Mwanasiasa wa chama tawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Marie-Celestin Karondwa, amepigwa hadi kufariki dunia baada ya kushiriki kipindi cha redio kilicholenga kutoa elimu kuhusu Ebola. Tukio hilo lilitokea Jumapili, Septemba 27, 2026, Mjini Butembo, Mkoa wa Kivu Kaskazini.
Karondwa, aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya UDPS mjini Butembo na msemaji wa chama hicho, alishambuliwa baada ya kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ebola.
Kwa mujibu wa Chama cha UDPS Butembo, Karondwa alipigwa, mali zake ziliporwa na nyumba yake kuchomwa moto. Karondwa baadaye alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata, chama hicho kilisema.
Tukio hilo linaongeza wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya timu zinazohusika na mwitikio wa Ebola, huku kukiwa na ukosefu wa imani miongoni mwa baadhi ya wananchi. Mlipuko huo, uliotangazwa Mei 15, umeambukiza watu 8,067 na kusababisha vifo 3,901, kwa mujibu wa takwimu za Serikali zilizotolewa Septemba 28, 2026.
Soma pia Mlipuko wa Ebola DRC: Idadi ya Waathirika Yazidi Kuongezeka Mashariki mwa Nchi
==============
A senior member of Congo's ruling party was beaten to death after taking part in a radio programme to raise awareness about the Ebola outbreak, a party representative said on Monday.
The incident happened on Sunday in Butembo, North Kivu province, which has recently become a hotspot in the ongoing Ebola outbreak.
Marie-Celestin Karondwa, acting president of the UDPS party's federal executive committee in Butembo and a party spokesperson, was attacked by residents of his neighbourhood after appearing on a radio show during which he promoted Ebola prevention measures, the UDPS federation in Butembo said in a statement.
The party said the attackers beat him, looted his belongings and set his house on fire. It was not immediately clear who carried out the attack, how many were involved or what motivated it. But the party said Karondwa was "an innocent victim for having defended the party's position on the existence of the Ebola virus disease (...) and the threat it poses to the population."
Karondwa later died from his injuries, the party said.
The mayor of Butembo did not immediately respond to a request for comment.
The incident is the latest in a series of attacks on Ebola response teams, underscoring persistent mistrust among the population.
On Saturday, armed men attacked a hand-washing checkpoint in nearby Beni territory, killing at least one person and wounding several others, a local civil society group reported.
The outbreak, declared on May 15, has infected 8,067 people and killed 3,901, according to government data released on Monday.
Source: Reuters