubai si nchi



Hakuna ubishi kwamba Tanzania na Ufalme wa Dubai zimesaini Mkataba wa Kiserikali kuhusu Ubia/Ushirikiano kama tulivyoona mwanzo. Lakini ukweli, kwa yaliyomo, huu ni Mkataba tofauti na Mikataba mingine ya Uwekezaji, tofauti pia na yaliyomo na unavyosomeka.



Dubai si nchi bali ni mji wa kibiashara na ni Ufalme pia wa kinasaba katika Shirikisho la Falme saba za Kiarabu (UAE) ambapo UAE ndiyo nchi. Shirikisho hilo liliundwa Desemba 2, 1971 ambapo chini ya Katiba ya Shirikisho, Mtawala wa Dubai anakuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa kudumu, na Mtawala wa Abu Dhabi hubeba nafasi ya Ras na Mkuu wa Nchi wa kudumu pia.

Falme zingine zinazounda UAE pamoja na Dubai, ni Abu Dhabi, Sharjah, Ras Al Khaimah, Ajman, Umm Al Quwain na Fujairah. Chini ya Katiba ya Shirikisho ambamo Dubai na falme hizo ni kama Mkoa, Jimbo au Serikali ya Mtaa, dola na nchi inayotambuliwa Kimataifa na yenye uwezo wa kuingia Mikataba ya Kimataifa kama huu unaozungumziwa, si Dubai bali ni UAE.

Kwenye Mkataba huu, Rais wetu alitia saini kwa kukasimu madaraka kamili kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, kwa Hati ya kukasimu ya Oktoba 3, 2022, na Mkataba kushuhudiwa kwa kutiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye hata hivyo hakuweka jina, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Mkataba huo (na Kisheria pia) kwa kuandika jina lake baada ya saini yake na kuzua maswali mengi. Na ndivyo ilivyokuwa kwa shahidi aliyeshuhudia Mkataba huo upande wa Dubai

Upande wa Mshirika wa pili, yaani, Ufalme wa Dubai, ametia saini Mtendaji Mkuu(CEO) wa Shirika la Bandari na Forodha na Maeneo huru (PCFC) la Dubai, Shekh Ahmed Mahboob Musabih, kwa kuteuliwa kwa barua Kumb. No HHRC/OUT/2022.0003846 ya tarehe 18/10/2022 na Mamlaka ya uteuzi ya Dubai yasiyoeleweka, tofauti na alivyokasimu Madaraka Rais Samia.

Yaelekea Mkataba huu ulitiwa saini chini ya mazingira ya kidharura bila msaada wa Wanasheria. Hilo linathibitishwa na ukweli kwamba, na kama inavyoonekana kwenye Hati, Mheshimiwa Mbarawa alianza kuweka saini yake kwa makosa sehemu ya Katiba Mkuu wa Wizara; akasituka, akaacha kwa kakomea njiani. Saini ya Katibu Mkuu imeanzia mahali Mbarawa alipojaribu kutia saini. Wangekuwepo Washauri wa Kisheria, Mashuhuda hao wasingeacha kuweka majina yao.

Tunataja mapungufu haya yaliopo juu ya uso wa Hati ya Mkataba huu kujenga hoja kwamba una mapungufu ya Kisheria kwa kutiwa saini isivyotakiwa (Irregulary signed), na hivyo batili kwa kiwango hicho.

Ukiacha kasoro tulizoona hapo juu, kufikia hapo, hapana shaka kwamba Mkataba huu (IGA) uliotiwa saini Oktoba 25,2022, ni wa Kimataifa kwa Sheria za Kimataifa, wenye kuendana na Maafikiano ya Kimataifa. Ni aina ya Mkataba (Intergovernmental Agreement) – IGA ambao chini ya Mfumo wa Sheria za Uingereza ambazo watekelezaji wake wameazimia kuzitumia na kuzifuata kutekeleza yaliyomo (Tazama ibara ya 21), Wakuu wa Nchi wana hiari, uwezo na Mamlaka ya kuingia Mikataba kwa niaba ya nchi zao.

Ni mfumo wa Kikatiba unaotumika kwa nchi zote za Jumuiya ya Madola. Hata hivyo, utafiti umeonesha kuwa hakuna mahali pengine Duniani ambako DPW imewekaza, imetumia au kutaka kutumia utaratibu wa IGA na HGA isipokuwa kwa Tanzania tu.

Mkataba huo ulitanguliwa na kitendo cha kutiwa saini Hati ya Maelewano(MoU) Mjini Dubai, tarehe 27 Februari 2022, kati ya TPA kwa kuwakilishwa na Mtendaji Mkuu wake wakati huo, Erick Hamis, na Kampuni la DP World ya Dubai, iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake, Sultan Ahmed Bin Sulayem, na yote kushuhudiwa kwa macho na Rais wetu, Mheshimiwa, Dakta. Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani nchini humo.

Kwa mujbu wa Gazeti la Serikali la kila siku la hapa nchini, The Daily News, la April 26, 2022, MoU hiyo ilihusu pia Mtaji wa uwekezaji wa dola za Kimarekani Milioni 500 kwa DPW, ambacho ni kiwango cha chini anazotakiwa kuwekeza Mwekezaji wa Kigeni kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji ya wakati huo ya Mwaka 1997.

Ukakasi katika Mkataba

Swali linalopaswa kujibiwa hapa kabla ya yote ni hili: Mkataba unazungumzia “Nchi Washirika” (State Parties) kuwa ndio wahusika (angalia sehemu ya Utangulizi na Ibara ya 1(a) kuhusu tafsiri). Na kwa kuwa Dubai sio Nchi bali ni Ufalme au jimbo tu ndani ya Shirikisho la UAE; Je, Dubai, achilia mbali Shirika la PCFC lililotia saini Mkataba na Serikali yetu, wana uwezo au uhalali gani wa kuingia au kutia saini Mkataba wa Kimataifa (IGA) kama huu walivyofanya chini ya Sheria za Uingereza na Sheria za Kimataifa walizoapa kufuata?. Jibu tunalopata haraka haraka hapa, kwa mujibu wa Sheria za Mikataba, ni kuwa “hawana uwezo wala uhalali huo” kwa kupungukiwa hadhi na sifa za kufanya hivyo.

