Kishimbe wa Kishimbe
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 5,566
- 5,477
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa kuropoka ndo kuna mcost.Hakuna kubembeleza wanafiki na wajasiliamali wa kisiasa.
Lisu kaza hapohapo
... tofautisha kati ya:Hivi team ya Mbowe akina Yericho Nyerere, akina Boni wao wanazungumza lugha nyepesi kuhusu Tundu Lissu? Na kama hawatumwi na Mbowe ni lini Mbowe ameonyesha kutohusika na akina Yericho Nyerere? Kama aliyosema ni kweli basi CHADEMA wajitafakari lakini kama si kweli basi Lissu mumhukumu.
20+ miaka aliyoongoza Mbowe haoni kuwa enough is enough awapishe wengine na awape ushirikiano ili waipeleke CHADEMA mbele? Mbowe na team yake wanaamini bila yeye CHADEMA haiwezi kusonga mbele?
Ninaamini kama Mbowe angekuwa na hekima angesoma alama za nyakati angemuachia Lissu peacefully kukomaa inaashiria kuwa vitu anaficha hataki vije kujulikana
Jamaa ana tuhuma kubwa sana za kuvujisha siri za kamati kuu, kama ikithibitika basi naona akipata rungu la kichwa.Lisu anafaa kabisa, Lisu anafaa kabisa, Lisu anafaa Kabisa, kabisa! The smartest upstairs Tanzanian Ever
My concern ni kuropoka alikoropoka Juzi, ku behave kama alivyo behave! Unaweza kuwa kuna mambo huyapendi wenzako wanafanya,unakaa unaangali the "friendly" way to air your views.
Kwani lazima uropoke kwa maadui wako CCM? Lisu kwa hilo alikosea sana, ndiyo kuropoka kutochagua useme lipi, uache lipi.....na wakati gani, mbele ya nani etc etc
Hatuelewani, hamnielewi msimamo wangu, to me kama mlivyo wengi, Mbowe alitakiwa apumzike amwachie Lisu....nilikuwa line hiyo kama walivyo wengi X na JF na kila mmoja, lakini baada ya kumuona anaanamga wenzake kadamnasi......nikawa na mashaka intergrity ya maamuzi yake huko mbeleni!
Mwisho: Andiko lako ni zuri.......zuri sana .... we need democracy, democracy, democracy!
Ulipokosea...kututukana kuwa tunashpaza shingo š š š š š š ššš
Sawa ndio maana nikasema ningelikuwa Dokta.Ndio maana wewe sio Dokta.
Madokta hawasubiri mtu mpaka afe ndio wafanya vipimo.
Wanapima kabla mambi hayajaharibika.
SahihiLowassa (japo hayupo duniani) akasome kwa lissu kwa nyomi atakayoondoka nayo kuelekea atakapotua ila isiwe ccm. Ni nyomi ya kihistoria kuwahi kutokea kwenye chama cha upinzani. Atahama na wanachama na mashabiki zake ambao humpigia kura
Uhalisia unaongea au hisia zako? Mjadala ni nini hapa Lissu na Mbowe kuweka dhamira ya kugombea uenyekiti au la?... tofautisha kati ya:
1) Kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti.
NA
2) Kuomba kupewa uenyekiti!
... Uenyekiti hautolewi bila kuchukua fomu na kwakua zimetolewa fomu kadhaa, sio Moja, basi ni rukhsa yeyote kuchukua pia!Uhalisia unaongea au hisia zako? Mjadala ni nini hapa Lissu na Mbowe kuweka dhamira ya kugombea uenyekiti au la?
Hizo unazoongea ni process za kuingia kinyang'anyiro cha kugombea uenyekiti, utaomba kupewa uenyekiti bila kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti? Bora kukaa kimya kama huna la kusema
Nini msingi wa hoja yako? Isiwe tunabishana huyu samaki, mwingine akisema hapana huyu ni somba mwingine hamjui huyu ni kambale huoni sharubu. Mwingine anasema this is fish you peasants.... Uenyekiti hautolewi bila kuchukua fomu na kwakua zimetolewa fomu kadhaa, sio Moja, basi ni rukhsa yeyote kuchukua pia!
BOKSI LA KURA!
Hana umaarufu kumzidi Dr Slaa sawa, Mbowe anao umaarufu kumzidi Tundu Lissu kwa sasa?Bado Lissu hana umaarufu kama aliokuwa nao Dr. Slaa...
Endeleeni kumjaza upepo.
Zitto = ACT, Hamad = ADC, Lisu = ?
Lissu haepukikiMAJARIBIO YOTE YA KUTAKA TUNDU LISSU AONEKANE MSALITI NDANI YA CHADEMA YAMESHINDWA VIBAYA SANA.
WATANZANIA NA WANACHADEMA WAMEKATAA NA MBINU HII IMESHAFELI VIBAYA SANA.
Je! UPEPO WA LISSU UTAPITA KAMA WALIVYOPITA WENGINE?
