DR Congo: Takriban watu 28 wamefariki baada ya ndege kuanguka katika makazi ya watu

DR Congo: Takriban watu 28 wamefariki baada ya ndege kuanguka katika makazi ya watu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Watu ishirini na nane wamefariki huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kutokana na ajali ya ndege iliyokuwa imebeba watu 18 wakiwemo rubani wa 2 na abiria 16 na wengine 10 ni wakazi wa eneo ambapo ndege ilianguka

Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Goma, kwenye mtaa wa Birere wenye watu wengi karibu na mpaka wa Congo na Rwanda,
Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu wangapi walikufa na wangapi walijeruhiwa

Zoezi hilo linafanyika kwa msaada wa wananchi wa mji huo ambao waendelea kupekua nyumba za majirani zilizo angukiwa na ndege hiyo ya kampuni ya Beesyby

Kampuni hiyo imekuwa ikifanya safari zake huko Kivu kaskazini ikisafiri kati ya miji ya Goma, Butembo na Beni.

Waziri wa Afia Kivu Kakule Kanyere Moise anasema kwa sasa ni mapema kusema watu wangapi waliofariki lakini mwandishi wetu Austere Malivika alishuhudia miili kumi na sita katika sehemu ya tukio na manusura mmoja.

781A34A6-2B69-4DA5-A4EA-478E8086236C.jpeg
 
Poleni wafiwa but DRC ni moja ya nchi yenye rekodi ya kua na ndege nyinhi chakavu... Na ni nchi yenye idadi kubwa ya ajali za ndege
 
Yaani ndege zinazofanya safari ndani ya Drc, ni sawa na zile daladala za usiku zinazofanya kazi dar!!! Yaani saa 12 asubuhi, zinafungiwa, hadi saa tano usiku tena!!! Lazima ajari ziwe nyingi sana!!!
 
Mzungu mweusi ndo yupoje? Mimi nikipanda ndege dereva akiwa mweusi nakosaga amani bora awe na asili ya pemba na kiarabu ukiacha mzungu la sivyo ntasali sana.
Duh sio mchezo

Kwa hiyo hata akiwa mzungu mweusi?
 
Mzungu mweusi ndo yupoje? Mimi nikipanda ndege dereva akiwa mweusi nakosaga amani bora awe na asili ya pemba na kiarabu ukiacha mzungu la sivyo ntasali sana.

Sounds foolish, ungekuwa unaangalia aircrash investigation, usingeleta utaahira wako wa visiwani.
 
Hawa jamaa wana ndege chakavu sana za abiria na kitokana na kutokuwa na miundombinu bora inawabidi watumie tu
 
Halafu ndege zao zote made in Russia
Kuna mwaka fulani ndani ya ndege huko drc, mamba alileta kizaa zaa, alikuwa amefungwa kwenye box, la mbao, akawekwa chini ya seat, babaa akabomoa hilo box, ilikuwa mtafutano!! Wewe kuku mbuzi, kiti moto, bata mtu anasafiri nao kwenye siti tu!!!
 
Back
Top Bottom