Sasa tunaanza kupata majibu ni kwa nini Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wanaanza kuogopa na kukimbia vivuli vyao kwa kudai kuwa Bunge halijapitisha wala kuridhia Mkataba wa Dubai/Tz; na zaidi kwamba, Dubai/Tz hazijaingia Mkataba kama huo isipokuwa Maelewano tu ya Kusudio (MoU), wakati si kweli.

Tena, tunaelezwa kuwa, Mkataba utaingiwa kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DPW ya Dubai. Maana yake wanaukana Mkataba wa IGA kwa utata wake, na kwamba Mkataba halisi na tarajiwa utakuwa ule wa Serikali Mwenyeji(HGA) na Kampuni za Mradi za DPW, utakaoundwa na kuingiwa chini ya, na kwa mujibu wa ibara ya 1(a), 1(b)(v), 2(a),(b),(c) na 25(3) za IGA.Tunasahau kwamba, bila IGA, HGAs haziwezi kuwepo, wala haziwezi kuundwa, lakini si kinyume chake.

Tena IGA inasema, mara tu baada ya kutiwa saini, shughuli za awali zilizotajwa katika Ibara ya Kwanza na ya Pili zitaanza kutekelezwa kabla hata Mkataba haujaridhiwa wala HGA kuingiwa. Ni kusema kwamba, kuanzia Mkataba ulipotiwa saini, Oktoba 25,2022, DPW wana uwezo na mamlaka kamili ya kuingia jikoni kutekeleza kazi kwa viwango husika chini ya Ibara hizo, ukiwamo ujenzi wa barabara toka barabara kuu kwenda Bandarini na Miundombinu mingine, na Mamlaka kamili ya kubomoa Miundombinu, iliyopo, bila kubagua Majengo na Makazi ya Wananchi.

Tuache hilo. Takwa la Mikataba ya kati ya nchi na nchi (IGA) kuridhiwa kwa kutungiwa Sheria ya Bunge ni Msimamo wa Kisheria uliowekwa na Jaji Lord Atkin, Mwaka 1937, katika Shauri la Mwanasheria Mkuu wa Canada Dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Ontario (1937) AC 326 pg 347), na sisi tumeridhia kama ilivyo katika Ibara 63(d) na (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977.

Katika hili, Mikataba midogo ya kiutekelezaji (HGA) itakayowekwa kwa nguvu ya IGA itakuwa Sheria juu ya Sheria zingine nchini na Sheria za Kimataifa kiwango cha matakwa ya Mkataba huu. Wala Mahakama za hapa nchini, ikiwamo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, hazitakuwa na uwezo wala Mamlaka ya kusikiliza, kuamua au kubatilisha IGA baada ya kutungiwa Sheria ya Utekelezaji na Bunge. Ni kwa sababu hiyo Mkataba umeweka Migogoro kusikilizwa na kutatuliwa nchini Afrika Kusini na Mahakama ya usuluhishi ya Kimataifa.

Tunayo mifano mingi ya Sheria za Utekelezaji (Implimentation Laws) chini ya Mikataba (Treaties), ya Kimataifa Mmoja wa Mikataba hiyo ni ule wa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar wa Aprili 22, 1964, maarufu kama “Articles of Union”, na Sheria yake ya Utekelezaji, maarufu kama “Acts of Union”, Na. 22 ya 1964.

Kwa Mukhtadha huo, Mgogoro wowote juu ya Muungano hauwezi kusikilizwa na kuamliwa kwenye Mahakama za kawaida hapa nchini, bali kupitia Mahakama Maalumu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo kazi yake pekee ni kutoa Uamuzi wa Usuluhishi juu ya suala lolote la Muungano kama Tafsiri au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sheria zingine za Utekelezaji zilizopata kutungwa na Bunge letu ni pamoja na zile kuhusu Mkataba wa Huduma za pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki (East African Common Service Organisation) – EACSO (Implimentation Ordinance) ya Mwaka 1961; Sheria ya Utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki(EAC) ya Mwaka 1967, na Mkataba wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania – Zambia (TAZARA) ya Mwaka 1968, na sasa tunasubiri Sheria ya Utekelezaji wa IGA juu ya Ubia wa Kiuchumi, Kijamii, na Uwekezaji Bandarini ya Mwaka 2023 unavyotaka Mkataba huu, kwa kutaja Sheria chache tu.

Watunzi na watia Saini wa Mkataba huu na wengine wote walio nyuma yake wanajua yote haya na maeneo yapi tunataka kukwidwa. Na kwa kuwa Bunge limeyavulia maji nguo, huku likipima ghadhabu ya Umma kwa kumangamanga, lazima liyaoge au lifute Ridhio lake na Sheria ya Utekelezaji(kama limetunga) na Mchakato uanze upya, bila hivyo Mkataba huu haukwepeki. Tumejitia kitanzi wenyewe.

Kipi Bunge limeridhia, MoU au IGA?

Si sahihi kudai kwamba Bunge limeridhia Mapendekezo (MoU) ya Ushirikiano/Ubia wa Kiweukezaji, kati ya TPA na DPW juu ya kuendeleza na Kusimamia Bandari zetu, au kwamba Mazungumzo yanaendelea ili hatimaye Mkataba uweze kuandikwa. Maana yake ni kusema kwamba Bunge limeridhia MoU kati ya TPA na DPW, ulitiwa sahihi Dubai, 27/2/2022 Kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiahirisha Mkutano wa Bunge la 12, Juni 2023, kwamba maoni ya Wananchi yaliyokuwa yakiendelea kutolewa yatazingatiwa wakati wa kuandaa Mkataba (HGAs) yanaonesha mtizamo huo.

Si kazi ya Bunge kuridhia MoUs, Mikataba au Makubaliano yoyote yasiyoingiwa na Wakuu wa nchi, achilia mbali Mikataba ya kawaida ya Kibiashara na Uwekezaji kati ya Taasisi na Taasisi (Institutional Agreements). Na hivi ndivyo Umma unavyoaminishwa kwa Makosa.

