BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Vyanzo mbalimbali ikiwemo #BBC vimeripoti kuwa Wafanyakazi wa Mashirika ya misaada kutoka maeneo ya Mashariki mwa #DRC wamesema kuna mapigano mapya kati ya Jeshi la Serikali na Waasi wa M23.
Serikali imeshutumu Waasi kwa shambulio la Machi 7, 2023 lililosababisha raia wengi kukimbia makazi yao, wakati huo huo #M23 wanasema licha ya kukubali suluhu ya amani wataendelea kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Jeshi la Congo au washirika wake.
Aidha, Serikali ya #Rwanda imekanusha kuunga mkono Waasi ambao wameteka maeneo makubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku wakitishia kuuteka Mji wa Kibiashara wa #Goma.
====================
A ceasefire has taken effect in the east of the Democratic Republic of Congo, although it is not clear whether it is being respected.
The UN Secretary General has urged the M23 rebel group to stop fighting and withdraw from captured territory.
The rebels launched fresh attacks on Congolese army positions on Monday, seizing a town and several villages.
Rwanda denies backing the M23 which has captured large swathes of territory over the past year and is threatening the regional capital Goma.
BBC