SI KWELI DR Congo: Muasi Sultan Makenga auawa

SI KWELI DR Congo: Muasi Sultan Makenga auawa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Mnamo Juni 27, 2022 kulitokea taarifa zikifafanua kuwa Sultan Makenga ameuawa baada ya Helikopta kuwashambulia. Katika Video ya YouTube iliyowekwa Juni 27, 2022 ilieleza:
"Fardc vs M23/ Rwanda: Tetesi za Kifo cha Sultani Makenga Zinaleta Hali ya Taharuki kwa Magaidi wa M23
Kulingana na mwandishi wa habari Christophe Rigaud wa Afrikarabia, kuna tetesi kubwa kuhusu kifo cha Sultani Makenga. Lakini hakuna "uthibitisho wa kuaminika kwa sasa, lakini chanzo cha usalama kimenithibitishia kifo cha Luteni Kanali Youssouf Mboneza na maafisa wengine 3 wa M23 baada ya helikopta ya FARDC kuwashambulia," mwandishi aliandika kwenye Twitter. Vyanzo vingine vimeripoti habari hiyo bila kuthibitisha, na kila wakati wakizungumzia "vyanzo vya usalama." Luteni Kanali Sultani Makenga ni kiongozi wa kijeshi wa Harakati ya Machi 23, kikundi cha waasi kilichoko katika maeneo ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Makenga ni Mutsi kwa asili na alikulia Kusini mwa Kivu. Aliwahi kupigana kwa niaba ya Front Patriotiki ya Rwanda wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda.

Taarifa hiyo licha ya kudokeza fununu zinazoelezea taarifa za kuuawa kwa General Sultan Makenga lakini inakiri kwamba taarifa hiyo haikiwa na uthibitisho wowote.

Upi ukweli kuhusu taarifa hii?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya habari na kubaini hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichothibitisha kifo cha Sultan Makenga;

Hata hivyo, JamiiForums imebaini kuwa Shirika la Habari la Sauti ya Marekani liliripoti taarfa ya Sultan Makenga kurejea Congo kuendelea mapigani mnamo Julai 5, 2022 ikiwa wiki moja tangu kiongozi huyo kudaiwa kuuawa.

Zaidi ya hayo mnamo Julai 7, 2023 ukurasa wa habari wa The News Times lilitoa taarifa ya Sultan Makenga kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mgogoro wa Congo.

Hivyo, kutokana na kuwapo kwa uthibitisho wa Sultan Makenga kuendelea na shughuli zake za kijeshi pamoja na kujitokeza kwenye mahojiano, JamiiForums inaona kuwa taarifa zilizomuhusisha kiongozi huyu na kuuawa kwenye shambulizi hazikuwa na ukweli.
Back
Top Bottom