Hatuwezi kumlaumu Waziri Mkuu wala Rais kwa hilo ila washauri wao wa karibu, Spika wa Bunge na AG ambao wote ni Wanasheria. Nguvu kubwa aliyotumia Spika kuongoza Bunge kwa kuzima hoja za Wabunge kuhoji uhalisia wa Mkataba huo, na AG kunyamazia, pengine ni ishara ya kuwapo jambo hasi lililofichika

Sehemu ya Ridhio hilo inasema: “Hivyo basi, kwa kuzingatia manufaa ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayopata(kutokana) na Mkataba (sawa, sio MoU) huu, Bunge katika Mkutano wake wa 11, na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e) ya katiba ya JMT, linaazimia kuridhia Makubaliano (limejikanganya, ni Mkataba) kati ya Serikali ya JMT na Serikali ya Dubai kuhusu…”

Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba inaongelea juu ya Madaraka ya Bunge kujadili na kuridhia Mikataba inayohusu JMT na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa, kama huu wa DPW. Kama kwa tamko lake lenyewe, kwamba Bunge hilo liliridhia Mkataba (IGA) na sio Makubariano (MoU), hili la kuridhia MoU linatoka wapi?

Tumeliwa kwa Saini zetu

Umma haulalamikii MoU, wala Dubai kutaka kuwekeza. Unayolalamikia ni yale yaliyomo kwenye Mkataba (IGA), yenye kutishia uchumi na uhuru wa Nchi, na ambayo baada ya kuridhiwa na Bunge(na kutungiwa Sheria) ndiyo yatakayozaa na kudhibiti HGAs zijazo, kwa mujibu wa Mkataba huu. Hayabadilishwi wala kurekebishwa kwa kuwa yanakuwa juu ya Sheria za nchi, ikiwamo Katiba.

Ulivyo Mkataba, usimamizi wa Miradi utafanywa kwa kuzingatia Masharti ya IGA na Kanuni za HGA sambamba na Sheria za Tanzania kama zilivyokuwa siku ya kutiwa saini Mkataba na kama tu hazigongani na Masharti hayo, au iwapo tu zitarekebishwa kuendana na matakwa ya IGA, vinginevyo zifutwe.

Lisingekuwa tatizo kama ushirikiano/ubia unaolalamikiwa ungekuwa wa kibiashara kati ya TPA na DPW pekee kwa misingi ya MoU iliyoanzishwa, kama ambavyo tu TPA ilivyoingia MoU na Port of AntwepBruges International, Februari 23, 2023 kuhusu Ushauri, Maandalizi na Utekelezaji wa Miundombinu, Maendeleo, Usimamizi na Mipango ya Maendeleo ya Bandari nchini inayopaswa kutekelezwa bila haja ya IGA.

Ulaghai uliotumika kuuvisha Mkataba huu Koti la Ubia wa Kimataifa na Bunge letu kuridhia, ni Ukoloni hodhi ambao bila kulindwa na Ridhio la Bunge ni batili kwa Sheria zetu na Sheria za Kimataifa pia.

Sasa tuna kila sababu kuamini kwamba ziara ya Wabunge wetu Dubai, iliyogharamiwa na DPW siku chache kabla ya Bunge kuketi kuridhia Mkataba huu, badala ya Wabunge hao kwenda kwa wananchi kupata mawazo yao ilivyo jadi. Ilikuwa kiini macho na kishawishi kwa Wabunge hao kupitisha na kuridhia wasichokijua, au walikijua lakini wakaweka maslahi binafsi mbele.

Wanasheria na Wanasiasa wenye kupungukiwa Uzalendo wasiwatoe wananchi kwenye reli kwa chambo cha tende na halua, na kwa kuwaaminisha kwamba Mkataba kati ya Dubai/Tz haujatiwa Saini, wakati kinyume chake ndiyo kweli, kama tulivyoona hapo juu.

Yapi ya Mkataba yanayokera?

Ibara ya 4(1,2) na 5 ya Mkataba inataja maeneo ya Ushirikiano, Utekelezaji na Watekelezaji kuwa ni wa Kuendeleza na Kuboresha utendaji kazi wa Bandari zetu za Bahari na Maziwa na fursa zingine kuhusu Bandari, Maeneo huru ya Kiuchumi na Shoroba (corridors) za Kibiashara, Sekta za ugavi na Usafirishaji watu na vitu(Logistics) nchini, kwa kuruhusu Dubai na Taasisi za Dubai pekee kuchukua fursa hizo. Kazi na wajibu wa Tanzania itakuwa ni kuijulisha Dubai fursa hizo zinapotokea.

Kwa mujibu wa Ibara 4(3),(4),TPA na DPW si wenye Mkataba wala kuwa na Mamlaka juu yake, bali wao ni Watekelezaji tu wa Miradi kama Mawakala wa Dubai/Tz kwa kuzingatia IGA na Sheria ya Utekelezaji/Uwezeshaji na HGA kama kitendea kazi chao.

Ibara ya 15(1) inataka shughuli za Miradi kuzingatia Sheria za Tanzania kuhusu ubora wa Mazingira, Afya, Ustawi na Usalama Kazini(EOHSS) kwa viwango takiwa, isipokuwa kama Mradi husika utakuwa umebanwa na shinikizo au matakwa mengine ya kutekeleza kutoka kwa Wafadhili au Wakopeshaji wa Kimataifa. Chini ya Ibara 4(5), DPW ina jukumu la kutafuta fedha kutoka kwa wakopeshaji kwa ajili ya Kampuni za Mradi kuendeleza shughuli.

Ni kusema kwamba, kwa Dubai na DPW, Usafi na Usalama wa Mazingira, Afya za Watumishi na za watu na Usalama wa Kijamii, si mambo muhimu ya kupewa kipaumbele, ikilinganishwa na uchu wa Mitaji na Madeni kwa Wafadhili. Ni kinyume na Sheria za Uingereza, za Kimataifa na Sheria zetu zenye kuheshimu na kuzingatia kwa viwango vya juu mambo haya.

Kwa Dubai hili halishangazi kwani mpaka sasa Serikali ya Falme saba za Kiarabu (UAE) ikiwamo Dubai, hazijaridhia Mkataba wa Kimataifa juu ya wajibu wa nchi kulinda Haki za Wafanyakazi na jamaa za familia zao, wa Desemba 18,1990, kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa No.45/158, kama sehemu ya misingi ya Haki za Binadamu.

Ibara hii inafifisha na kuumbua ibara ya 17 juu ya mambo hayo kuonekana kama mzaha tu Kisheria. Ni kusema, ibara ya 17 inatoa, wakati Ibara ya 15(1) inanyakuwa kijanja haki hizo kwa mlango wa nyuma.