KUELEKEA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CHADEMA - TAIFA
Sehemu III
"Kila kizazi kinapaswa kuwa na dhamira yake ya kutimiza au kuisaliti, katika hali ya uwazi kabisa" Fratz Fannon
Oktoba 1993 alifariki mtu aliyeitwa Rajab Omar Mbano Kakolwa, aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya CCM. Hii ilimaanisha kungekuwa na uchaguzi mdogo kwa ajili ya kujaza nafasi iliyoachwa wazi. Mapema mwaka uliofuata, 1994 uchaguzi mdogo uliwakutanisha miamba minne ya siasa za Kigoma; Azim Premji wa CCM, Kashugu Anzaruni wa TADEA, Hussein Beji wa NCCR na Dr. Amani Walid Kaborou wa CHADEMA. Matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Azim Dewji wa CCM kwa kupata kura 9453 akifuatiwa na Dr. Amani Walid Kaborou wa CHADEMA kwa kura 5325.
Hatahivyo Dr. Kaborou alipinga matokeo hayo mahakamani kwa hoja 14, zikiwemo hoja za mgombea wa CCM kusaidiwa na serikali ya Rais Mwinyi kwa kupewa usafiri wa serikali, upendeleo kupitia redio ya serikali (enzi hizo Radio Tanzania Dar es Salaam au RTD) kwa Azim Dewji, na kutumia fedha nyingi kinyume na sheria za uchaguzi. Agosti 1994, mahakama kuu ilifuta matokeo ya uchaguzi na kuacha tena jimbo la Kigoma likiwa wazi. Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ilikata rufaa na kupeleka kesi hiyo Mahakama ya Rufa, lakini kufikia Desemba 1994 tume ya uchaguzi ilitangaza kutokuwa na uchaguzi tena katika jimbo hilo hadi Uchaguzi Mkuu wa 1995.
Dr. Amani Kaborou, mkufunzi wa Historia aliyekuwa akifundisha huko Marekani, na baadaye kurudi Kigoma kujiunga na siasa za upinzani mapema kabisa baada ya kukubalika kwa mfumo wa vyama vingi, alitumia muda uliobaki kuikuza CHADEMA katika mkoa wa Kigoma. Katika uchaguzi mkuu wa 1995, Dr. Kaborou alimshinda Azim Premji wa CCM na kuwa mmoja kati ya wabunge wanne wa CHADEMA wa bunge la kwanza la vyama vingi Tanzania. Hata hivyo ubunge wake huo ulipingwa mahakamani na Azim Premji na kisha Dr. Kaborou akapoteza katika uchaguzi wa marudiano. Lakini mwaka 2000 aligombea tena na kushinda. Aliwahi kuwa kiongozi wa upinzani bungeni kwa muda mfupi kabla ya kumuachia Dr, Wilbroad Slaa, naye wa CHADEMA mwaka 2003.
Mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu wa Chama - Taifa, Dr. Kaborou alipoteza ubunge kwenye uchaguzi mkuu. Na baada ya minyukano ndani ya CHADEMA, aliamua kuhamia CCM mwaka 2006 na punde akachaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Huyu ni mtu aliyependwa sana pale Kigoma na katika siasa za upinzani. Alikuwa msomi, anayeijua dunia, aliyezungumza kwa ushawishi. Aliwahi kubebwa juujuu na mashabiki wake kutoka stesheni ya reli Kigoma hadi Ujiji, umbali wa Km 8.
Ukiacha Dr. Amani Walid Kaborou, kuna Dr. Wilbroad Slaa ambaye sitakuwa na haja ya kumuelezea hapa kwani nguvu yake akiwa CHADEMA inajulikana. Lakini tunakubaliana jambo moja, kwamba kugombea Urais kwa Dr. Slaa mwaka 2010 kulikuwa sababu ya CHADEMA kupata ushindi katika majimbo mengi mwaka huo. Ni kama kugombea kwa Lowasa mwaka 2015 kulivyosaidia CHADEMA kushinda viti vingi vya wabunge na udiwani na hata kuongoza halmashauri za majiji makubwa (Dsm, Arusha, Mwanza, Mbeya) na hata manispaa kubwa kama Iringa na Moshi. Naam upepo wa Dr. Kaborou ulipita, upepo wa Dr. Slaa ulipita, upepo wa Lowasa ulipita, Je! Upepo wa Lissu utapita? Utapitaje?
Kuna watu wengi waliokuwa wakitazamwa kama mashujaa wakiwa CHADEMA lakini walipoondoka wamepuuzwa. Hawa walitazamwa kama wasaliti, waroho wa madaraka na pesa, watu wasio na misimamo, mamluki na majina yanayofanana na hayo. Je! Lissu naye anafanana na majina hayo?
Kama kuna kosa kubwa CHADEMA itafanya ni kumtazama Lissu kama hao ndugu wengine hapo juu. Nimezungumza na marafiki wengi ndani ya Chama na kuonya kuwa wakati huu ni wakati tofauti. Kinachomtofautisha Lissu na hao wengine sio ushawishi alionao, naam Lowasa alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi, na hata Slaa alikuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwa jamii kuliko Lissu (hili naweza kulitetea zaidi baadae). Kinachomtofautisha Lissu na hao wengine ni NYAKATI.
