johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Msemaji wa serikali ametolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa, haki za binadamu na kustaafu kwa CAG.
Dr Abbas amesema ukiachalia mbali CAG hata Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amewekewa kanuni zinazombana na kumuongoza katika utendaji wake wa kila siku.
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa Dr Abbas amesema mambo yote yamekwenda vizuri na wenye malalamiko watasikilizwa.
Kadhalika amewataka wananchi kuwapuuza watu wanaojiita "wachambuzi wa siasa" kwa kuwa watu hao wamejaa ubabaishaji na uchochezi.
Chanzo: Star tv habari