Ibara ya 23 inaweka Muda Wa Mkataba kuwa wa milele maadamu haja na shughuli za Bandari na za Mradi zitaendelea kuwapo; au kutokana na kufikia ukomo kwa HGAs na Mikataba yote ya Miradi. Na kama kutakuwa na mgogoro au mfarakano, Mkataba utaendelea kuwepo hadi hapo utakapokuwa umetatuliwa.

Neno “Mradi”(Project) limefafanuliwa kumaanisha shughuli yoyote au Mradi unaoendeshwa na Mwekezaji yeyote au Kampuni ya Mradi (DPW) au Washirika wake au Wakandarasi katika kukidhi madhumuni ya Mkataba huu, yakiwamo “kuendesha, kusimamia, kutawala na kutumia Bandari; wakati neno “Shughuli za Miradi” (Project Activity) limefafanuliwa kumaanisha shughuli yoyote inayoendeshwa na Mwekezaji au Kampuni ya Mradi au Washirika wake au Wakandarasi kuhusiana na Mradi.

Kwa jumla, Mkataba huu unahusika, sio tu na uendelezaji na uboreshaji wa Bandari pekee, bali unajumuisha pia uwekezaji, uendeshaji, kutawala, kumiliki, kusimamia na kudhibiti Bandari zote nchini hadi hapo shughuli hizi zitakapofikia kikomo.

Swali ni je, ni lini na wakati gani Mwekezaji au Mwendeshaji wa Bandari kiwango cha faida hodhi na turufu ilivyo chini ya Mkataba huu, atakubali kuachia unono huo kwa hiari? Kuna ukweli katika usemi kwamba, Mkataba huu hauna ukomo unaofahamika.

HGA tarajiwa haziwezi kutamka tofauti na IGA, kama ambavyo tu Sheria ya kawaida haiwezi kutamka kinyume cha Katiba ya nchi inavyotaka juu ya jambo linalotungiwa Sheria. Ni kwamba, kama ambavyo Katiba ya nchi ilivyo Sheria mama ya Sheria zote za nchi hivi kwamba Sheria inayokiuka Katiba ni batili kuanzia kutungwa kwake (void ab initio) ndivyo IGA ilivyo Sheria mama kwa HGA.

Kwa misingi ya Sheria za Uingereza ambazo Mkataba huu umechagua kutumia, hakuna Sheria iliyo na Kinga kwa udhalimu wa kukwida haki na misingi ya Sheria za kistaarabu kama inavyotaka ibara hii.

Hapa tena, hili halitushangazi, ikizingatiwa kwamba kwa UAE (ikiwamo Dubai), suala la haki za Kiraia na za Kisiasa si la kipaumbele zaidi ya “utukufu” na mali. Ukweli, hadi sasa UAE kama nchi, haijaridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Kiraia na za Kisiasa (International Covenant On Civil and Political Rights) wa Mwaka 1967, kama moja ya misingi mikuu ya Utawala bora kwa Mataifa.

Ibara ya 23(4) inatuhabarisha kuwa, mara taratibu zote za Mkataba kukamilika, nchi haitakuwa na haki tena ya kuukana, kujitoa, kusitisha au kukatisha Mkataba kwa sababu na kwa mazingira yoyote ukiwemo, ukiukaji mkubwa (fundamental/material breach) wa Mkataba, kubadilika kwa Mazingira kusipoepukika au kutarajiwa(force majeure) au kubadilika kwa Sheria za nchi, au mabadiliko ya Serikali na Sera za nchi, kuvunjika kwa Mahusiano ya Kidiplomasia au Kibalozi au sababu zingine halali zinazotambuliwa na Sheria za Kimataifa.

Kubwa hapa ni kwamba, Mkataba huu hautambui mabadiliko yoyote ya Kisheria hata kama ni ya kuendeleza nchi, au yenye manufaa kwa nchi na Wananchi kwenda na wakati kama mabadiliko hayo au Sheria mpya hiyo itakayotungwa itagusa maslahi ya DPW na Miradi yake.

Msimamo wa Sheria za Mikataba kote duniani na Sheria za Kimataifa pia, ni kwamba ukiukwaji mkubwa wa Mkataba unaotetewa na Mkataba huu na sababu zingine zote zilizotajwa hapa, ni sababu tosha kusababisha Mkatba kuvunjwa, kukatishwa au kusitishwa. Vivyo hivyo, Mkataba wowote unaofikiwa kwa madhumuni ya kukiukwa bila kuwajibisha upande unaokiuka ni batili tangu kuingiwa kwake.

Mikataba ya usimamizi na Utekelezaji Miradi (HGAs) tarajiwa na ambayo tunaambiwa itazingatia Maoni ya Wananchi, haitapelekwa Bungeni kwa sababu misingi yake imo na inatawaliwa na IGA iliyoridhiwa na Bunge [1(2)], wala haitawekwa hadharani kwa Umma kujua kwa sababu ni siri za DPW na TPA (10(1)). Ni wajibu wa PDW na Makampuni yake ya Miradi tusiyoyajua kupendekeza Masharti ya HGA na kazi ya TPA itakuwa ni kupokea na kutekeleza yote kwa mujibu wa Ibara ya 5(3).

Tumesaini IGA kukubali, pamoja na mambo mengine, kwamba Mkataba huu hauna mawaa na kwamba unakubalika na pande zote pasipo na maoni kinzani. Pia kwamba nyongeza na viambatisho vyake vitakavyotiwa saini na pande zote mbili(juu ya nini na kwa Mamlaka ya nani?) mara kwa mara vitahesabiwa kuwa sehemu ya Mkataba(24 (1),(2).

Chini ya Ibara ya 25(4), Matakwa ya Mkataba yanapaswa kuridhiwa na kutungiwa Sheria na Bunge kabla ya utekelezaji, isipokuwa yale yanayohusu kazi za awali (Early Project Activities – EPA) kama vile ujenzi wa Miundombinu na Barabara kutoka barabara kuu kwenda kwenye eneo la Mradi. Kwa hili, ni kinyume cha sheria kwa baadhi ya vifungu vya sheria inayotungwa kuanza kutumika kabla ya Sheria yenyewe kuanza kama ulivyo Mkataba huu.