Naam, wakati Dr. Kaborou anahama chama mwaka 2006, mwenyekiti Mbowe alikuwa na miaka 2 tu kama mwenyekiti wa chama. Wakati Chacha Wangwe akipinga yanayoendelea ndani ya Chama mwaka 2008, mwenyekiti Mbowe alikiwa na miaka minne tu kama mwenyekiti. Na zaidi mwaka 2010 chama kilifanya vema zaidi kwahiyo, ya kale yakawa hayanuki.
Kati ya mwaka 2010 hadi 2015 chama kiliendelea kukua mara nyingi zaidi ingawa kulikuwa na migogoro ya hapa na pale (ni kawaida kwa taasiso zote za kisiasa) iliyopelekea kuondoka kwa Zitto Kabwe, David Kafulila, Kitila Mkumbo na wengine. Ujio wa Lowassa mwaka 2015 ulimuondoa Dr. Slaa, na hapo akabadilishwa jina na kuwa msaliti. Mafanikio makubwa ya Chama yaliyopatikana mwaka 2015 yalitusahaulisha zaidi kuhusu Dr. Slaa, na upepo wake ukawa umepita.
Je! Upepo wa Lissu nao utapita? Utapitaje?
Kwa mara ya kwanza mtu aliyeonekana kutibua hali ya hewa ndani ya Chadema anaungwa mkono na kundi kubwa la watu wenye ushawishi kwenye jamii. Watu wengi waliowatazama akina Slaa, Zitto nk wasaliti hawamtazami Lissu kama msaliti wa Chama. Na hii sio kwa sababu ya nguvu ya Lissu, no, ni kwa sababu ya mazingira yaliyopo katika siasa za leo ndani ya nchi yetu. Vituko vya CCM vya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, na uchaguzi mkuu wa 2020 ambavyo vimerudiwa tena 2024, na vinaweza kurudiwa tena 2025 vimerudisha sana morali ya wanambadiliko na kuitazama Chadema kama chama kisicho na uwezo wa kukabiliana na vituko hivyo. Chama kilichokuwa na wabunge 116, sasa kina mbunge mmoja (wa kupewa). Ingawa inajulikana fika kwamba haya ni matokeo ya 'UPUMBAVU' wa dola la Tanzania chini ya CCM, lakini pia inawapa sababu ya watu kutamani mabadiliko katika siasa za upinzani. Wapo watu wengi wanaomini Chadema haijaweza kujitetea vya kutosha dhidi ya 'UPUMBAVU WA DOLA LA TANZANIA CHINI YA CCM'. Katika mazingira hayo, Lissu ambaye anaonekana kuwa mtu wa siasa kali (radical) anaweza kuongoza jaribio la kuikabili dola la wazandiki la CCM. Sambamba na hilo, wapo wanaoamini uongozi wa Chadema uliopo umeshindwa kujabiliama na wazandiki wa CCM; Watekaji, Watesaji, Wauaji na Waharibifu wa demokrasia. Wapo pia wanaoamini baadhi ya viongozi wa Chadema wanakula CCM na kulala Chadema. Hayo yanamfanya Lissu kuwa mtu wa tofauti na wengine walionekana 'kutifuana' na Uongozi wa Chadema huko nyuma.
Naam, jaribio la kumpa Lissu jina la usaliti lilishindwa mapema baada ya ofisa wa karibu wa Mwenyekiti Mbowe, Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kufananisha kitendo cha Lissu kuchukua fomu ya uwenyekiti na uhaini, na kuahidi kumshughukia. Jaribio lingine ni lile la Yericko Nyerere la kutaka kuharibu taswira ya Lissu kwa kuandika makala ndefu yenye mambo mengi kuelezea sababu za kwanini Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Majaribio hayo mawili yamekutana na upinzani mkali, si kutoka CCM, bali ndani ya Chama na hata kwa watu wa nje ya chama ambao mara nyingi wameiunga mkono Chadema. Ni upepo tofauti.
Hitimisho!
Pamoja na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba Lissu anaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya Chadema, lakini kuna idadi kubwa ya watu - hasa wanachama wa chini wanaomuunga mkono. Na hapa niseme, watu hawa si kwamba wanamtaka zaidi Lissu la! Ni kwamba wamepoteza tumaini na hali ilivyo sasa.
Upepo wa Lissu ni tofauti na upepo wa kina Dr. Slaa. Ni upepo ambao kama utapita hautapita na Lissu peke yake, ni upepo unaoweza kukisomba na kusambaratisha chama.
Hekima ya viongozi wa Chadema waliopo madarakani, ambao wengi wao hawamuungi mkono Lissu, ndio inayoweza kukiokoa Chama au kukiacha kisombwe na upepo wa Lissu.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
Ni kweli kabisaMAJARIBIO YOTE YA KUTAKA TUNDU LISSU AONEKANE MSALITI NDANI YA CHADEMA YAMESHINDWA VIBAYA SANA.