Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
WATOTO wawili wameokolewa wakielea karibu na ufukwe wa ziwa Kivu huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku chache baada ya mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 400.
Haijabainika jinsi watoto hao wachanga walivyonusurika kwa siku tatu katika ziwa hilo, lakini mashuhuda wanasema walionekana wakiwa wanaelea.
Vijiji viwili viliathiriwa zaidi na mafuriko yaliyotokea wiki iliyopita na maiti zaidi zilipatikana kwenye tope siku ya Jumatano, na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 411. ambapo kati ya marehemu hao, 317 tayari wamezikwa.