Mkataba wa Ushirikiano au Uwekezaji?

Mkataba huu unatambulishwa kama Mkataba wa Ushirikiano wa nchi mbili, lakini yaliyomo na mengine mengi yatakayojitokeza yana sura ya Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya Kibiashara kwa maeneo teule. Ni mchanganyiko wa shughuli za kidiplomasia (Ushirikiano), biashara na usimamizi wa Miradi (Uwekezaji) mambo mawili tofauti kwa hadhi, uendeshaji wake na kwa Sheria tofauti ndani ya Mkataba Mmoja. Kwa lugha rahisi, Mkataba huu ni aina ya “Mixed Grill” au “Mchanganyiko maalumu”.

Hata Bunge kwa upande wake, kama tulivyoona, limejikanyaga kwa kutamka “Mkataba wa Ushirikiano” IGA, na hapo hapo kutamka “Ridhio la Makubaliano”, kumaanisha “MoU” kuashiria kutoelewa kipi hasa lilikuwa likiridhia. Haya pekee yanalifanya Ridhio hilo na Sheria itakayotungiwa kuwa batili.

Kamusi ya Sheria inatafsiri neno “ratify”, yaani “kuridhia” kuwa ni “approval of a Treaty by the State to make it officially and legally binding on the State”. Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, “ni kuthibitisha Mkataba ulioingiwa kati ya nchi na nchi, kunakofanywa na nchi kuupa nguvu ya Kisheria wa kufuatwa na kutekelezwa na nchi hiyo”.

Kwa kuwa yote yaliyomo katika IGA yanahusu Biashara, Uwekezaji na Usimamizi wa Miradi ya kiwekezaji, hapakuwa na haja ya IGA wala Ridhio la Bunge kwa sababu Sheria na Sera zetu za Uwekezaji zinaruhusu bila haja ya kuingia IGA.

Kuhusu uwekezaji katika Bandari, mamlaka kwa mambo hayo yanasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) No 17 ya Mwaka 2004 inayotumika Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa kuwa Bandari za Bahari, Maziwa na Forodha ni jambo la Muungano.

Kwa kuwa Mkataba huu umeingiwa na Rais wa JMT inayojumuisha pia Zanzibar, unaigusa pia Zanzibar hata kama hapana Mradi wa kuingizwa au kutekelezwa kwa sasa. Sheria ya Bandari Zanzibar ni Sheria ndogo kwa Sheria ya Muungano(TPA) Katika Nyanja Hizo.

Kazi na Mamlaka ya TPA, kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria hiyo, ni pamoja na 12(1)(a), Kumiliki ardhi na maji yaliyomo ndani ya Mipaka ya Bandari; 12(1)(d) Kupatana au kuingia Maelewano (MoU) au Mkataba na mtu yeyote wa kupangisha, Maridhiano, Usimamizi, Huduma au aina yoyote ya Mpangilio wa Kimkataba na mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na Shirika lililoanzishwa Kisheria kwa Madhumuni ya TPA kukasimu Mamlaka yake kwa Shirika hilo kufanya shughuli zake kama itakavyokuwa kwenye Hati ya Mkataba.

Mamlaka mengine ni 12(1)(l) Kukuza uwekezaji wa ndani na wa kigeni(pamoja na kuingia Mikataba) katika huduma za Bandari na Vietendea Kazi, na (12(1)(v) Kusimamia viwango vya juu vya Usalama wa Bandari na Mipaka ya Bandari.

Tunarudia kusema kwamba, utaratibu wa MoU iliyoingiwa 27/2/2022 kati ya TPA na DPW ambayo hatimaye ungezaa Mkataba wa kawaida wa Kibiashara au uwekezaji, tofauti na IGA na HGAs tarajiwa, ndio sahihi uliotakiwa kuwa kwa madhumuni hayo, tofauti na utaratibu wa Kidiplomasia wa IGA.







IGA kwa ajili gani?

Mkataba wa IGA umetumika makusudi na kimkakati kuupa Uwekezaji huu na Miradi ya PDW na Makampuni yake hadhi ya kidiplomasia tofauti na Mikataba mingine ya Kibiashara na Kiuwekezaji iliyopata kuingiwa hapa nchini. Lengo ni kufanya uogopwe kwa kinga ya kidiplomasia na kwa nguvu ya Sheria ya Ridhio la Bunge kuhalalisha yote yaliyomo, mema na mabaya, ya ukweli na ya uongo kama tulivyokwishaona hapo juu.

Sheria iliyotungwa na Bunge letu kuridhia Mkataba huu itaungana na Sheria pacha nyingine kama hii, neno kwa neno, ya kuridhia IGA, itakayotungwa na Bunge la Dubai(kama lipo) na kuzaa Sheria moja ya utekelezaji yenye nguvu na hadhi ya Kikatiba kwa nchi hizi mbili. Wakuu wa nchi watabadilishana Sheria hizi kwa misingi ya Kidiplomasia na kuwa Sheria inayobana nchi zote mbili juu ya yaliyokusudiwa.

Ni kusema, chini ya IGA na HGAs tarajiwa, kwa kupewa nguvu na Sheria za Mabunge ya nchi mbili hizi, Sheria ya TPA itapoteza nguvu kwa mambo ya Bandari. itatekeleza wajibu ule tu uliotajwa kwenye IGA/HGAs hata kama ni kwa kukiuka Sheria yake yenyewe, madhumuni na majukumu yake ya Kisheria tuliyotaja hapo juu.

Mfano, kwa DPW kutaka kumilikishwa ardhi 6(1); 8(b),(c), na kwa kiwango fulani kuwa na kauli kuhusu mambo ya usalama wa nchi, siri na usalama wa Bandari (12(a), (c), (d) na (e), sio tu ni kwenda kinyume na Sera ya Umma na Usalama wa nchi, bali ni kupora majukumu hayo ya TPA kama taasisi ya Serikali; majukumu ambayo hayahamishiki wala kugawanyika.

Marekani ilipowatimua DPW nchini humo Mwaka 2006, baada ya kuonekana kuwa na kauli kwa mengi maeneo ya Bandari, yakiwemo mambo ya Usalama, ilikuwa ni kwa misingi ya Usalama wa nchi. Tunapaswa kujifunza kutoka kwa wenzetu wenye kujali Usalama wa Nchi zao kama Marekani.

