Dr. Chris Cyrilo: Kwa Upepo huu kama ataondoka CHADEMA utakisomba chama chote siku moja majaribio yote ya kumwita Msaliti yamekwama Lissu ni shujaa tu

Kuna Mwamba kule chato alipambana na wakati, watu walimshauri sana. Akakaza shingo
Yule jamaa angetuliza kichwa na kuamua kuwaunganisha watanzania angeipeleka nchi mbali sana.
Badala yake akabadilika na kuwa mnafiki. Majukwaani anaimba maendeleo hayana Chama, gizani anateka, anaua na kufunga wapinzani. Huku akiwa amejiapiza kuua kabisa na huo upinzani wenyewe.
Akaishia alipoishia
 
Yule jamaa anaye alifeli kama mbowe
 
Mkuu Tafuta kazi nyingine.....kibarua kinaensa kuota nyasi
Ngoja nikupe taarifa kidogo
Nilimaliza UDSM Bsc 1983, MSc...1990................nikafanya kazi kooooooooooooooote unakoweza kufikiria. sasa nipo nyumbani nakula kapensheni kaduchu πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ ..... (nitacheki miaka vema)

Hivyo you can guess my age... siajiliwi kokote at this age, ila bado niko very energetic, quite energetic na vimiradi vyangu vya kunifanya niweze kukaa kwenye desktop kuwasiliana nawe hapa JF!

Have a nice Sunday
 
Wapiga ramli kipindi cha uchaguzi hawakosi. Hawa watasema hivi, wale vile. Sisi watazamaji tunasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa chama.
 
Labda tuweke sawa, moja ya sababu ya kutenguliwa ubunge wa Azim Premji ni swala la uraia.
Chadema katika uhai wake hakijawahi kupata katibu mkuu Bora wa chama Kama Dr. Slaa na mpaka Sasa hivi wameshindwa kuziba pengi lake. Kumwita mtu msaliti kisa wametofautiana ndio matokeo ya chawa Kama Ntobi, Yeriko, Bon Yai na wengineo.
Wacha wafu wazikane.
 
Tukisema Lissu ni shupavu na shujaa tunapuuzwa. kina besigye, tsvangirai, ingabire, maalim seif na odinga wakasome kwa Lissu. Lissu hana kikundi cha kumpambania na si mjeshi lakini anahenyesha makundi makubwa mawili na nusu ya kisiasa na kiharakati hasi dhidi yake lakini anasonga mbele tu. tunaita one man show, imegeuka kuwa burudani kama sinema fulani hivi yeye akiwa ni sterling akipambana na majambazi/magaidi/mafia/majahili wakatili na anawafyekelea mbali pamoja na wingi wao na maguvu yao. Wapo duniani wanatoa tuzo ya ushupavu na ushujaa apewe mtu huyu yungali hai?
 
Lissu si mjinga, ni mtu mwelevu sana. Kama anaipenda siasa anasehemu 2 tu. Chadema na CCM.

Ama aamue kuachana kabisa na siasa, aende kwa familia yake ama abakie kufanya kazi za uwakili bila kufanya siasa.

Naamini vyoyote iwavyo bado ataendelea kuwa mtu bingwa sana.
 
Mbowe atumie busara watu wamemchoka
 
Mjinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…