Boss Kama biashara ni huria na nzuri kodi ya duka inaweza fika juu sana. Kipindi cha Jk kuna maeneo kupata tu unatoa kilemba Tsh 800,000/=, hii sio kodi ni asante dalali kwa dili. Ukishafanya hivi unakutanishwa na mwenye nyumba naye anataka miezi isiyopungua 6, wakati mwingine wanakataa wanataka mwaka mzima ndo unapewa funguo.
Kufikia 2019 wenye nyumba wanakuomba ujishikize tu maana hakuna mkodishaji na maeneo yalikuwa wazi hakuna biashara, hakuna mpangishaji, mpaka 300,000 unaitiwa frem na dalali ulipe mwezi mwezi na wewe mpangaji unahisi utapoteza hela tu, biashara hazilipi. Bora uweke mzigo godown uwape machinga.