Mbaya zaidi Mkataba huu na Sheria iliyopitishwa na Bunge zinakiuka Sera ya Umma na Sheria kwa kuegemea upande mmoja wa DPW kufanya kazi ya DPW kuwa ya kutoa majukumu na wajibu kwa Tanzania, na kazi pekee ya Tanzania ni kupokea na kutekeleza majukumu hayo.

Kwa IGA kuruhusu ukiukaji wa Mkataba bila hatua za kuchukua kwa mujibu wa Sheria zinazotambuliwa kimataifa (23(4)); au IGA kutambua shughuli za Mradi zilizofanyika kabla ya tarehe ya kuanza kwa Mkataba au kuundwa kwa HGAs 25(3), na kwa nchi halali kulazimishwa kutotumia, kutotambua au kuwa sehemu ya Sheria yoyote halali ya ndani au ya Kimataifa ilimradi kukidhi matakwa ya IGA na DPW, au kuzuiwa kuwajibika Kisheria na kihalali kuzingatia au kutekeleza Sheria yoyote ya ndani au ya Kimataifa, Kanuni au Mikataba halali kwa kukinzana na Mkataba huu, HGAs na Mradi wowote ambao nchi ni Mshirika, ni kufubaza Sheria zetu za nchi, utawala bora na utawala wa Sheria. Huko ni kukaribisha migogoro, mifarakano na chuki katika nyanja za Mahusiano na diplomasia kimataifa

Uhalali wa Kisheria

Mkataba huu utatawaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia Sheria za Uingereza. Lakini, kama tulivyoona, unakiuka mengi ya Mfumo wa Sheria hizo, ikiwa ni pamoja na juu ya uhalali na uwezo Kisheria unaohojika, wa waliotia saini au kuingia Mkataba huu (28), achilia mbali ya kuwa kinyume cha Sera za Umma na mengine mengi.

Msimamo wa Kisheria juu ya hayo ulikwishawekwa wazi katika Shauri la Regazzoni v.KC Sethia (1956) 2 Q.B 490, kwamba “Mkataba utakuwa haramu na kinyume cha Sheria kama utafungwa katika nchi moja kwa kusudi la kutekelezwa katika nchi nyingine kinyume au kwa kukiuka Sera ya Umma au Sheria za nchi hiyo; au kwa lengo la kumwezesha mtu kuzivunja au kusaidia katika kufanya hivyo”. Mkataba wa Dubai/Tanzania ni wa kundi hilo.

Kinachoshangaza ni kwa nini Mkataba kama huo umepitia ngazi zote za Serikali na Bunge lenye kuongozwa na Spika Msomi wa Sheria ngazi ya Shahada ya Uzamivu, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Msomi kwa kiwango hicho; na kwa nini Umma ulifichwa. Huko ni kukaribisha ghadhabu ya Umma. ni ishara pia ya kujengeka kwa matabaka nchini.

Ni hatari kwa ustawi wa nchi jamii inapogawanyika kwa misingi ya kiuchumi na kisiasa kati ya “Wao” (Waheshimiwa, Matajiri au Walala heri) na “Sisi” (Wadunda kazi, au Walala hoi), Wavuja jasho bila kipato.

HGA kwa Maslahi ya nani?

Imeelezwa, “Home Government Agreement”(HGA) au Mkataba kati ya Serikali Mwenyeji na Mwekezaji, mbali na IGA kwa mujibu wa Mkataba Ushirikiano huu, ni Mkataba wa Serikali kupitia TPA na DPW kwa niaba ya Shirika la Bandari na Forodha la Dubai (PCFC) na kwa niaba pia ya Serikali ya Dubai, juu ya uendeshaji wa Bandari.

DPW itakuwa ndiyo yenye kutoa mapendekezo na TPA/Serikali kupokea kwa kuwa taratibu zote, mifumo ya uendeshaji na wajibu wa Serikali yalikwishawekwa kwenye IGA na Sheria ya Bunge, hivi kwamba Maidhinisho Serikali itakayotoa chini ya Mkataba huu hayawezi kufutwa, kuboreshwa au kutorudiwa(to renew) Dubai ikitaka.

Kwa kawaida na Kisheria pia, HGA huingiwa kati ya Serikali na Mwekezaji wa Kigeni kujumuisha vifungu juu ya udhibiti (Stabilization) ili kupunguza au kuzuia hatari za kifedha na kisiasa zinazoweza kumpata Mwekezaji kwa sababu ya mabadiliko ya ghafla ya Sheria za nchi iwapo tu haki za Mwekezaji huyo hazikuwekwa au kufafanuliwa kwenye IGA.

Kwa hili, yaliyopaswa kuwa kwenye HGA yamewekwa na kufafanuliwa vyema kwenye IGA, kuanzia Ibara ya 4 hadi ya 31 kufanya HGA kutohitajika. Ni kusema, Mkataba wa Dubai/Tanzania ulivyo sasa ni vyote viwili, yaani ni IGA na ni HGA pia. Lakini, ni kwa nini HGA inatakiwa hapa?

Kunaweza kuwa na sababu nyingi, zote zisizo za msingi wala Maslahi kwa nchi. Moja ni kwa DPW kutaka kushinikiza Masharti zaidi kinyemela kwa kutumia udhaifu wetu ikizingatiwa kwamba HGA ni zao la IGA kuikweza kuwa na nguvu za Kisheria na Kikatiba pia.

Pili, ni kutaka kufanya HGA kuwa juu ya Sheria za nchi na za Kimataifa(ikiwamo Sheria ya TPA) kuhusu Mradi huu, kama inavyofafanuliwa kwenye Ibara ya 26 na 27 ya IGA. Hii ni kutokana na IGA kupewa nguvu za Kisheria kama sehemu ya Sheria za nchi.

IGA na HGA zinatambua siku ya kutiwa saini IGA(25/10/2023) kuwa tarehe kigezo na kipimo anzio kisichobadilika kwa yatakayohusu Mkataba huu kama yalivyokuwa tarehe hiyo (Ibara 30).

Sheria ya uwekezaji iliyokuwa ikitumika wakati huo, Namba 26 ya 1997, iliwataka wawekezaji wa Kigeni kwamba, ili waruhusiwe na kulindwa na pia kustahili kupata vivutio kwa uwekezaji, kuwa na mtaji usiopungua dola za Kimarekani 5,000,000 kama ilivyobainishwa tu kwenye MoU ya TPA na DPW ya tarehe 27/2/2022.

Hata hivyo, chini ya Sheria mpya ya Uwekezaji ya Mwaka 2022, iliyoanza kutumika Desemba 2022, kiwango hicho kimeongezwa kufikia dola 50,000,000, sambamba na Mwekezaji kutakiwa kuzalisha ajira zisizopungua 1,000(DPW ina watumishi 4,500 kote duniani) ili astahili kupewa vivutio, ikiwamo misamaha ya Kodi. Bila shaka DPW walijua Sheria hiyo inakuja wakati wakisaini Mkataba.

Kwa hiyo kuweka 25 Oktoba 2022 kwenye IGA na HGA kuwa tarehe kigezo kunawakingia kifua DPW wasilipe kiwango kipya cha Mtaji na dhidi ya Matakwa ya Sheria zingine zote zilizotungwa au kurekebishwa kwa maslahi ya Taifa baada ya tarehe hiyo.

Hitimisho

Sakata la Mkataba wa Dubai/Tanzania na mtafaruku wa Kisiasa na Kijamii liliozua juu ya uwekezaji tarajiwa wa Kampuni ya PDW ya Dubai, halitokani na kutaka kuzuia uwekezaji wa DPW nchini. Hilo halihitaji maelezo kwa kuwa Sheria zetu ziko wazi; zinaruhusu bila ubaguzi.

Wala sio kutetea ufisadi uliokithiri kwenye Bandari zetu na Serikali kuonekana kuinua mikono. Wala halimaanishi Dubai kubaguliwa kama “nchi” ya Kigeni kwa misingi ya kiuchumi, kiitikadi za Kisiasa au Kidini nchini. Kufikiri hivyo ni uzuzu, na kusema kweli ni uzezeta wa kufarakanisha wananchi na kudhoofisha umoja wetu wa Kimataifa.

Sakata hili ni juu ya Mkataba mbovu wa kufilisi nchi na kudhalilisha Taifa uliopitishwa na wenye mamlaka kimya kimya, kwa kificho, hila na ghiliba. Ni tukio linalozua ghadhabu ya Umma pale watetezi wake wanapojaribu kupotosha kwa kuulisha Umma propaganda za yasiyokuwemo wala kuandikwa kwenye Mkataba. Kwa lengo gani na kwa manufaa ya nani?.

Lakini Mwananchi wa leo si yule tuliyezoea kumhadaa na kumpora jasho lake, haki zake za Kiraia na haki za Kiuchumi miaka iliyopita, akakaa kimya kwa kuridhia maovu hayo.

Wananchi wana haki ya kuuliza kutaka kujua, kwa mfano; Kwa nini ni Mkataba wa Bandari zote za Bahari, Maziwa na nchi kavu, zilizopo(kwa awamu, kwa kuanzia na Dar) na zijazo? Kwa nini Mwekezaji alindwe na IGA, na kwa nini IGA imeingiwa kati ya nchi na Kampuni kupitia Mgongo wa Mji wa Dubai badala ya nchi ya UAE?.

Vivyo hivyo wanataka kujua, kwa nini Mkataba haukuwekwa kwenye tovuti ya Bunge ilivyojadi kwa Umma kujua?, na maswali mengine ya msingi.

Umbumbumbu wa Katiba kwa Umma, Wabunge na wenye Mamlaka kutenda, kwa kujua au kwa kutokujua au kwa kudharau na kubaza Katiba ni mambo yaliyokuza utata kwa Mkataba huu. Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna mtu mmoja wala kikundi cha watu, kinachoweza kudai kustahili au kushikilia Hati miliki ya nchi hii bali Wananchi Wazalendo.

Inapokuwa hivyo, kwa nini Wananchi wazuiwe au kuzodolewa wanapotumia Haki yao ya Kikatiba kujitosa kuchangia mawazo kwa uhuru juu ya Sakata hili ilimradi Katiba ya nchi (Ibara 21(2)) inawapa “Haki na Uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia yanayowahusu wao, maisha yao au yanayolihusu Taifa”?

Kwa nini isiwe hivyo, bila ya kulishwa maneno yakawajaa kinywani, asemavyo Franz Fanon tulivyomnukuu hapo juu; tabia na utamaduni wa kuabudu, kuimba kusifu “Mashujaa” wa kuumba wakati Katiba (Ibara ya 18(a)) inatoa Uhuru kwa kila mtu “kuwa na Maoni na kuelezea fikra zake”?

Kwa nini Wananchi waachwe kumangamanga kujitafutia ukweli wa matukio kwa kututusa, wakati hilo ni jukumu na wajibu wa Serikali Kikatiba(Ibara 18(d)) kwamba, “kila mtu anayo Haki ya kupewa Taarifa(sahihi na kwa uwazi) wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za Wananchi, na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii”, kama hili la uwekezaji tata?

Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere(1961-1985), alifanya hivyo kupitia Mikutano yake na Wazee(mara nyingi wa Dar es Salaam) aliyoitisha, kama tu alivyofanya Rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi(1985-1995).

Rais wa tatu, Benjamin William Mkapa(1995-2005), na Rais wa nne, Jakaya Mrisho Kikwete(2005-2015) wao walihutubia Taifa kila mwisho wa Mwezi chini ya utaratibu waliojiwekea.

Lakini kuanzia utawala wa Rais wa tano, Hayati John Pombe Magufuli(2015-2021), na wa Rais wa sita, Mama Samia Suluhu Hassan(2021-), uzingatiaji wa takwa hili la Kikatiba ulitoweka na watu kuanza kujitafutia matukio makuu ya nchi kwa kututusa. Umma unapotafuta ukweli wa jambo kama hili la DPW kwa njia hii nani alaumiwe?

Huu si Mkataba wa kwanza tata zama hizi, wenye lengo baya kwa nchi. Hatujasahau jinsi Mkataba wa ovyo wa kufua na kusambaza umeme ulioingiwa kati ya TANESCO kwa niaba ya Serikali, na Kampuni la Mechmar la Malaysia, Mwaka 1995; lililoungana na Kampuni ya VIPEM ya hapa nchini, kuunda ubia unaotiwa IPTL(Independent Power Tanzania Ltd), ulivyofilisi nchi na kudumaza uchumi wa Taifa hadi leo.

Toka mwanzo, Mechmar lililomiliki asilimia 70 ya Hisa za IPTL, lilitambulishwa kama Shirika la Serikali ya Malaysia, kama ambavyo DPW ilivyotambulishwa kuwa ya Serikali ya Dubai. Ilielezwa kuwa Mkataba huo wa kufilisi nchi ulikuwa kwa lengo la kuimarisha Ushirikiano wa nchi masikini za Dunia ya tatu chini ya Tume ya “South – South Commision” ambayo Mwalimu Nyerere alipata kuwa Mwenyekiti wake. Lakini tofauti na huu kati yetu na DPW, japo kwa mazingira yale yale, Mkataba wa Mechmar haukuwa wa aina ya IGA na HGA, wala haukuridhiwa na Bunge kwa kutungiwa Sheria.

Aidha, hatujasahau pia Mwaka 1999, iliundwa Kampuni ya Meremeta kama Ubia kati ya Tanzania na Kampuni ya Kigeni ya TRIENNEX kuendesha Mradi wa kusaidia wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu nchini na uvunaji wa Dhahabu kupitia Mgodi wa Buhemba, Msoma. Tuliambiwa Mradi huo ulikuwa wa Usalama wa Taifa(TISS) kwamba haukupaswa kuingiliwa wala kukaguliwa na Serikali.

Watanzania, kwa upole na uungwana wao wakaamini hivyo hadi Kampuni hiyo ilipokomba Dhahabu yote, ndipo walipotambua ulikuwa Mradi na Ubia wa kilaghai wa kupora rasilimali za nchi. BoT ikalazimika kulipa matrilioni ya fedha kwa madai ya Kampuni bandia kwa kisingizio cha kukiuka Mkataba.

Wanufaika wa utapeli huo walikuwa ni pamoja na wamiliki wa Kampuni bandia za hapa nchini kama vile “Kagoda”, “Deep Green” na zingine ambazo wamiliki wao bado wapo wakirandaranda katikati na miongoni mwetu.

Sakata hili ni ishara ya jamii kuanza kujitambua kwa kukataa kutwezwa bila kujibu. Pongezi kwa Rais, Mheshimiwa, Dakta Samia Suluhu Hassan kwa hulka yake ya uvumilivu, ya kuheshimu mawazo ya wengine na Uhuru wa kujieleza.

Nguvu kubwa inayotumika kutetea Mkataba huu kichwa kichwa ni Unabii mbaya kwa enzi za ufisadi wa kitabaka wa Miaka ya 1990/2000 kurejea ambapo kikundi kidogo cha Wanasiasa kwa kuungana na tabaka la Wafanyabiashara wakubwa, kwa kupewa nguvu na ubeberu wa Kimataifa chini ya Sera za Soko Huria na Utandawazi, kiliteka Serikali kwa nguvu turufu kuonekana kuwa juu ya Serikali Madarakani. Ufisadi ukatia fora, Maadili ya uongozi na ya Taifa yakapotea, Uzalendo ukayoyoma, Demokrasia ikatiwa kitanzi.

Leo, kwa mazingira yetu, si aibu tena kwa wananchi kutakiwa kujitoa kwa Maendeleo ya baadaye huku wakishuhudia wachache wakinufaika kwa rasilimali za Taifa, Umma wa wakala hoi kugeuzwa kundi la masikini wa Kaya hohe hahe, bakuli la “omba omba” mkononi kusubiri misaada ya kupunguza umasikini kutoka “TASAF”, wakiaminishwa kuwa Sekta binafsi na Uwekezaji wa Kigeni ndizo injini pekee za Maendeleo, kwa hiyo tuwapambe maua bila kuhoji wawekezavyo.

Kitendo cha Bunge kuuficha Umma juu ya IGA kati ya Dubai na Tanzania, kinatia doa Demokrasia ya uwakilishi kwa njia ya Bunge kwa kujenga jamii iliyojifunga; na kwa mambo ya Umma kuendeshwa kwa siri na wananchi kugeuzwa watazamaji tu, wapiga majungu wanapo hoji au kulalamika badala ya kuonekana washiriki na watoa hoja kwa yanayogusa maisha yao.

Kinatia doa Mstakabali wa Nchi juu ya Utawala Bora na Utawala wa Sheria. Sakata hili linatuambia kwa kuonya, kama lilivyo jina la Kitabu cha Mwanafasihi Nguli Baram Afrika, hayati Chinua Achebe, “Hamkani, si Shwari Tena”(No Longer At Ease) japo hatuchelewa kujisahihisha. Babu wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, aliliona hili mapema Miaka ya 1990 baada ya kung’atuka madarakani, alisema kwa kuonya:

“Ninyi Waswahili (Watawala) wachache, mnategemea kweli kuwatawala watu kwa shuruti,ulaghai na nguvu wakati mkiona wanazidi kupoteza matumaini na mtarajie watakaa kimya kwa amani?

“Amani”, alisema Mwalimu, “ni zao la matumaini; matumaini yakipotea kutatokea vurugu na mitafaruku ya Kijamii. Nitashangaa kama Watanzania hawa, kwa uwingi wao, watakataa kuasi. Kwa nini wasiasi? Labda kama watu hawa ni wajinga, mazuzu au mazezeta kukubali kutawaliwa kwa ulaghai, kutwezwa na kukandamizwa na wachache ndani ya nchi yao”.

Yanayotokea ni uthibitisho tosha kwamba Watanzania si mazuzu tena. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.

 
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi ni kwanini bado serikali hii ya kifisadi haijapeleka mswada wa DPW bungeni ujadiliwe hadi tupate majibu ya wizi huu unaofanywa na mafisi wa CCM?
 
Kwa hili linalofanyika sasa mabapo DPW wanataka kuwafukuza wazalendo kutoka bandarini ili wabaki peke yao wapitishe silaha na madawa ya kulevya, ni bora hata Rais Samia awapishe ikulu ahamie nchi nyingine.
 
Nitawashangaa sana watumishi wa TPA watakaositisha mikataba yao na kuhamia DPW. Miarabu ni mijitu midini na minyanyasaji sana. Haikawii pia kuwafundisha ushoga. Kuweni makini na hiyo miarabu koko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…